Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Naumaliza mwaka Kwa machungu ya kuachana na mwanaume wangu niliyempenda sana

Aibu ya kuvunjika mahusiano ndio kitu gani?

Sikiliza binti, huyo bwana angekuwa amejitambulisha na kukulipia mahari hiyo ndiyo ingekuwa aibu, siyo hii unayoiongelea hapa.

Hayo yalikuwa mahusiano ya kawaida, kinachokuumiza ni malengo na upendo ambao unasema ulikuwa nao juu yake, usijiongezee vitu vya kukuumiza moyo.

Lakini, kosa lako lilikuwa kutuma ujumbe wa kuvunja mahusiano, ungekaa kimya ungeondoka na ushindi mkubwa maana pengine alipatwa na matatizo wewe kwa kukurupuka kwako umevuruga mambo.

Pengine anaweza kurudi, msikilize sababu zake na lazima hili lililotokea uliweke kama taa nyekundu, kama hana sababu za msingi inabidi uyape fikra ya upili hayo mahusiano yenu. Na asiporudi songa mbele, achana na mambo ya kujidhuru ni ukatili kwako na wapendwa wako.

Pole.
Ahsanteee week 3 mtu unapiga hapokei sms hajibu nikamuandikia io text ya Kuachana nithibitishe kama tumeachana
 
Huu ndio ukweli unamuwazaje mtu ambaye hakuthamini kama ni mimi nitaishia Tu kukukera basi lakini sio niache kuwaza mambo yangu nikuwaze wewe usieona thamani yangu hapana
Baaasi kwa kuwa umeyajua hayo, utakufa kwa mengine, ajali, malaria, na vinginevyo lakini sio stress za mapenzi.
 
Siwezi kushauri kitu hapa kwa sababu sijaona response ya upande wa kiumeni..

mwanamke kafanya makosa sana kutuma sms ya kuachana kwa sababu hajui hali aliyokua nayo mwanaume wake at that moment..

Miss_Mariaah ulipaswa kuwatafuta ndugu na jamaa wa mchumba wako ili ujue kama mumeo mtarajiwa ametekwa ama amelazwa hospitali ama kapotea tu, hapo ndio unge draw conclusion..

Otherwise niseme una akili kama za wqtoto wa 2000. Wanafanya maamuzi ya moto wa kifuu badae yanakuja kuwacost pakubwa..
 
Unataka kujidhuru kisa kuachwa ziko sawa kichwani kweli wewe alaaaaaah 🤔🤔 kabla hujajimaliza tupe location tuje kupiga mpunga hapo
 
Lazima kuna shida mahali, sio rahisi mtu kukupa mikausho mikali bila sababu na mnakaribia ndoa.
Labda kuna kitu kagundua juu yako, au yeye kapata mtu huko.

Kama kakausha mpe muda kama wiki/mwezi usimtafute, akikausha muda huo uliojiwekea basi anza process za kumove on.

Wewe ushamtafuta na bila shaka ushamtumia text nzito nzito kibao, mwisho wa siku wewe mwenyewe tena unamwambia muachane ilhali hujui sababu ni nini (hapa umekosea). Ungeendelea kumtafuta kikawaida na kumpa muda, muda uliompa ukiisha basi unamwambia muachane.

Sio hujatafutwa siku kadhaa tu unaanza kusema muachane.
 
Siwezi kushauri kitu hapa kwa sababu sijaona response ya upande wa kiumeni..

mwanamke kafanya makosa sana kutuma sms ya kuachana kwa sababu hajui hali aliyokua nayo mwanaume wake at that moment..

Miss_Mariaah ulipaswa kuwatafuta ndugu na jamaa wa mchumba wako ili ujue kama mumeo mtarajiwa ametekwa ama amelazwa hospitali ama kapotea tu, hapo ndio unge draw conclusion..

Otherwise niseme una akili kama za wqtoto wa 2000. Wanafanya maamuzi ya moto wa kifuu badae yanakuja kuwacost pakubwa..
Mkuu nilimtafuta dada yake Na Kaka yake nikaongea nao nikawaeleza situation wakaongea Nae lkn hakunitafuta
 
Hello wakuu,

Nimeona nishare sababu niko katika hali mbaya. Mawazo mabaya ya kujidhuru yananijia kichwani. Sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye. Kila kitu kilikuwa vizuri, ghafla akakata mawasiliano. Wiki 3 sasa nikimpigia hapokei, sms hajibu.

Nimehangaika, nikaongea na dada na kaka yake lakini bado alinikalia kimya. Mara ya mwisho kuwasiliana naye tulizungumza vizuri tu. Mipango yetu ilikuwa tufunge ndoa na alipanga mwezi huu aje nyumbani kujitambulisha. Lakini ghafla kimya chake kikatokea.

Baada ya kimya kirefu, siku 5 zilizopita nikamtumia sms ya kuachana lakini hakunijibu kitu. Naumia sana. Sijawahi kumkosea chochote ila ameamua kunifanyia ukatili huu. Naumia na najiuliza maswali ambayo sipati majibu.
Njoo nikupe faraja
 
Back
Top Bottom