Naufananisha Uwanja wa Ndege wa Chato na Ofisi ya Spika ya Urambo

Kweli mkuu wakati Mobutu Sese Seko anajenga uwanja wa ndege kijijini kwake watu walikuwa na wivu kama huu, leo uwanja unaingiza pesa nyingi za kigeni na kuchangia pato la taifa, kwani watalii mbali mbali wamekuwa wakimiminika kwenda kuyashangaa magofu na kujiuliza aliwezaje kujenga uwanja kama huo katikati ya lindi la umasikini wa wananchi wake. View attachment 629913 View attachment 629914
Teh teh teh teh
 
Mbaya zaidi Kampuni inayofanya ujenzi ni YAKE MWENYEWE.. MAYANGA CONTRACTORS ENGINEERING LTD...
Ni ile ile iliyofanya upanuzi wa Barabara inayotaka Mwanza Airport..
Aibu kabisa.

Labda pasi ndefu ili ikimaliza ikapewe wa mwanza na vingine si unajua fursa za kibiashara za viongozi wa kiafrika. Ukienda mbali hizi ndio sababu za wao kuja kung'ang'ania madarakani ili na kampuni ziendelee kuishi.

Utashangaa saa nyingine hata bomba la mafuta wameshatia mikono yao.
 
Hata kama ni 'Mtu kwao',hii sasa imezidi. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa,Hayati Samwel Sitta alianzisha na kusimamia ujenzi wa Ofisi ya Spika huko Urambo,Tabora. Nyumbani na jimboni kwake. Ofisi ikajengwa.

Sasa unajengwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa huko Chato,Geita. Nyumbani na lililokuwa jimbo la Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM,Dr. John Pombe Magufuli. Uwanja umeshaanza kujengwa na ujenzi umeshika kasi.

Ofisi ya Spika kule Urambo,kama ulivyo Uwanja wa Ndege wa Chato,ilijengewa hoja na kutetewa na Wabunge wetu wa CCM. Kwasasa,haijulikani Ofisi ile ya Urambo inatumikaje na inatumika na nani. Labda Spika Ndugai huwa anaitumia.

Mambo ya Urambo yaweza kujirudia Chato. Hii ndiyo courtesy begins at home? Urambo=Chato?

Bunduki za nini tena jamani katika kujenga hoja!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Kibiti,Pwani)

WanaCCM mlichotuletea mnakijua wenyewe ila mtatulipa watanzania kwa u............p.............................z...........i huu mliotuletea
 
Mbaya zaidi Kampuni inayofanya ujenzi ni YAKE MWENYEWE.. MAYANGA CONTRACTORS ENGINEERING LTD...
Ni ile ile iliyofanya upanuzi wa Barabara inayotaka Mwanza Airport..
Aibu kabisa.
.

huo uwanja tu hauna faida kwa jamii... ila hiyo kuweka kampuni yake ni kashfa nyingine... TAKUKURU mko wapi...
 
mkuu kuna chochote unajua kuhusu mmiliki HALISI wa kwanza wa hii kamuni..

hii ni kashfa kubwa sana..

hata ikiwa wamebadilisha profile details hawawezi kubadilisha taarifa za wamiliki kule Brela.
 
Hata kama ni 'Mtu kwao',hii sasa imezidi. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa,Hayati Samwel Sitta alianzisha na kusimamia ujenzi wa Ofisi ya Spika huko Urambo,Tabora. Nyumbani na jimboni kwake. Ofisi ikajengwa.

Sasa unajengwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa huko Chato,Geita. Nyumbani na lililokuwa jimbo la Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM,Dr. John Pombe Magufuli. Uwanja umeshaanza kujengwa na ujenzi umeshika kasi.

Ofisi ya Spika kule Urambo,kama ulivyo Uwanja wa Ndege wa Chato,ilijengewa hoja na kutetewa na Wabunge wetu wa CCM. Kwasasa,haijulikani Ofisi ile ya Urambo inatumikaje na inatumika na nani. Labda Spika Ndugai huwa anaitumia.

Mambo ya Urambo yaweza kujirudia Chato. Hii ndiyo courtesy begins at home? Urambo=Chato?

Bunduki za nini tena jamani katika kujenga hoja!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Kibiti,Pwani)
Hivi wewe ni raia wa Tanzania au ni mgeni? Kila Rais uwa anaangalia kwao. Mwalimu Nyerere alitoa kipaumbele kwa watu kutoka mkoani kwake kuwa na nafasi nyingi jeshini, Mkapa kajenga daraja kubwa kwao, Kikwete kajenga bandari kwao na sasa huyu wa sasa amejenga uwanja wa ndege kwao Chato. Hata kama mimi ningekuwa Rais leo hii, ni wazi kwamba ningeweza kuweka au kujenga kitu chochote cha maana nyumbani kwetu. Dunia nzima, asilimia kubwa ya marais uwa wanawekeza nyumbani kwao. Sasa sijui wewe ni kwa nini unashangaa leo!
 
Mbaya zaidi Kampuni inayofanya ujenzi ni YAKE MWENYEWE.. MAYANGA CONTRACTORS ENGINEERING LTD...
Ni ile ile iliyofanya upanuzi wa Barabara inayotaka Mwanza Airport..
Aibu kabisa.
Jamani jamani!! Kama Ni kweli Basi nchi inakuwa plundered
 
Hata kama ni 'Mtu kwao',hii sasa imezidi. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa,Hayati Samwel Sitta alianzisha na kusimamia ujenzi wa Ofisi ya Spika huko Urambo,Tabora. Nyumbani na jimboni kwake. Ofisi ikajengwa.

Sasa unajengwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa huko Chato,Geita. Nyumbani na lililokuwa jimbo la Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM,Dr. John Pombe Magufuli. Uwanja umeshaanza kujengwa na ujenzi umeshika kasi.

Ofisi ya Spika kule Urambo,kama ulivyo Uwanja wa Ndege wa Chato,ilijengewa hoja na kutetewa na Wabunge wetu wa CCM. Kwasasa,haijulikani Ofisi ile ya Urambo inatumikaje na inatumika na nani. Labda Spika Ndugai huwa anaitumia.

Mambo ya Urambo yaweza kujirudia Chato. Hii ndiyo courtesy begins at home? Urambo=Chato?

Bunduki za nini tena jamani katika kujenga hoja!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Kibiti,Pwani)
Usiseme kwa sauti, wasiojulikana wapo karibu nawe.
 
Anataka wageni wamfuate chato wapande bombadia na kulala kwenye hoteli zake.
 
Kweli mkuu wakati Mobutu Sese Seko anajenga uwanja wa ndege kijijini kwake watu walikuwa na wivu kama huu, leo uwanja unaingiza pesa nyingi za kigeni na kuchangia pato la taifa, kwani watalii mbali mbali wamekuwa wakimiminika kwenda kuyashangaa magofu na kujiuliza aliwezaje kujenga uwanja kama huo katikati ya lindi la umasikini wa wananchi wake. View attachment 629913 View attachment 629914
Mkuu hii fasihi imekaa vema wachache watakuelewa ......
 
Back
Top Bottom