Can you elaborate huo uwiano mbaya wa faida unaopatikana sasa,na utuoneshe tunaostahiki kupata
Wewe ni mtu tegemezi sana. Bila shaka huko shuleni ulikuwa msumbufu sana kwa walimu wako. Kila mara unahitaji 'spoon feeding'?
Haya, ngoja nikupe muda kidogo:
Bandari nchi inatafuta mikopo kuiboresha miundo mbinu zake ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Huo mkopo ni wananchi ndio watakao ulipa (usiniambie wananchi hawahusiki, maana nimegundua akili yako inavyo fanya kazi).
Baada ya kuiboresha bandari kwa ukarabati huo, badala ya kufanya juhudi kuweka usimamizi mzuri wa uendeshaji wake, unakwenda nje kutafuta kampuni ije kufaidika na hali hiyo nzuri iliyopo hapo bandarini.
Hapa umeshindwa kama kiongozi kuhakikisha kwamba Tanzania pia inahitaji kujijengea uwezo wa kuendesha shughuli za bandari zake. Kiongozi anaona bora "agawe" (wewe unaita uwekezaji)! Dola za Marekani ?250 milioni katika miaka mitano? (Uwekezaji)?.
Bandari hiyo huyo aliye gawiwa anakaa nayo miaka 30, na pengine zaidi; na wewe kiongozi usiye kuwa na akili kichwani unaona hilo ni jambo zuri sana. Haiingii akilini mwako kwamba hata kama WaTanzania wote wangekuwa na akili finyu, ndani ya miaka 30 wasiweze kuwa wamefuzu katika uendeshaji wa shughuli za Bandari.
B\Na siyo hivyo tu. Bandari hiyo hiyo, kabla ya kuwatafuta hawa "wajomba" na wao waje kufaidi, palikuwepo na "wawekezaji"? wengine, walio kaa hapo zaidi ya miaka 25; na katika muda wote huo, wananchi wa nchi yako bado waliendelea kuwa vihiyo, wasioweza kitu katika maswala ya uendeshaji wa bandari?
Tafadhali sana, mkuu 'Gallo'; nimetumia muda wote huu kueleza kwa haraka sana ninavyo kusikitikia wewe na viongozi wako. Nchi hii haitakuwa tofauti na Haiti katika miaka 100 ijayo kama mwendo wenyewe ndio huu huu wa viongozi hawa na wananchi wa aina ya 'Gallo'.