Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Miss_MariaahHello wakuu,
Nimeona nishare sababu niko katika hali mbaya. Mawazo mabaya ya kujidhuru yananijia kichwani. Sijawahi kupenda kama nilivyompenda yeye. Kila kitu kilikuwa vizuri, ghafla akakata mawasiliano. Wiki 3 sasa nikimpigia hapokei, sms hajibu.
Nimehangaika, nikaongea na dada na kaka yake lakini bado alinikalia kimya. Mara ya mwisho kuwasiliana naye tulizungumza vizuri tu. Mipango yetu ilikuwa tufunge ndoa na alipanga mwezi huu aje nyumbani kujitambulisha. Lakini ghafla kimya chake kikatokea.
Baada ya kimya kirefu, siku 5 zilizopita nikamtumia sms ya kuachana lakini hakunijibu kitu. Naumia sana. Sijawahi kumkosea chochote ila ameamua kunifanyia ukatili huu. Naumia na najiuliza maswali ambayo sipati majibu.
Binti mrembo.
Ni jambo la kusikitika kuumiza moyo kwa mtu ambaye haoni thamani yako tena.
Haijalishi ni mzuri kiasi gani lakini kama amekuvunja moyo hupaswi kumpa nafasi ya kuomboleza na kumkumbuka.
Furabia maisha, ukweli ni kwamba hupendwi wewe kama wewe isipokuwa eidha your good looking, hekima/ busara zako, uli honacho...baaasi.
Jifunze kuishi wewe kama wewe.
Furaha yako ikimtegemea mwanadamu utalia kila siku.