Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Hello wakuu,

Nimeona nishare sababu niko katika hali mbaya. Mawazo mabaya ya kujidhuru yananijia kichwani. Sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye. Kila kitu kilikuwa vizuri, ghafla akakata mawasiliano. Wiki 3 sasa nikimpigia hapokei, sms hajibu.

Nimehangaika, nikaongea na dada na kaka yake lakini bado alinikalia kimya. Mara ya mwisho kuwasiliana naye tulizungumza vizuri tu. Mipango yetu ilikuwa tufunge ndoa na alipanga mwezi huu aje nyumbani kujitambulisha. Lakini ghafla kimya chake kikatokea.

Baada ya kimya kirefu, siku 5 zilizopita nikamtumia sms ya kuachana lakini hakunijibu kitu. Naumia sana. Sijawahi kumkosea chochote ila ameamua kunifanyia ukatili huu. Naumia na najiuliza maswali ambayo sipati majibu.
Kuna jambo huliweki wazi, si rahisi kwa hatua mlofikia mtu kukata mawasiliano ghafla bila sababu yoyote.
 
Wiki tatu mbona ndogo mimi sikuongea na mpenzi wangu mwezi mzima nillkua na stress zangu siyo kwamba nilikua nimuacha ila sikua ba furaha ya kuongea nae nilitaka utulivu
Mwezi mzima na bado unampenda unamkalia mtu kimya mwezi mzima
 
Hii ni lugha katili kwa mwanadamu mwenzako anayepitia mazito kama haya.....

Mitandao ya kijamii isitufanye tuwe makatili wa kihisia dhidi ya binadamu wenzetu kwa kuwa tu tuna uhuru wa kuandika chochote......
Wewe acha unafiki hapa,

Ulikua unatuma picha za watu waliouawa Gaza,picha ambazo hazikua nzuri kiubinadamu,

Nikakuripoti kwa moderator,ila ukawa unazidi tu kutuma hizo picha kwa makusudi,

So,acha unafiki wako hapa na kujifanya eti una busara.
 
Hello wakuu,

Nimeona nishare sababu niko katika hali mbaya. Mawazo mabaya ya kujidhuru yananijia kichwani. Sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye. Kila kitu kilikuwa vizuri, ghafla akakata mawasiliano. Wiki 3 sasa nikimpigia hapokei, sms hajibu.

Nimehangaika, nikaongea na dada na kaka yake lakini bado alinikalia kimya. Mara ya mwisho kuwasiliana naye tulizungumza vizuri tu. Mipango yetu ilikuwa tufunge ndoa na alipanga mwezi huu aje nyumbani kujitambulisha. Lakini ghafla kimya chake kikatokea.

Baada ya kimya kirefu, siku 5 zilizopita nikamtumia sms ya kuachana lakini hakunijibu kitu. Naumia sana. Sijawahi kumkosea chochote ila ameamua kunifanyia ukatili huu. Naumia na najiuliza maswali ambayo sipati majibu.
Amesema amekukuta sio bikira,yupo chimbo anashughulikia mission ya kumpata mwanamke wa ndoto yake
 
Kaa utulie dada Tena kama waweza FUTA namba yake kabisaaaaa, ana moyo wake na fikra zake, enda na mtu anapoenda sawa akipinda shika hamsini zako, si rahisi lkn ndio ukweli, shika hamsini zako kama hujawahi mjua, maisha Yako yana thamani kuliko ya mwenzako aliyekutelekeza Tena kimya kimya.
 
Alipropose wewe ukaja na yako ya ili unioe fanya hivi na vile na vile, kaaangalia kaona hapa naingia kwenye dushu hili ngoja nilale mbele hapa naenda kupigwa, demand zenu kabla ya ndoa ziwe na akili sio mna-demand vitu sio vijana wanaingia mitini na wanaofanya hivyo ni wale wenye akili pekee mazombi wanakubali kila kitu
Mkuu nilikua mwema Na mtulivu Sana Kwa kijana Wangu Wala sikutaka mambo makubwa sababu uwezo wake naujua
 
Mara YA 3

Ohoo, move on dear, kama wako atarudi kama sio ndo kwaheri.
Ukija kupata mwingine hii kauli uifute kinywani mwako na kwenye maandishi yako na ujifunzage kujipa muda ikitokea sinto fahamu, ndugu zake ungepiga tu kujua kama ndugu yao yuko mzima au la, ulivyojua mzima basi nawe ungekausha tu ila sio kuanza kuwashtakia.
Anyway pole utakua sawa muda ni tiba tosha.
 
Mkuu nilikua mwema Na mtulivu Sana Kwa kijana Wangu Wala sikutaka mambo makubwa sababu uwezo wake naujua
Kijana wako? Dadadek ndio maana kala unyoya wewe kumuitaje kijana wako hivi unaelewa hilo neno maana yake wewe huyo jamaa ni km kijakazi wako mkata majani ya sungura?
 
Lazima kuna shida mahali, sio rahisi mtu kukupa mikausho mikali bila sababu na mnakaribia ndoa.
Labda kuna kitu kagundua juu yako, au yeye kapata mtu huko.

Kama kakausha mpe muda kama wiki/mwezi usimtafute, akikausha muda huo uliojiwekea basi anza process za kumove on.

Wewe ushamtafuta na bila shaka ushamtumia text nzito nzito kibao, mwisho wa siku wewe mwenyewe tena unamwambia muachane ilhali hujui sababu ni nini (hapa umekosea). Ungeendelea kumtafuta kikawaida na kumpa muda, muda uliompa ukiisha basi unamwambia muachane.

Sio hujatafutwa siku kadhaa tu unaanza kusema muachane.
Sasa nifanyaje tayari nishamwambia tuachane nlikua too emotional
 
Sasa nifanyaje tayari nishamwambia tuachane nlikua too emotional
Pole kama ni mwanaume mwenye akili atajua humaanishi, ila kama nae anatumia hisia kama wewe, mtasuluhisha kwa tabu hilo suala, usipende kumwambia muachane mtu ambae humudu kuachana nae.

Kama ushatumia means zote kumtafuta na bado hajibu, na wewe utulie sasa, kumtafuta zaidi na huku anaona kabisa unamtafuta ni kuzidi kumsumbua tu na wewe kujitesa zaidi.
 
Back
Top Bottom