Naufunga mjadala: Zuchu ni mwandishi bora wa nyimbo kuliko Lady Jaydee

Naufunga mjadala: Zuchu ni mwandishi bora wa nyimbo kuliko Lady Jaydee


Kwenye pen game hakuna msanii wa kike wa bongofleva amewahi kufikia uwezo wa Zuchu toka bongofleva izaliwe nasema hakuna.

Jide ni msanii mkali, anauwezo mkubwa kafanya hitsong nyingi namheshimu kwa ilo ila huu mjadala nimeuona uko kuwa Jide anaweza andika kumzidi Zuchu haupo sahihi.

Jide ni mkongwe ila ngoma nyingi ameandikiwa, Zuchu 97% ya ngoma zake anaandika mwenyewe.

Nafikiri mnaona uhandishi wa Zuchu hata wasanii wa kiume wengi hawamuwezi.

Nyimbo kama Raha, Kwaru, Nisamehe, Naringa ni uhandishi wa kiwango cha juu sana cha sanaa.

Huu mjadala usiendelee popote nimeumaliza rasmi.
Je Zuchu anaweza kusimama mwenyewe na uandishi bila Diamond na WCB?
 
Binafsi nilikuwa sidhani kama Zuchu ana andika mwenyewe nyimbo zake
Amezungukwa na waimba taarabu kuanzia mama yake na hawa watu kwenye uandishi ni balaaaa
Nenda youtube andika Baby Zuchu feat Mzazizo wimbo sijui unaitwa Dad nifundishe. Hana uwezo huo aisee maana kutunga, kuandika na kuimba kwa wakati mmoja si mchezo japo kipaji cha kuimba anacho sana
 
Zamani hapakuwepo na sababu ya kuzuia matumizi ya bangi kwani watumiaji walikuwa wakivuta pale wanapokuwa wanaelekea kufanya kazi zinazohitaji matumizi ya nguvu nyingi na muda mwingi,akianza kulima saa moja asubuhi atapumzika saa kumi na moja baada ya bangi kumuisha kichwani.

Ila sasa hivi serikali ina sababu nyiiiiingi za kuzuia matumizi ya bangi ikiwemo hii ya watumiaji wake kuvuta bangi ili waje kutoa maoni tena mbaya zaidi kwa kuandika.
 
Jay Dee si kumlinganisha na Zuchu.
Jay Dee huyo anamzaa huyo Zuchu, heshimu amekaa kwenye game muda wote huo na bado anapambana na watoto wa 2000s.

Kitu ambacho hatuna uhakika Zuchu atafika hapo...

Kama ulishawahi ingia shows za Jay Dee utakiri Zuchu hawezi kufanya live performance kwa kuimba kama Jay Dee....
Kwenye kipaji jide amemuacha sana Zuchu ila mtoa mada kazungumzia uandishi
 
Yes nami naongelea uandishi angalia hata siku hazigandi ni kama Version ya NARINGA Kwa sasa

Angalia WANGU aliyopiga na Byser mule Jide alitulia kuandika
Jide mara nyingi anaandikiwaga naamewahi kukiri domokaya ni moja kati ya mwandishi wake tofauti na Zuchu anaandika mwenyewe kwenye hili namuunga mkono mtoa mada but overall ukizungumzia kuhusu ubora wa kuimba Jide yupo by far zaidi ya Zuchu
 
Binafsi nilikuwa sidhani kama Zuchu ana andika mwenyewe nyimbo zake
Amezungukwa na waimba taarabu kuanzia mama yake na hawa watu kwenye uandishi ni balaaaa
Mkuu, shikilia hapo sasa, kama unataka kufahamu anachokifanya Zuchu;
  • Mixing ya taarabu na singeli
  • Boosting ya matusi
  • Sauti inasaidiwa na vyombo

Show ya kwanza ya Jide naudhuria pale Diamond Jibilee, 2001, imeandaliwa na Clouds, nilipata wasaa wa kukaa naye meza moja aisee; itoshe kusema,
- Mleta mada anatafuta mileage kwenye thread yake na si vinginevyo!
 
Back
Top Bottom