Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Pole sana mkuu kama kweli hukumkosea chochote kibaya basi ipo siku atakutafuta kwa spidi ya ngiri mkia juu baada ya kutendwa aendako.
 
Pole sana, huenda ulionyesha interest ya kutaka Ndoa zaidi kuliko yeye! MUNGU atakupa wa Kwako at the right time. Kama unahisi upweke, unataka kutoka, please DM! Huhitaji kujidhuru, wewe ni wa thamani Zaidi ya Ndoa!

Kama utajisikia kutoka, kusafiri, kubadilisha mazingira, I am ready, at zero cost! Nitaheshimu
 
Tatizo liko kwako. Kwanini umtumie sms ya kuachana. Na kwanini unaeleza ru kuhusu ukimya wake na namna alivyopotea huelezi ulichomkosea? Tatizo wanawake mmekuwa mkiringa sana. Unaipata iliyo haki yako, face it.
 
Mkuu mbona husemi yote, siku ile nimeshika simu nilikuta nini pale? Au unadhan niliyo yaona katika simu yanapaswa kuchukuliwa kawaida kama unavyotaka. Siwezi kuwa na mioango mingi na mikubwa na ww kisha ufanye yale unayotaka kuendelea kufanya ilihal unajua hayatakiwi katika mahusiano.

Na jibu kali kuliko yote huwa ni kukaa kimia
 
Ni ngumu sana hiyo, isikie kwa jirani, hiyo hali alitakiwa aitengeneze wakati yuko naye
 
Nimeipenda hii
 
Nimeipenda hii
 
Angalia kitu kinachoweza kukusogeza kwenye malengo yako kwasasa, Usishikilie ya nyuma.

Focus kwenye Kujiimarisha zaidi hayo yote ni destructions tu.

Lakini kumbuka hilo limetumika kama somo pia.
 
Namnukuu Kiranga πŸ‘‡πŸ»

Ukiachwa hilo ni kosa lako.

Ama umemkubali mtu ambaye si sahihi tangu mwanzo. Kosa lako.

Ama mtu alikuwa sahihi mwanzo akabadilika, ukashindwa kumuacha wewe kwanza. Kosa lako.

Ama mtu sahihi, ila kakuchoka tu. Kosa lako.

Vyovyote vile hutakiwi kuachwa.

Ukiachwa usilalamike. Tafuta mwingine tu.

Kwa sababu, kuachwa ni kosa lako.

Bila kujali wewe ni mwanamke au mwanamme. Bila kujali unahudumia au unahudumiwa.

Unatakiwa kuwa na mvuto mkali sana kiasi kwamba wewe tatizo lako liwe ukiingia kwenye mahusiano watu hawataki kuachana nawe.

Yani wao ndio wawe wanalazimisha mahusiano na wewe, sio wewe unalazimisha mahusiano na wao.

Ukiachwa ujue ushazembea sehemu hapo.

Jitafute ujiongeze mwenyewe bila kutaka kumdhuru mtu.
 
Dah,

Hiki somo gumu kumeza kwa watu wengi naona.

Shukurani kwa kutukumbusha.
 
Pole nadhani kuna uwezekano mkubwa uliamua kumpa tunda mapema kabla ya ndoa ukiamini hiyo ndio njia ya kumkamata,kumbe hapo ndio ilikuwa chanzo cha kukutoa umaana wako na leo hii hana hata cha kujutia,kwani hana alichobakiza kwako ambacho ni kipya....
 
Mengi wamesema wadau hapo,yangu ni haya kwakuwa ulituma meseji kwamba muachane basi tuma meseji hii kisha kaa kimya,hapa unaondoa kosa ulilolifanya

baby ukimya wako unaniumiza sana mpaka nikajikuta nakutumia meseji ya kuachana,lkn sikumaanisha ni hasira tu kutokupata mawasiliano yoyote kutoka kwako
Ukimya wako unanitesa sana,love you always


kisha kaa kimya kpnz,kama alikuwa anakujaribu atakucheki tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…