Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

USAFIRISHAJI: Leo Desemba 8, 2023 Watumiaji wa huduma za Usafiri za Mabasi ya Masafa Marefu (Mabasi ya Mikoni) na Mafupi (Daladala) wanakutana na gharama mpya za Nauli.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), nauli za Mabasi yote zimepanda baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Watoa Huduma na Wadau wa Usafiri (Wananchi).
Hawakushirikishwa,
Walisikizishwa!!
 
Gharama za uendeshaji ziko juu sanaa.....mafuta yamepanda sana spare ndio usiguse....nauli ilitakiwa ipande mwaka sasa....mafuta yamepanda mwaka sasa
Ila mishahara inaongezwa 12000 kwa mwaka,wafanyakazi mtafika mmechoka sana,motivation speaker unategemeaje mshahara?
 
USAFIRISHAJI: Leo Desemba 8, 2023 Watumiaji wa huduma za Usafiri za Mabasi ya Masafa Marefu (Mabasi ya Mikoni) na Mafupi (Daladala) wanakutana na gharama mpya za Nauli.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), nauli za Mabasi yote zimepanda baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Watoa Huduma na Wadau wa Usafiri (Wananchi).
Sisi tunatumia STM , hivyo kwani mlikuwa mnalipa kiasi gani?
Kama imepanda kwa chini ya mia tatu sasa mnalalamika nini?
Naona sawa tu, vipuli navyo vimepanda bei lakini kumbuka SHUJAA aliruhusu kila gari litoe hela ya ku-brashi viatu, hivyo nao wanapata kwenye hizo nauli.

#Asiyetaka kulipa ahamie Burundi.
#Asiyetaka kulipa apige mbizi.
 
Haya mambo Mama anayafanya ili kutuamsha wananchi kuwa nyinyiemu siyo chama cha kukichagua uchaguzi ujao lkn utashangaa kinachaguliwa hiki chama kimeshachoka wakuu tukipumzishe kijipange upya
 
mafuta yanashuka bei nauli zinapanda.

aise
 
1000005805.jpg
 
Mafuta pamoja na gharama nyingine za uendeshaji zinapopanda basi huwa inakuwa rahisi sana kupandisha bei, ila pale mambo yanaporudi kuwa sawa huwa hatusikii habari za bei za awali kurudi.
Gharama za maisha zinapanda na Huwa hazishuki ndio mfumo wa Maisha Duniani kote.
 
Sawa tumekusikia Mmiliki wa mabasi.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom