Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Kuna mtu anahoji ni maono gani aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere.

Hiki kiswahili tunachotumia katika mijadala humu JF ni sehemu ya maono ya Mwalimu Nyerere, alihakikisha kila tarafa ya Tanzania kiswahili kinakuwa ni lugha ya mawasiliano. Hayo ni maono kwani yamechangia katika hii amani na umoja tulivyonavyo leo hii.

Malema mwanasiasa wa Afrika ya Kusini anapigia debe Afrika nzima kiswahili kiwe ni lugha ya mawasiliano ili tuweze kuwa na umoja wa bara zima ambao utatupatia urahisi wa sisi kwa sisi kuweza kuwasiliana na kuwa na bara moja lenye nguvu za kiuchumi.

Hayo ni maono ya Mwalimu Nyerere ya enzi hizo za awamu ya kwanza.
 
Walitaifisha kutokana na presha ya waliokuwa chini yao katika suala la kiuongozi.

Baada ya uhuru waingereza walimwambia Nyerere waijenge Kariakoo na sehemu kubwa ya jiji la Dar ili liwe ni jiji lenye kutazamika kimataifa, wazee wa kiswahili waliokuwa na nyumba zao Kariakoo walimbishia Nyerere pamoja na hao wazungu.

Waliwataka waingereza waondoke haraka bila hata ya kutimiza hiyo azma waliyomwambia Mwalimu Nyerere. Miaka mingi baadae watoto wa hao wazee wamekuja kuuza nyumba zile zile ambazo baba zao walishauriwa zijengwe upya kwa ajili ya kuwa na jiji la Dar lenye muonekano mzuri.

Hatuwezi kujua ni akili zipi haswa alizokuwa nazo Nyerere miaka hiyo ya awamu ya kwanza. Tukumbuke kielimu tulikuwa bado tupo nyuma sana. Mwalimu alikuwa na wigo mdogo wa washauri miaka ile ya uhuru.
 
Sunguratex, Mwatex, Mutex, UFI, Tamco, Tanganyika Packers na vingine vingi. Awamu zilizofuata ziliviua viwanda vyote japo ni kwa sababu ya presha ya IMF.
Kiwanda cha Tanganyika packers kilijengwa na mkoloni sawa na Willimson Diamond,Shirika la Usagishaji na Mazao N.M.C,Mamraka ya bandari, Tanzani Railways kuanzia Meli,Gari Mosh, Mabasi,Mpaka Malori,Posta na Simu,
Kiujumla tulirithi vitu vingi sana kutoka kwa mkoloni lakini tulishindwa kuviendesha,Sawa na kusema Africa pamoja na Tanzania,zingekubali uhuru wa bendera lakini wasingemfukuza mkoloni wangewachia wabaki kumiliki njia kuu za uchumi wakabaki wakusanyaji kodi tungekuwa mbali sana

,Nimetembelea inchi mbalimbali za Africa,utaona kwa macho yako uwekezaje waliofanya wakoloni ni tofauti walioendereza wale waliokuja kujiita wazalendo
Nitakupa mfano wa inchi moja inaitwa Mozambique, Mreno aliijenga vizuri sana kuanzia Miji,Mabarabara na kila kitu,Vita vya kupigania Uhuru vilipoisha chama cha Frelimo na selikali iliyoingia madarakani imeshindwa hata kujenga mita moja ya barabara na miji,kuendeleza pale alipoishia mkoloni,
Nenda Botswana,Namibia,South Africa, Angola,Zimbabwe, utaiona akili kubwa ya Mzungu iliyotumiaka jinsi miji yao ilivyo mizuri
 
K
Kina Kambona walimshauri vizuri,lakini wanasema alikuwa hashauliki
 
Na mama pia nchi imemshinda hiii
 
K

Kina Kambona walimshauri vizuri,lakini wanasema alikuwa hashauliki
Alishaurika na alipenda sana mijadala. Ndiye aliyeanzisha msemo wa 'hoja haipigwi virungu'

Pia alitumia maneno haya ' nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu'.

