bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
usitetee mipango mibovu. Hata Nyerere mwenyewe alikiri kukoseaNi sababu iliyo changia, siyo sababu pekee; na hakuna mtu aliye kuwa amepanga itokee hivyo. Watu kuhama ilikuwa ime pangwa hivyo bila kuwa na ufahamu wa kitakacho tokea na hali ya hewa.
Mwenye ufahamu kuhusu katiba mbovu ni wewe umechukua hatua zipi,soma kuhusu ostracism na human herding utanishukuruKatiba mbuvu nani alituachia?
Hebu Kwanza!usitetee mipango mibovu. Hata Nyerere mwenyewe alikiri kukosea
Shida ya Nyerere ni ujuaji mwingiSiyo nchi tu hata familia yake iangalie ilivyo
Haukumshinda, kuongoza ni changamoto na alikuwa na nia njema ndio maana alianzisha viwanda zaidi ya 100 nchi nzima.Nimezaliwa miaka 1970, nimekutana na maisha magumu Sana, kulikuwa hakuna Sabuni, Sukari, Mafuta na hata nguo.
Watu walivaa magunia, kulikuwa hakuna vyakula na wakati tunapata uhuru aliikuta Tanganyika iko vyema kutoka kwa mkoloni nchi ikiwa vizuri.
Je, Uongozi ulimshinda?
Aliongoza watu wachache kwani tulikuwa ni taifa lenye wajinga wengi. Chuo kikuu kimoja tu miaka ile ya 60 leo vipo kibao na taifa limezalisha mamilioni ya wasomi, uwezo wetu wa kuhoji umeongezeka sana.Shida ya Nyerere ni ujuaji mwingi
By the time wanakwisha na wewe utakuwa umego. Ni generations nyingine tatu au nne mambo yatakaa tofauti. mark my words.Watu wenye roho mbaya ndivyo walivyo uwa wanajijali wenyewe tu na wanapenda sifa na kuabudiwa na ndivyo hali ilivyo hivi sasa nchini mwetu,
Nyerere anaabudiwa kuliko Mwenyezi Mungu aliyetuumba,kila kitu utasikia Mwalimu alisema!
Angalia hata Muungano tulionao ulistahili kabisa muundo wake kupitiwa upya lakini ni kama vile kila kiongozi anaogopa kuchokonoa jambo hilo kwani anaona atauudhi mzimu wa Nyerere sasa labda tusubiri hadi vile vizee vyote vinavyomuabudu huyo bwana mkubwa vife vyote.
Japo sijakuelewa ulichokusudia lakini naheshimu maoni yako.By the time wanakwisha na wewe utakuwa umego. Ni generations nyingine tatu au nne mambo yatakaa tofauti. mark my words.
Halafu Nyerere hakutufundisha kuiba na kula rushwa. Na hili nalo uliongeze kwenye matatizo yanayokusibu.
Japo sijakuelewa ulichokusudia lakini naheshimu maoni yako.
Tafadhali kijana - wewe unaona kuhamia vijiji vya ujamaa ilikuwa mipango mizuri? Kutaifisha mashamba ilikuwa mipango mizuri? Wewe unaujua umri wangu hata ukasema nimekariri? Na wala hakuna sehemu nimesema Nyerere amekosea katika mambo yote. Mimi degree yangu ya kwanza nilipata mwaka 1980, kwa hivyo hiyo enzi ya Nyerere uliyoisoma kwenye vitabu mimi nimeipitia katika maisha yangu.Hebu Kwanza!
Ni wapi "nimetetea mipango mibovu"?
Kuhamia vijijini ilikuwa "mipango mibovu"? Nani kasema kuwa ilikuwa "mipango mibovu"?
Kwa vile tu umekariri ulicho soma bila kutumia akili, ndiyo uje hapa kunieleza nikubaliane na wewe kuwa ilikuwa mipango mibovu?
