Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

That is my point, hizi number sio za bahati mbaya. Ila ni bahati mbaya kwamba kwa hizi numbers, watafeli kabla ya kuanza. 29K Dar mpaka Moro ni anasa.
Sahihi lakini nadhani wametumia negotiation skills kwamba wameanza na dau la juu ili wanapojadiliana na walaji basi wapate bei reasonable kwa pande zote mbili.
 
Sahihi lakini nadhani wametumia negotiation skills kwamba wameanza na dau la juu ili wanapojadiliana na walaji basi wapate bei reasonable kwa pande zote mbili.
Ngoja tuone, lakini wakija na bei ambazo sio rafiki, Abood ataendelea kujaza mabasi ya Dar Moro, na Shabiby ataendelea kutawala Dar Dom
 
Yaani treni ya kusimama hapa na hapa ndo nauli iwe kubwa namna hii! kwani hiyo reli mmejenga kwa pesa zenu? treni mmenunua kwa pesa zenu? hovyo sana....
 
Ni kitu gani ambacho ni hindrance ya mtu kukaa point A na kufanya Kazi point B..., Kama kuna usafiri unadhani kuna shida gani ya mtu kukaa popote pale na hii inapunguza population density kubwa sehemu moja
Mawazo yako ni sahihi Sana Mkuu. Anayekubishia Hana uelewa mpana wa unachoongelea. Kazi zinazoweza kufanywa Dar huku Mtu akiishi Morogoro ni nyingi kama Mtu atakuwa na uhakika wa usafiri na gharama nafuu Kwa mwezi. Kwa usafiri huu huu wa dala dala watu wanaishi Kibaha Kwa Mathias na wanafundisha Dar city centre.
 
Viongozi wanamiliki m bus ya mikoani, waliowekeza huko ni lazima washinikize nauli za treni ziwe juu, ili wasije pata hasara kwenye uwekezaji wao... maana mabus wanayo mengi na bdo wanasubiri return
 
Nakumbuka nilikuwepo kwenye uzinduzi wa ujenzi wa hiii reli,nakumbuka maneno ya hayati Magufuli,

Alisema anataka reli hii iwasaidie wafanya biashara wadogo ,akatoa mfano wa mtu anatoa mchicha morogoro anakuja kuuza kariakoooo Kisha anarudi zake Moro,

Sasa Kwa bei hiii kweli mm muuza mchicha ngerengere naweza kumudu hiii gharama kweli,RIP MAGUFULI .

Ninavyowajua ccm shida wameianzisha wao hlf mother of the nation ataitatua hlf Kila mtu atafurahia na kumpamba kua ni rais ni msikivu bc watampost na kumuona shujaaa.

Aliyeturoga wabongo cjui no nani ,bb wa Mbinguni utusamehe
 
TRC inatakiwa ijiendeshe kibiashara. Wakichaji nauli ya 6,000 hiyo faida itatoka wapi?! Labda serikali ikubali kufidia.
Kujiendesha kibiashara ndio bei inatakiwa iwe sawa na ya basi au chini kidogo which is possible. Hio bei ya elfu 24,000 ni ya kipigaji. Wameshindwa kabisa wangeiset kwenye 12,000 sababu umeme ni cheaper than diesel.
 
Yaani hadi nimemkumbuka jpm.Ukilinganisha nauli za sgr ya Kenya na naijeria unaona kabisa nauli za Tanzania ni Mara tatu ya zile za Kenya na nigeria na kwa umbali huo huo.Hii inchi imringiliwa na mafisadi
Tatizo tz gharama za umeme ni juu sana
 
Kujiendesha kibiashara ndio bei inatakiwa iwe sawa na ya basi au chini kidogo which is possible. Hio bei ya elfu 24,000 ni ya kipigaji. Wameshindwa kabisa wangeiset kwenye 12,000 sababu umeme ni cheaper than diesel.
Weee, sio kwa tz, waulize uwanja wa jamhuri Dodoma watakupa majibu, pale kwa mechi moja ya usiku wakitumia umeme ni sh mil4 wakati wakitumia diesel ni mil2
 
Weee, sio kwa tz, waulize uwanja wa jamhuri Dodoma watakupa majibu, pale kwa mechi moja ya usiku wakitumia umeme ni sh mil4 wakati wakitumia diesel ni mil2
Kama ni hivi ni hatari kubwa.
 
Waweke 15k ntapanda ila 24, napanda kimbinyiko napitiliza Dodoma
 
Pumbavu kweli wewe nauli ndogo wakati kuna watu waliiba billion 3 wako segerea. Basi moja inabeba watu si chini ya 350 during rush hours. Nauli ndogo ni 750. Per trip ni 262,500 hio ya kuishia Kimara tu. Chukulia basi kumi zifanye mzunguko huo mara 6 kuanzia saa 10 jioni hadi saa 3 usiku.

Roughly 262,500x10x6=15,750,000 hio ni Gerezani - Kimara one way hujahesabia kurudi. Ukiweka nenda rudi manaake unazungumzia 25M.

Kivukoni-Kimara nako upate 15,750,000 one way. Ukiweka nenda rudi maanake unazungumzia 30M kwa traffic ya ferry.

Hapo sijagusa ya mbezi mwisho ambayo ni 400x350=140,000
Ukiweka mabasi 10 yaende 6 trip kila moja ni 140,000x10x6 =8,400,000 hio ni one way Kimara-Mbezi tu during rush hours. Ukiweka 2 way maana yake inaweza gonga 12M.

Sijazungumzia less profitable routes kama Moroco, Muhimbili na Mwenge. Tuchukulie zote combined two ways zilete 23M tu during rush hours.

Twende kwenye hesabu ya jumla sasa.
Kwa masaa 5 tu ya jioni kuanzia saa 10.

Kimara-Gerezani: 25M
Kivukoni-Kimara: 30M
Kimara-Mbezi: 12M
Muhimbili-Morroco-Mwenge: 23M
SUB Totals================90M

Routes asubuhi: 70M
Routes jioni: 90M
TOTAL================160M

EXPENSES
FUEL. 20M
MISC. 5M (25)

NET==================135M

Humo una justify vipi kwamba umeshindwa nunua basi? Hio ni hesabu ya siku tu. Fanya kwa mwezi mzima utagundua kuwa hizo basi zinaweza generate 4.05B ukitoa mishahara ya kulipa staff wote, maintanance na vipuri utagundua the company makes around 2.5 Billions each month on average.

Basi moja la kichina likizidi sana ni 300M na hununui kila siku. Ukimeki kila mwaka useme ununue 10 tu kwa hio income inashindikanaje? Mwendokasi unauliwa na ufisadi. Msimamizi mzuri wa mradi hayupo wamekabidhiana wezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…