Nauli ya Zanzibar kuwa Tsh 25,000 vigezo gani vimetumika?

...Labda ni kwa Sababu unakwenda 'Nchi' nyingine!
 
Biashara Kama haina ushindani hiyo ni fursa wenye uwezo wa kuweka vyombo vya usafiri lazima wanufaike ila kukiwa na ushindan mbona naul itarud kawaida tu
 
Kuna maeneo mengine barabara zipo hovyo sana. So nadhani hili nalo linachangia
 
Mi napandaga VIP
 
Jana nimemkatia mtu v.i.p elf 35 Ni dkt alikwenda kwenye semina
Ni ghli Sana sijapenda na akuna alternative au washindani wengi ktk hyo viasha na muda wa boti Ni saa moja saa sita .na saa kumi

Kampuni Ni mbil tu Zanzibar feri na Kilimanjaro expres
 

Hiyo 35,000 sio VIP, ni Business Class. VIP 60,000 na Royal 80,000 Kwa Kilimanjaro 7.
 
Tumieni hii fursa mnayojipima pesa za mgao mjenge daraja hapo yaheee....
 
Fleet ya Azam Marine ni boti aina ya Catamaran ambazo zinarange kati ya bilioni 8 hadi 10 plus kila moja. Azam wanazo 8 kwa info nilizo nazo sasa. Nadhani cost zinaanzia hapo.

Pia gharama za uendeshaji wa boti ni kubwa sana ukilinganisha na mabasi. Unahitaji captain, wasaidizi na watu wa mifumo ambao mishahara yao ni mikubwa ukilinganisha na mabasi. Hapo bado hujaweka wahudumu wa ndani ya boti yenyewe.

Yacht binafsi inagharimu kwa kawaida asilimia 10 ya thamani yake kwa mwaka kwenye uendeshaji ila kwa kuwa za Azam ni za biashara so inaweza kuwa tofauti kidogo.

Moja ya Catamaran boat wanazotumia Azam Marine: V2V Empress Passenger Ferry for sale - YachtWorld
 
Kama unaona ni nyingi piga mbizi tuu mkuu
 
Maji chumvi ndugu yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…