Halafu kuonyesha jinsi gani usivyo tumia akili yako sawasawa, nionyeshe mahali ambapo "Hata Nyerere mwenyewe alikiri 'kukosea'" - kwa kuanzisha vijiji, au kukosea katika mambo yote? Ni binaadam yupi asiyekosea maishani mwake?
Ulitegemea Nyerere awe malaika? Kila mara watu wa aina yako mnakimbilia hiyo hoja ya Nyerere "kutokosea", jambo ambalo mna lizua wenyewe kwa kukosa hoja za kupinga aliyo yasimamia kama kiongozi.
Kambona alimwambia ujamaa haufai,tukaishia kumtusi kwenye nyimbo za mchakamchaka shuleni,hashauriki yule,aliitwa haambiliki enzi zakeHayati Mwalimu ni Siasa za Ujamaa na Kujitegemea ndio zilimshinda na alishindwa kukiri kuwa zimemshinda na KAMA KAWAIDA YA WATANZANIA WANAKUSHAURI MAMBO UNAYOPENDA KUYASIKIA HUKU WANAKUOGOPA KINAFIKI.
Kizazi 1980s hakimtukuzi huyo mzeeNi hivi kusema wafe watu ndio legacy yake ipotee sio kitu cha siku mbili tatu. Pengine generation kadhaa nyingine. Wewe na mimi tutalikosa hilo boti.
The roots are so deep. It requires same level of thinking to uproot them
Umeandika nini?Kweli hata ccm haisababishi umasikini wa watanzania ila INAONGOZA vizuri sana na magaidi yanashugulikiwa
Kuna msemo unasema 'huwezi kutumia akili iliyosababisha tatizo kutatua tatizo'..haishangazi kuona kwamba hakuona tatizo kwenye ujamaa wake,ujamaa kwake ulikua dini,alichukia sana mtu kuwa tajiriYule mzee alikua anakiri kukwama dhahiri kabisa.Ni kwamba tulishindwa kumuelewa na kuchukua hatua muhimu.
-alitoa kitabu cha kuhusu Ujamaa na kusema kila akikisoma(maandishi na si uhalisia)hakuona kilipokosewa hadi akaja kusikia azimio la Zanzibar.
-alikiri kukosea mambo mengi na mengine yalikua mema tu.Akaendelea kuasa kwamba shida ni sisi hatujui kuacha mabaya na kuchukua mazuri yaendelezwe kwa mazuri mengine ili kuleta ustawi.
-aliikataa CCM hadharani na kwa hisia alisema kwa sababu inaenenda hovyo,angeiacha.Si mama wala baba yake hiyo CCM.
-alienda mbali akatuletea uhalisia(siyo utunzi)wa nchi kimaandishi jinsi nchi ilivyokua imeharibika kimifumo/kuoza.Kitabu kikazua taharuki.
-jumlisha na hotuba mbalimbali za kuasa na kujuta.
Kazi ikabaki kwetu kusuka twende kilioni au butus!
Moja ya vitu alivyofanikiwa Nyerere ni kutufanya Watanzania kuwa mandondocha wa kufikiri yeye ni kiumbe wa kipekee ambaye alikuwa sahihi kwa kila jambo alilofanya! Kuna watu wanamuona yeye ni zaidi ya Mungu!Ni hivi kusema wafe watu ndio legacy yake ipotee sio kitu cha siku mbili tatu. Pengine generation kadhaa nyingine. Wewe na mimi tutalikosa hilo boti.
The roots are so deep. It requires same level of thinking to uproot them
Sasa kwann alilazimisha tupate uhuru wakt bado tulikuwa hatuna uwezo kujiongozaBinafsi namkubali mwamba Kuibadili nchi kutoka umasikini wa 0 ni kazi ngumu sana , Laiti angekata tamaa Tusingekua hapa..
Watu hawakua na elimu ya kutosha, Serikali haina akiba yeyote, Watu walikua na Mindset ya kusaidiwa na serikali...
Alipata tabu sana mwalimu