Uchaguzi 2020 Natoa onyo la mwisho kabisa kwa Tundu Lissu

Magufuli hana lolote sitaki kujutia baadae akifanya ujinga wake. Hapa anasema akishinda kazi yake ya kwanza itakuwa kujenga uwanja mkubwa Dodoma. Wanadodoma wanahitaji Uwanja mkubwa au maji kila kaya ?
Utakuwa hujaitendea haki nchi yako, kama unataka tufike mbali, basi Magufuli anatufaa sana mkuu.
 
Bavicha hawajakuelewa.

Ongeza volume
 
Siku upinzani ukiacha kujikite kwenye malalamiko na kujiegemeza katika sera watakua tayari kuingia Ikulu.

Siku wakigundua kwamba UNAPOKUA NA HASIRA HUTAKIWI KUTOA MAAMUZI watakua wamepevuka kujua si kila kitu unachokijua lazima umsimulie mwenzio.

NIONAVYO MIMI
Kuna uwezekano mkubwa hawa Jamaa wakaona aibu itakayowakumba 28102020 ni kubwa hivyo wakaamua kutafuta sababu za kususia Uchaguzi.

Zitto Kabwe
Alijitahidi kujenga mfumo imara wa kupata kura nyingi Ila naona ameanza kuyumbishwa na hawa wavaa magwanda ya kaki
 
KOSA KUBWA ILIKUWA KUTEUA MAJERUHI AU MANUSURA WA KIFO,KUTOKA HOSPITALI HADI JUKWAANI KUTAKA URAISI NA SIO KUUOMBA URAIS.

YEYE ANAHISI KILA MTU NCHI HII NI DADA AU KAKA YAKE WA DAMU HIVYO ANASIKITIKA SANA NDUGU YAKE KUUMIZWA.HIVYO ATAPIGIWA KURA KWA HURUMA BILA SERA.
 
Swadaktaa
 
Well Said. Tukio la risasi alichukua almost robo tatu ya muda. Tunataka atuambie kwa nini tumpe kura. Binafsi nilisema nampa kura yangu ila jana kaniangusha kabisa. Kura yangu bora nimpe Babu Rungwe.
Mnaumia sana akizungumzia madhira yaliyomsibu eh? Uzinduzi wa ilani ya CDM bado.
 
Unatoa onyo kama nani? Yaani wewe mtu wa mitandaoni ni wa kumpa onyo Lissu? Unajitambua Kweli? Lissu si saizi yako wala hawezi kujua kama kuna mtu kama wewe duniani. cha msingi kaa kwako kula ugali wa sukuma wiki ulale.Acha mboyoyo zisizo na msingi kwa Taifa.
 
Watu hata Hasheem Rungwe anawashinda.
 
Mkuu uneongea kiutu uzima.
Shida ninayoiona mimi kwa Chadema...ni kama chama hakiko pamoja kwenye hizi harakati.
Ukiangalia kwa umakini utaona uongozi kama vile umemwacha mgombea aamue mwenyewe atazungumza nini.

Upande wa mgombea(Lissu) anaonekana kama vita ya mtu mmoja, ..asiyeambilika/kushaurika.
Anayeamini katika yeye mwenyewe tu..hili ni tatizo kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…