Suala la kina Kambona ni binafsi kwa maana ya ugomvi wa Mwalimu na Kambona, mafahari wawili.
 
Nchi ilitopea kwenye umasikini wa kutisha, alinusulika kupinduliwa mara mbili, yeye ndie muasisi wa kuzigeuza TISS na JWTZ kuwa matawi ya CCM, watu waliishi uhamishoni kwa kutofautiana nae mitazamo.

Hatuwepo wakati huo lakini rekodi zipo
 
Nchi ilitopea kwenye umasikini wa kutisha, alinusulika kupinduliwa mara mbili, yeye ndie muasisi wa kuzigeuza TISS na JWTZ kuwa matawi ya CCM, watu waliishi uhamishoni kwa kutofautiana nae mitazamo.

Hatuwepo wakati huo lakini rekodi zipo
CCM ilikuwa na chuo pale kivukoni tangu ilipoanzishwa mwaka 1977, ni sera ya chama sio Nyerere kama Nyerere.
 

And I tell exactly the same...that has never been a reliable way of passing on education or any important information from generations to generations. It is very backward. Africa has lost tremendous amount of knowledge because of using that same way to propel forward education.
Unachosema sio cha maana na haina maana mkisimuliana kwenye kahawa mnaambiana ukweli. Most of the time mnadanganyana sana.
Ndio maana wenzetu wote walioweka knowledge kwenye maandishi wanatupita mbali sana. Tusiendelee kudharau elimu na hasa kuandika. Hata wewe anza kuandika hata kwenye diary ili wajukuuu zako waje kusoma one of the days. Sio wasubiri kulishwa matango pori kwa porojo zisizoeleweka
 
Lugha inakuwa na maana kama unauchumi mkubwa,sasa wewe unajua kiswahili unaenda kuomba kazi kwa mtu anayejua kiingereza au kichina,kiswahili kitakusaidia nini?
Angalia wakenya walivyotupiga gape kimataifa kila sehemu wapo,sababu ya lugha ya kiingereza siyo kiswahili
 
Kubolonga kwa wasomi waliofuata hakuondoi mabaya ya Nyerere, teacher na hao waliomfuata wote wamepuyanga ndio maana tupo hapa.
 
Nchi ilitopea kwenye umasikini wa kutisha, alinusulika kupinduliwa mara mbili, yeye ndie muasisi wa kuzigeuza TISS na JWTZ kuwa matawi ya CCM, watu waliishi uhamishoni kwa kutofautiana nae mitazamo.

Hatuwepo wakati huo lakini rekodi zipo
Kumbe kama ulikuwa umeshazaliwa kipindi kile basi itakuwa ulikuwa bado mdogo ! πŸ™πŸ™
 
Uko sahihi kabisa. Binafsi nawaheshimu mno wazee kwa sababu hiyo. Kuna mzee fulani mitaa ya Ilala alikuwepo siku ya sherehe za uhuru huwa ananisimulia mno mikasa iliyotokea. Tatizo wazee wengi huwa kuna mambo wanaishia kuguna na kuelezea juu juu.
Wazee wanaogopa kusema mengi wanayoyajua na waliyoyapitia kwa sababu wameshawaona wenzao wakidhalilishwa na wenye kushika Hatamu za Uongozi Eti kwa sababu tu ya kuusema Ukweli !!

Acha waendelee kuukumbatia Uongo na kuwahujumu wanaosema Ukweli !
Lakini wajue Ukweli una tabia ya kujitokeza hadharani hata kama utafichwa kwa muda mrefu !
Iko siku utajitokeza bila kupingwa πŸ™πŸ™
 
Umeongea ukweli
 
Hivyo viwanda mbona vilishindwa kuzalisha bidhaa za mahitaji muhimu ya kila siku,hadi watu kutumia sukari guru,kuvaa magunia,sabuni tu za kufulia/ogea hazikuwepo?.. viwanda vilianza kumfia mwenyewe!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…