Uchaguzi 2020 Natoa onyo la mwisho kabisa kwa Tundu Lissu


Naunga mkono hoja 💋💕
 
Magufuli hana lolote sitaki kujutia baadae akifanya ujinga wake. Hapa anasema akishinda kazi yake ya kwanza itakuwa kujenga uwanja mkubwa Dodoma. Wanadodoma wanahitaji Uwanja mkubwa au maji kila kaya ?

Pia akasema atanunua ndege mpya 5 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Sera zipo let him address hii engua ya kuhuni. Stupid na wewe muhaya nshomile, unadhani kwa uhuni huu Kajage atamtangaza. Ngoja aweke mazingira ya kutangazwa akishinda.
 
Ushakula lakini au unashinda njaa kusubiri mkeka uliobeti
 
Well Said. Tukio la risasi alichukua almost robo tatu ya muda. Tunataka atuambie kwa nini tumpe kura. Binafsi nilisema nampa kura yangu ila jana kaniangusha kabisa. Kura yangu bora nimpe Babu Rungwe.
Me hata kampen namgonjea mzee rungwe 😂😂😂nione mtu kapigwa kati kwenye sinia la walu
 
Hapo anakuambia akishinda atanunua ndege tano zingine. Tujiandae kwa miaka migumu mingine 5.Huyu hapati kura yangu. Akishinda hata akiendeleza ma ujenzi yake mimi nitajifariji kwa kusema sikumpigia kura.
Hahahah tuko pamoja
 
Kweli umeongea Fact
 
Eti natoa onyo, wewe nani? Au kwakuwa wewe ni shemeji yake Slaa basi unaona umefika mwisho wa reli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuache masihara jana lissu alikuwa chini ya kiwango sana sana leo asirudie kama alivyofanya jana ukweli lazima usemwe CCM imechokwa ila lissu asipojipanga tutaongea mengine October
 
Magufuli namwita babu kufuli. Ukitaka kujua anaingia nini nenda kamuulize. Shkamoo child benz
 
Ndugu William, Unaonyesha uu Mtu mwenye Mapenzi na Nia nzuri na Tundu Lissu. Kwani Akupendae na mkweli ndiye anaye Kuonya, Kushauri na kukuonyesha makosa yako, Lakini wanokushangilia na kukusifu hata unapokosea, hao ni maadui na hawana nia nzuri.
Tokea arudi hadi leo, Lissu hajajitangaza kisiasa ila kulalamika na kumponda Magufuli, Yote hayo atapata muda na fursa, lakini huu ni wakati wa kuwavutia wapiga kura , kuwashawishi wajitokeze kwa wingi na wampigie kura, angeweza kuwapata wapiga kura wengi wa chama chake na vyama vinginevyo.

Kwa Mfano jana hapakuwa na sababu ya kutoitangaza ILANI yao Ya Uchaguzi na pia wakazungu,zia uonevu wa wagombea wao kukatwa. Jana Uongozi wa Chadema na Lissu wameudhihirishia UMMA kuwa hawana uwezo wa kufanya au kubeba Ajenda Mbili au zaidi kwa pamoja ( MULTI TASKING). Kuna wengi tunaliona hili la jana , kama mbinu za kumkwamisha TL, au kumtoa kwenye focus.
 
Na weh nawe ndio nini kutoa onyo kwa mtu mzima
Hebu tuondolee utwana na ubwana wako hapa eboh!
Ungesema hata ' Nakuagiza ufanye haya na haya eti natoa onyo.. kwani wewe ni mzazi wa Lissu
Punguzeni upumba kha
 
Huu uchaguzi badala ya kumuinua Lissu ndio anaenda kuwa exposed! Mambo yanapelekwa kimihemko sana.
 
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini Membe alikataa kumuachia agombee peke yake kwa tiketi ya Upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…