Naufunga mjadala: Zuchu ni mwandishi bora wa nyimbo kuliko Lady Jaydee

Hivi hako kamdomo anakabinuaga au ndo alivyo huyu mrembo?
 
Huyu si walitaka kampusua viatu vya kichwani majuzi hapa?
 
Nashauri tusitumie Matusi, Lugha ya kuudhi, udhalilishaji wala kuwachapa viboko Vijana wa miaka ya 2000 mpaka sasa. Tuwasaidie wajue Muziki umetoka wapi na kwa nini Wasanii wa zamani ni Bora kuliko sasa. Si Lady Jay Dee tu uliyemtaja kwa kebehi; Tafuta Kizazi chote cha akina Dully Sykes, K Sal, Daz Nundaz, Prof Jizeee, Baba Tunda na AsanteSana kutoka Misufini Moro, Mtoto wa Chemba Squad Noora -Mez B wa Area C bila kumsahau Mkali wangu wa Free style wa muda wote Cowboy Ngwea, Inspector Haroun Babuuu, Juma Nature Kiroboto, Mkongwe wa game Sugu, Solo Thang, TID wa Zeze, Wagosi wa Kaya na Kesi ya Mkoa, Chid Benzinoo, East Coast ya Mwana FA -AY-King Crazy GK, Pauline Zongo nk, Mandojo na Domokaya ...Taja Vipaji vyote vya zamani halafu fananisha na muziki wenu wa sasa UTAELEWA KWA NINI BONGO FLEVA ilishakufa, tunasikiliza muziki ili mradi siku ziende. Mkongwe Master J aliwahi kusema, itakuwa fedheha kubishana na Kijana wa sasa ambaye anamuuliza 'Master J ulifanya nini enzi zako?'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…