Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Nauli mpya za Mabasi zimeanza kutumika, vipi Mdau ulishirikishwa kupanga nauli hizo?

Yaani nikionaga haka kapicha huwa natukana kimoyo moyo. Kwanini kusiwe na board inayofuatilia utendaji wa hawa wakuu wa idara mbalimbali au ndio mwendo wa kulindana kwasababu wote wanatoka kwenye duka moja?
Kama umeshirikisha na utandawaz huu mbona wananchi hao hao hawana habari? Kwanini wanalalamika sasa?
Nyambafff......
 
Tunaiomba mamlaka husika kulitizama hili kwani vigezo vilivyotumika havifahamiki ukizingatia mafuta yameshuka bei kwa shs 200/-

MAMLAKA HUSIKA USAIDIENI UMMA HUU WA WANYONGE,SHUSHENI NAULI NA ONGEZENI SHS 50/- KWA NAULI ZA MIJINI, INAUMIZA MNO.
#Based on town trips!
Na sio nauli / safari za mikoani.
Kila siku tunalia unyonge unyonge.
Si tuache kusafiri?

Hao wasafirishaji wako na mikopo mikubwa ya magari.
Vipuli kodi juu, wataendeshaje hizo biashara na kulipa mikopo?

Unyonge na uhalisia...unyonge hauna nafasi.

Tanzania ina watu legelege na kutska huruma mchana kutwa.
Ukiona wenye magari wanafaidi nawe pambana ununue bus uanze usafirishaji
 
Tutetee walio wengi, mbona kwenye sukari tulipiga kelele, shughuli nyingi za mnyonge ni za kuangaika huku na kule na pengine asirudi na chochote!
 
Tutetee walio wengi, mbona kwenye sukari tulipiga kelele, shughuli nyingi za mnyonge ni za kuangaika huku na kule na pengine asirudi na chochote!
Dunia haiko hivyo mkuu, tunazidi kuleta siasa kwenye masuala nyeti.

Unyonge wako hauna uhusisno na mtu mwenye mķopo mkubwa bank akanunua mabus halafu ukamdhibiti kwenye nauli.

Kuwa na bus sio utajiri bali huo nao ni ujasiria mali.

Mbona wauza mazao na mitumba hawadhibitiwi bei?

Tunawakandamiza na kuwafilisi watoa huduma za usafiri.

Kumbuka nje ya siku za wanafunzi kurudi shule na msimu wa mwisho na mwanzo wa mwaka wenye abiria wengi, wakati uliosalia hakuna abiria mabus yapo tupu je watajiendesha je?

Mimi sina basi lkn naiona taabu yao.
 
Ccm mbele kwa mbele,wacha waisome namba eee waisome namba ccm mbele kwa mbelee,rudia kiitikio x 5.
 
1. Umeme haushikiki
2 kodi za nyumba hadi vibanda
vya akina bibi huko bush
3. Kodi za miamala ndo usiseme
4. Leo nauli imeenda juu.
5. Mikopo huko nje ni kila siku
6. Mafuta yamepanda kwa zaidi
ya 50%
7. Wenye biashara ndogo vijijini
ni mateso kwa kodi

CHA AJABU SASA
1. Tangu Oktoba shule hazipati
ruzuku ya matumizi.
2. Umeme umezidi kuwa tatizo
3. Huko hospitali huduma
zimezidi kuwa janga
4. Nyongeza ya mshahara ni
usanii mtupu.
5.Bei za bidhaa zinazidi kupaa.
6. Nchi imegawanyika kati ya
wenye nacho na wasio

Kodi zetu zinaenda wapi?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom