Uchaguzi 2020 Natoa onyo la mwisho kabisa kwa Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Natoa onyo la mwisho kabisa kwa Tundu Lissu

Niko bush sehemu yenye tatizo la network, sipati habari kwa mtiririko mzuri. Ila nashauri sana kwa sasa tuko kwenye kampeni, Lisu anapaswa kufanya siasa za kupata uungwaji mkono wa umma zaidi kuliko siasa za madhila aliyopitia. Nashauri sana Lisu azungumzie mahitaji ya wananchi kwa 80%, kisha madhila yake na ya upinzani ayaongelee kwa 20% tu.

Kushinda pambano la ngumi sio uwezo wa kurusha ngumi nzito pekee, bali ni kurusha ngumi nzito zenye pointi. Ni vyema Lisu asitumie approach aliyoitumia wakati anasaka wadhamini, bali atumie approach ya kuweka mahitaji na shida za wananchi kwanza. Inatakiwa hata akishindwa awe ameacha ahadi za uchonganishi, ambazo zitawafanya kutekeleza hata kama hawapendi.

Naunga mkono hoja 💋💕
 
Magufuli hana lolote sitaki kujutia baadae akifanya ujinga wake. Hapa anasema akishinda kazi yake ya kwanza itakuwa kujenga uwanja mkubwa Dodoma. Wanadodoma wanahitaji Uwanja mkubwa au maji kila kaya ?

Pia akasema atanunua ndege mpya 5 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Sera zipo let him address hii engua ya kuhuni. Stupid na wewe muhaya nshomile, unadhani kwa uhuni huu Kajage atamtangaza. Ngoja aweke mazingira ya kutangazwa akishinda.
 
Ushakula lakini au unashinda njaa kusubiri mkeka uliobeti
 
Well Said. Tukio la risasi alichukua almost robo tatu ya muda. Tunataka atuambie kwa nini tumpe kura. Binafsi nilisema nampa kura yangu ila jana kaniangusha kabisa. Kura yangu bora nimpe Babu Rungwe.
Me hata kampen namgonjea mzee rungwe 😂😂😂nione mtu kapigwa kati kwenye sinia la walu
 
Hapo anakuambia akishinda atanunua ndege tano zingine. Tujiandae kwa miaka migumu mingine 5.Huyu hapati kura yangu. Akishinda hata akiendeleza ma ujenzi yake mimi nitajifariji kwa kusema sikumpigia kura.
Hahahah tuko pamoja
 
Watu walitegemea makubwa katika ujio wa huyu muheshimiwa asiyeshaurika kabisa. Kama angejipanga vizuri kwa hoja nzuri, Tafiti na Kuzuia hasira alikuwa na nafasi ya kushinda kwenye UCHAGUZI lakini kumbe ni hopeless kabisa.

Hivi nani anayemuandalia hotuba Lissu. Huenda anatumika.

Leo namuonya Tundu lissu kwa mara ya mwisho.

1. Jenga hoja kupitia kero za watu, Maisha ya watu na sio matatizo binafsi au ya chama chako
huwezi hamasisha watu wakuonee huruma au wakipiganie chama Jenga hoja vizuri ili watu waamini wanajipigania wao na nyie mko mbele yao tu. Sijui Kama unaelewa kirahisi. Swala la ukosefu wa Ajira ata kwa sekta zenye uhitaji mkubwa Kama afya na elimu vijijini, kunawasomi wengi mtaani na huo utakuwa mtaji wenu. Jifanyeni mnapigania haki za wakulima juu ya masaibu mengi mno wanayopitia.

Ni mengi na ukiyasema kwa kuguswa kabisa na kuonesha kuumia na kusisitiza umoja unaitajika kuushinda unyonyaji. Kusisitiza na kuwapa matumaini hakuna mtanzania mnyonge tena. Utapata support kubwa kwao. Kutolipwa kwa wakati mazao ya biashara na funga mipaka inavyoathili Bei ya mazao ya chakula Kama mahindi na Michele na vitunguu. Wape matumaini Mapya wakulima. Usifumbe, usitumie lugha ngumu, usiulize maswali andaa speach nzuri tu.

Swala la kupigwa risasi na zilizoingia mwilini ni ya kipuuzi mno kwenye kipindi hiki cha UCHAGUZI na hazisaidii kuimalisha maisha ya watu.

Watanzania tuna roho ngumuu, wewe Jenga hoja za huruma tu utapona Oct 28. Hawa watanzania ukiangusha shilingi elfu Kumi mbele ya watu ishirini akina wa kukushitua ata moja wanakuacha unaenda wanagawana miatano miatano. Wakishika mwizi wanaua, tajiri akikamatwa na polisi ata Kama hanakosa wanashangilia. Huwajui watu.

Ombeni Kura kwa kuonesha dira na matumaini Mapya na sio kulialia tu jukwaani. Nazani hujui tu binadamu ni wabinafsi. Watu wanashida zao wewe unakuja kuwaeleza shida zako ili iweje.

Jenga hoja askali mliwaweka ili kuwapigania wamekatwa. Msikubali kukosa fursa ya kusaka haki yenu ya kuchagua.

Ongelea masaibu waliyopitia wakosoaji wote waliotaka kuweka Mambo sawa wako wengi mno kama Akina Kakobe, Msisahau Gwajima, Lowasa, Viongozi wa dini na nyaraka zao, wasanii, hadi wabunge wa CCM kusini, walipojaribu kupambana bungeni juu ya fedha zao za pembejeo za korosho na Hadi Waziri mkuu alivyokoswakoswa na kuonywa. Baada ya yote hayo wote wameunga mkono juhudi mliobaki kuwasemea na kupigania haki NI yeye. Japokuwa umepitia uliyopitia. Sasa hapo wapitishe kidogo Kama dk 3 tu uliyopitia lkn hujarudi nyuma na kuwatia ujasiri kwenda pamoja. Ukweli Lissu hujui kujenga hoja za kisiasa labda za kisheria

2. Huu sio wakati wa kusema sema au kufanya vitu hovyo na kila kitu kulazimisha Sheria
Wasomi au watu wenye Akili kubwa mnashida Sana. Ongelea hoja zenye nguvu tu, zitakazoeleweka na wajinga kirahisi na hoja ngumu kueleweka au ngumu kuaminika au nyepesi kupotosheka ata kama ni ya ukweli na inamsaada mkubwa iache kabisa.

Sikuelewa kusudio la pingamizi lako. Ukiamini Raisi atakatwa na time au unataka kutuambia Lina msaada gani kwa watu. Kama unashida na Raisi huu NI wakati wa kumshitaki kupitia hoja thabiti kwa wananchi na sio Kiki za magazeti.

Wanahabari wanakosa headline inayoendana na dira na mwelekeo wako ukiwa Rais. CCM inajua siasa bwana inawachokonoa mnapandwa hasira mnaacha hoja za muda wote mnaanza kujisemea. Mna miezi miwili hubiri risasi zako tu uone ata asilimia 20 Utapata.

3. Usiunde na ondoa uadui na kila mtu. Wape ahadi na nzuri Viongozi wengi wa serikali
Mawaziri, tumia Akili kubwa. Ukishindwa kuwashawishi wafanyakazi wa imma na wa juu hutoboi. Hao ndio wasimamizi na walinzi. Askari, wanajeshi,, na wengine.

NI wakati wa kuonesha upendo na ahadi nzuri asa uhakika wa Ajira au malipo mazuri kwa Viongozi wa juu wasiopenda kutishwa. Wakurugenzi, wafanyakazi wa tume na wengine wengi.

Omba Kura za CCM pia. Hata NDANI ya CCM lazima Kuna makwazo wanahidi umoja wa kitaifa.
Kweli umeongea Fact
 
Magufuli namwita babu kufuli. Ukitaka kujua anaingia nini nenda kamuulize. Shkamoo child benz
 
Ndugu William, Unaonyesha uu Mtu mwenye Mapenzi na Nia nzuri na Tundu Lissu. Kwani Akupendae na mkweli ndiye anaye Kuonya, Kushauri na kukuonyesha makosa yako, Lakini wanokushangilia na kukusifu hata unapokosea, hao ni maadui na hawana nia nzuri.
Tokea arudi hadi leo, Lissu hajajitangaza kisiasa ila kulalamika na kumponda Magufuli, Yote hayo atapata muda na fursa, lakini huu ni wakati wa kuwavutia wapiga kura , kuwashawishi wajitokeze kwa wingi na wampigie kura, angeweza kuwapata wapiga kura wengi wa chama chake na vyama vinginevyo.

Kwa Mfano jana hapakuwa na sababu ya kutoitangaza ILANI yao Ya Uchaguzi na pia wakazungu,zia uonevu wa wagombea wao kukatwa. Jana Uongozi wa Chadema na Lissu wameudhihirishia UMMA kuwa hawana uwezo wa kufanya au kubeba Ajenda Mbili au zaidi kwa pamoja ( MULTI TASKING). Kuna wengi tunaliona hili la jana , kama mbinu za kumkwamisha TL, au kumtoa kwenye focus.
 
Na weh nawe ndio nini kutoa onyo kwa mtu mzima
Hebu tuondolee utwana na ubwana wako hapa eboh!
Ungesema hata ' Nakuagiza ufanye haya na haya eti natoa onyo.. kwani wewe ni mzazi wa Lissu
Punguzeni upumba kha
 
Huu uchaguzi badala ya kumuinua Lissu ndio anaenda kuwa exposed! Mambo yanapelekwa kimihemko sana.
 
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini Membe alikataa kumuachia agombee peke yake kwa tiketi ya Upinzani.
 
Back
Top Bottom