Nitakuelewesha na utaelewa wala usiwe na wasiwasi ndugu yangu.
Wazazi wetu wote humu ndani wamezaliwa miaka tofauti tofauti yote ikiwa ndani ya karne ya 20. Kwa historia fupi tu, kipindi hicho elimu juu ya masuala ya kijamii na kiuchumi haikuwa kubwa kama ilivyo kwa sasa. Uzazi ilikua ni fahari. Elimu ya uzazi wa mpango haikuwa kubwa kama ilivyo sasa. Wengi walipata watoto bila uwiano wa idadi dhidi ya uwezo wao kiuchumi.
Wazazi wa karne ya 20, wengi wao walijua ukishamsomesha tu mtoto basi umemaliza. Na kisheria hili ni sahihi kabisa kwani baada ya umri wa miaka 18 mzazi hawajibiki tena na maendeleo yako. Kinachofuata baada ya hapo ni hisani.
Ila kwa sasa dunia imeshabadilika sana kwani mzazi anaetaka mwanae awe vizuri kiuchumi, inambidi kumuandalia misingi mizuri kando ya elimu. Japo hili pia sio jukumu.
Mtoto kumsaidia mzazi pia sio jukumu bali ni upendo na jadi yetu sisi waAfrika hivyo hakuna ubaya wowote kwa mtu kujilaumu kwa kushindwa kutimiza jambo hili la upendo kwa watu waliomlea na kumgharamikia.
Unachokiongea wewe ni sahihi ila sio sahihi kwa jamii yetu.
Nawasilisha.