Uchaguzi 2020 Natoa onyo la mwisho kabisa kwa Tundu Lissu

Umesahau kuweka namba ya simu

Sent from my HUAWEI VNS-L22 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umekosea kutoa neno onyo,kumbuka mh lissu kwa Sasa sio level yako mkuu ,alafu maandishi Kama aya tuwe tunaweka akiba ya maneno,kesho anaweza kuwa rais wako,na ukakosa pa kuficha uso wako,msijidanganye kwamba ccm haiwezi toka madarakani,inawezekana au haiwezekani unategemea wananchi wameamua Nini basi
 
Wewe subiri kwanza usijitingishe lissu ameshaingiza sindano subiri asukume dawa angalia sindano isije ikavunjikia kwenye mfupa
 
Huna hoja Yaani chadema waacha kulalamika juu ya hujuma za CCM kisa utasema wanalialia jukwaani? Wanaomba kura na poa lazima walalamikie faulu za CCM ikiwemo kuwatumia Polisiccm na NECCCM Tumeccm kuwadhoofisha
 
Swala la kupigwa risasi ni la kipuuziπŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
Kweli dawa inawaingia vizuri
 
CCM inaweza toka madarakani japo si 2020.

Tundu Lissu hawezi kushinda katika Uchaguzi huu.

1.Jengeni Chama Vizuri.
2.Tafuteni watu Smart wa kusimama katika Uongozi.

3 .Jengeni ofisi zenu kupitia Ruzuku mnazopata(Sio hayo Mabanda ya nguruwe tunayoyaona mtaani,Mnatukatisha tamaa).

Labda...Labda, Tunaweza wakabidhi nchi Miaka ya Mbeleni.
 
Hakuna mazuri ya CCM kwa chadema lazima wapinge vyote, acheni kufanya uchakachuaji unyanyasaji kama mnajua kuna visasi na kama mnajua hakuna vya kupingwa iweje muwe na hofu ya visasi?
 
Ofisi iliyopo ndiyo hiyo hiyo inawapeleka puta CCM mpaka kuwabambikia kesi kuwapiga risasi je? Chadema wakiwa na ghorofa 10 si mtawapiga na vifaru nyukilia? Kama mtukufu magufuli mtu muonevu mnyanyasaji mpenda visasi kawa Rais sembuse Tundu lisu mpenda haki? Hilo Banda la nguruwe unaloliona mtaani ndilo hilo hilo Polisiccm na NECCCM Tumeccm wanakesha kulihujumu kupanga uchakachuaji wizi wa kura
 
Mkuu wenda unaongea kiushabiki tu wa chama chako ,ila hapo ulipo ukweli moyo wako unashuhudia,iko ivi wengine tunaongea kimwili na kiroho zaidi 2020 Ina sufuri mbili lakini pia mbili mbili ,niishie hapo msijipe matumaini Sana mtakuja kulia na msipokua makini waweza shangaa upo mental clinic, kwa vitu vidogo ,mchezo wowote Kuna kushinda na kushindwa na ukilijua hili amini nakwambia unakua free kuanzia kiakili mpaka moyo, sawa kada
 
Lisu ni mpropokajia tangu kitambo ndio maana wenye chama wamemuacha ahenyeke peke yake
Kama kuhenyeka ni huku mbona jiwe anakutamani? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mwaka 1998 baada ya mfumo wa vyama vingi ilipaswa CCM wagawe majengo viwanja vyote kwa vyama vya upinzani kwa usawa lakini wakapora kila kitu ndiyo maana huogopa vyama vya upinzani mno, hofu yao kuu ni mali za CCM kugawanywa kwa upinzani na pili ni kashfa mbalimbali, ufisadi Ndungai kupiga bilion 12, kupiga trilion 1.5 wakamtoa CAG kafara, ununuzi wa Ndege ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge na ufisadi mkubwa kwenye miradi yote mikubwa
 
Uonevu unyanyasaji uovu wa CCM ni ajenda muhimu zaidi kwani hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu atataka kuendelea kuteseka na hayo manyanyaso
 
Wapiga kura hawatumii akili za kuvukia barabara "they know who is who '
 
Hili suala hata mimi nimeliona
Kimsingi Lissu sio muongeaji mzuri na mjenzi mzuri wa hoja hili ni tatizo la watu wenye akili nyingi,angepata watu Kama Zito ambao inaonekana huko cdm hawapo ingesaidia kuweka bond mzuri.
Lissu angejua kuelezea kirahisi hoja ya bima ya afya na kuhusisha na Hali ya umaskini wa watu ingemsaidia Sana.Kwa mfano umeme umefika karibu kila Kijiji,sasa unakuta Kuna kaya 400 lakini ni kaya 25 tu Zina umeme ,,huu ni mfano tosha kuelezea Hali mbaya ya umaskini maana kaya zote hizo zimeshindwa kulipa 27,000 ya umeme,watu Kama Hawa eti unawaambia tumenunua ndege.Na mengine mengi ambayo ni ya kawaida Ila tu mtu ujue kuyanyumbua na uwe na takwimu
 
Uonevu unyanyasaji uovu wa CCM ni ajenda muhimu zaidi kwani hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu atataka kuendelea kuteseka na hayo manyanyaso
Kwani humuyajui kama yamemikuta, inabidi muelezwe kwa marudio na kila mkutano wa Lissu. Nasi iko shida kubwa ya kumbukumbu. Mtu unatakiwa ujue utakaye mpigia kura , muda vyama shindani vitangazapo wagombea.
 
Lisu ni mpropokajia tangu kitambo ndio maana wenye chama wamemuacha ahenyeke peke yake
Nani kamuachia chama peke yake? weee ndiyo unaropoka uzushi, kama Lisu angekuwa peke yake mngehangaika kumhujumu kupitia NECCCM Tumeccm na Polisiccm vyombo binafsi vya CCM, kipindi hiki CCM wapo busy kuwahujumu chadema kwa kila hali lazima wagombea wengi wasalie majimboni kupambana na hujuma za CCM kwa msaada wa Polisiccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…