Naufunga mjadala: Zuchu ni mwandishi bora wa nyimbo kuliko Lady Jaydee

Je Zuchu anaweza kusimama mwenyewe na uandishi bila Diamond na WCB?
 
Binafsi nilikuwa sidhani kama Zuchu ana andika mwenyewe nyimbo zake
Amezungukwa na waimba taarabu kuanzia mama yake na hawa watu kwenye uandishi ni balaaaa
Nenda youtube andika Baby Zuchu feat Mzazizo wimbo sijui unaitwa Dad nifundishe. Hana uwezo huo aisee maana kutunga, kuandika na kuimba kwa wakati mmoja si mchezo japo kipaji cha kuimba anacho sana
 
Zamani hapakuwepo na sababu ya kuzuia matumizi ya bangi kwani watumiaji walikuwa wakivuta pale wanapokuwa wanaelekea kufanya kazi zinazohitaji matumizi ya nguvu nyingi na muda mwingi,akianza kulima saa moja asubuhi atapumzika saa kumi na moja baada ya bangi kumuisha kichwani.

Ila sasa hivi serikali ina sababu nyiiiiingi za kuzuia matumizi ya bangi ikiwemo hii ya watumiaji wake kuvuta bangi ili waje kutoa maoni tena mbaya zaidi kwa kuandika.
 
Kwenye kipaji jide amemuacha sana Zuchu ila mtoa mada kazungumzia uandishi
 
Yes nami naongelea uandishi angalia hata siku hazigandi ni kama Version ya NARINGA Kwa sasa

Angalia WANGU aliyopiga na Byser mule Jide alitulia kuandika
Jide mara nyingi anaandikiwaga naamewahi kukiri domokaya ni moja kati ya mwandishi wake tofauti na Zuchu anaandika mwenyewe kwenye hili namuunga mkono mtoa mada but overall ukizungumzia kuhusu ubora wa kuimba Jide yupo by far zaidi ya Zuchu
 
Binafsi nilikuwa sidhani kama Zuchu ana andika mwenyewe nyimbo zake
Amezungukwa na waimba taarabu kuanzia mama yake na hawa watu kwenye uandishi ni balaaaa
Mkuu, shikilia hapo sasa, kama unataka kufahamu anachokifanya Zuchu;
  • Mixing ya taarabu na singeli
  • Boosting ya matusi
  • Sauti inasaidiwa na vyombo

Show ya kwanza ya Jide naudhuria pale Diamond Jibilee, 2001, imeandaliwa na Clouds, nilipata wasaa wa kukaa naye meza moja aisee; itoshe kusema,
- Mleta mada anatafuta mileage kwenye thread yake na si vinginevyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…