Nauliza, Mwalimu Nyerere nchi ilimshinda kuongoza?

Minaki ya wamisionari babu, nyerere hakujenga sekondari yoyote,hakukuwa na jkt kila mkoa,get your facts right bro,pawe na kambi ya jkt kila mkoa?..forodhani ni shule iliuotaifishwa
 
Mbona alikuwa analindwa sana,unazani alichokuwa anaogopa nini?
"Alikuwa analindwa sana" kwa vipi, na kufananisha na nani

Hili nalo ni jambo la kuleta hapa kujadili?

Tuonyeshe huko kulindwa sana kulikuwaje hadi udhani kulikuwa na sababu za kipekee sana.
 
Mwinyi akiwa Rais alimwambia Mwalimu wewe Mwalimu ni mlima mimi Mwinyi ni Kichuguu tu
Kichuguu hakiwezi kushindana na Mlima 🙏🙏
Mwinyi alijuwa hadhi kubwa ya uongozi aliokuwa nao Mwalimu Nyerere. Na siyo yeye pekee aliye tambua hivyo.

Hawa wanao kuja hapa na kuibua vi-mada vya hovyo hovyo ni wajukuu wa wale walionyang'anywa maslahi yao kwa manufaa ya waTanzania; au kwa sababu zao za kiimani kama wazee wa Kariakoo.
 
Minaki ya wamisionari babu, nyerere hakujenga sekondari yoyote,hakukuwa na jkt kila mkoa,get your facts right bro,pawe na kambi ya jkt kila mkoa?..forodhani ni shule iliuotaifishwa
Zipo nyingi tu mkuu huko mikoani, kutaifisha maana yake zinatumiwa na watoto wa kizalendo. Ni mali ya walipa kodi baada ya kuwa zimetaifishwa,

Wewe labda mgeni, JKT Makutupora, JKT Mafinga JKT Buhimba, kule Kigoma, pia kulikuwa na JKT. Kila mkoa ulikuwa na JKT angalau moja.

Punguzeni chuki, kumchukia Marehemu ni kujitafutia laana zisizo na msingi.
 
Unaijua hadithi ya mwinyi ya kuoga bafuni na mwendawazimu kupitia nguo zako?..ulisikia alichokisema kwenye hotuba yake inayofichwa ya mikuki mitatu?..hapo alikua 'anamkoga' tu
 
watu wengi wanamuona Nyerere kama nabii ,kwamba alipaswa kuanzisha na kumaliza yeye kila kitu .
wanasahau kuwa Nyerere ni mwanadamu japo na kwa zama zake alifanya makubwa sana

Kipindi tunapata uhuru, vitu vya msingi vilikuwa ni
1.Disunity
2.Ujinga
3.Ukabila
4.Decentralized Settlements
5.Udini
yote haya yakifanikiwa ndo huduma za kijamii zingefanikia kutolewa kwa watu wengi ndani ya muda mfupi

Nyerere alipokea nchi ikiwa bado ipo jehanam , asingeweza maliza kil kitu yeye binafsi

Alianzisha nia ila waliofuata wakabadili njia na ndo matokeo ya haya tunayaona sasa
1.Ufisadi
2.Utekaji
3.Mikopo ya hovyo
4.Mikataba ya hovyo
 
Jkt ruvuma,rukwa,kagera,singida,kaskazini unguja,kusini,chakechake, kutaifisha siyo kujenga, acheni ujinga, hakuna anayemchukia bali ukweli uwekwe wazi
 
Acha uwongo wewe,disunity gani ilikuwepo nchini?..kariakoo kulikua na wanyamwezi kibao na makabila mengine wakiishi pamoja,tanga, morogoro makabila tofauti yslikuwepo,wahehe na watu wa tanga na tabora walikua na mafungamano tangu 1800 huko,wangoni na wahehe pia, nyerere kaacha ualimu kapewa nyumba magomeni aishi na alihudumiwa familia yake,hakubaguliwa mtu kuwa dini yake wala kabila,yeye ndiye aliyekua na agenda za dini
 
Mimi na wewe nani ambae hana akili? Nimetaja mambo ambayo yalikuwepo katika uongozi wake lakini wewe reply yako imejaa dhihaka na vijembe mwanzo mwisho, nilitegemea wewe mwenye akili upinge nilichoandika kwa mifano anuai. Katika uongozi wa teacher nchi haikutumbukia kwenye umasiki?, watu hawakukimbia nchini kwenda kuishi uamishoni?
 
Mimi hoja yangu hakujenga shule ya sekondari,kutaifisha alitaifisha hadi nyumba za kuishi za wahindi kariakoo na temeke,ni unyang'anyi wa kawaida tu
Ajenga zenu za chuki za kidini hazina mantiki yoyote. Alikuwa na wakati mgumu kuendesha nchi tofauti na hawa kina Mwinyi na wengine waliofuatia.

Wahitimu hawakuzidi kumi na tano nchi nzima, kwa maana ya shahada za chuo kikuu, taratibu akaanza kupata wasaidizi wenye elimu zenye kuweza kujenga nchi.
 
Tatizo la njaa lilisababishwa na nini? Kama lilitokea kwa majirani zetu jr ni halali kutokea kwetu?. Uko Kenya sehemu kubwa ya ardhi yao haikubalinkilimo kama hapa kwetu, kwa wao kukumbana na tatizo la huaba wa chakula ni kawaida.

Reply zako unashambulia mtu binafsi badala ya kushambulia hoja.
 
Unajua nchi aliyoipokea mwinyi mpaka useme nyerere alichukua nchi ikiwa kwenye hali ngumu?..wazee walisema bora ya mkoloni,maana ilikua hovyo, ambulance kufuata wagonjwa ilishindikana wakati mkoloni alifanya
 
Unajua nchi aliyoipokea mwinyi mpaka useme nyerere alichukua nchi ikiwa kwenye hali ngumu?..wazee walisema bora ya mkoloni,maana ilikua hovyo, ambulance kufuata wagonjwa ilishindikana wakati mkoloni alifanya
Kukosoa ni kazi nyepesi sana. Nyerere alirithi nchi mbovu zaidi. Barabara ya kwanza ya lami ilijengwa mwaka 1956 na marehemu Kikenya, tumetoka mbali.

Haina tija yoyote kumsimanga marehemu asiyeweza kujitetea, alifanya kazi ngumu katika kuujenga msingi wa kitaifa.
 
Mkuu Mwalimu Nyerere anasimangwa na vijana wasiojua historia ya nchi hii na hata wae wasio na uwezo wa kuona mbali.
Mwalimu hstoria yake inajitetea yenyewe.
Mwalimu hakuwa mlafi
Mwalimu alikuwa na huruma
Mwalimu kwa fani yake ya ualimu alikuwa ana fundisha na kushawishi zaidi kuliko kitu kingine
Mwalimu hakuwa mbaguzi licha ya kutoka kabila dogo sana
Mwalimu hakujipendelea kimaslhi kujenga nyumba kwao wala barabra ya kwenda kwao.

Wengi humu hawajui kuwa Mwalimu hakuwa na barabara ya kwenda kujijini kwao kwa vile miaka yote ya Urais wake alikataa kujipendelea. Hata nyumba yake nzuri ya kwanza aijengewa na Jeshi kwa kulazimishwa.

Watu wengi walishindwa kwenda na filosofia ya Mwalimu kwa vile mioyo yao ilijaa mtamanio yao ya kujitajirisha kifisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…