ndolelejiUduhe
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,837
- 3,027
Kweli Elimu ilikuwa bado ni ndogo na yeye Mwalimu alilijua hilo,Walitaifisha kutokana na presha ya waliokuwa chini yao katika suala la kiuongozi.
Baada ya uhuru waingereza walimwambia Nyerere waijenge Kariakoo na sehemu kubwa ya jiji la Dar ili liwe ni jiji lenye kutazamika kimataifa, wazee wa kiswahili waliokuwa na nyumba zao Kariakoo walimbishia Nyerere pamoja na hao wazungu.
Waliwataka waingereza waondoke haraka bila hata ya kutimiza hiyo azma waliyomwambia Mwalimu Nyerere. Miaka mingi baadae watoto wa hao wazee wamekuja kuuza nyumba zile zile ambazo baba zao walishauriwa zijengwe upya kwa ajili ya kuwa na jiji la Dar lenye muonekano mzuri.
Hatuwezi kujua ni akili zipi haswa alizokuwa nazo Nyerere miaka hiyo ya awamu ya kwanza. Tukumbuke kielimu tulikuwa bado tupo nyuma sana. Mwalimu alikuwa na wigo mdogo wa washauri miaka ile ya uhuru.
Ndio maana alikataa hata Madini ya dhahabu na mengineyo yasichimbwe kwa sababu waliokuwa wanahitaji kuchimba walitaka wapewe kwa masharti yao wawekezaji,
Mwalimu akawaambia acheni kwanza wenye Nchi wasome wajue thamani ya hayo Madini ili watakapokubali yachimbwe hawatakubali wapunjwe !
Bahati mbaya walipokuja hao wasomi waliokuwa wanasubiriwa Tukapigwa na kitu kizito kichwani !