Naumia sana ninaposhindwa kuwa msaada kwa wazazi wangu

Naumia sana ninaposhindwa kuwa msaada kwa wazazi wangu

Ila mkuu suala la kukata mawasiliano sio jambo jema maana hata kuwasalimia tu inaweza kuwa faraja kubwa sana kwao...wazazi Huwa wanahitaji kuwajali tu hata kwa namna ya kuwa karibu yao

Mkuu nakuelewa unachokisema ila huwezi kuelewa uzito wa kiatu usichokivaa. Mama yangu akiongea nasikia kuishiwa nguvu kabisa. Kiukweli anahitaji msaada na sio salamu.

Utakua unapiga simu kumjulia hali kila siku mtu anaehitaji msaada na wewe kila siku uko mikono mitupu?

Yaani assume mtoto kafukuzwa ada shuleni halafu baba kila siku anapiga simu kusalimia tu na sio kuleta suluhisho? Ni sawa?
 
Hongera sana elon mask watu kama nyinyi ndio mnaotakiwa humu sio kama Mzee

Hongera sana elon mask watu kama nyinyi ndio mnaotakiwa humu sio kama Mzee wa kupambania kutwa kutuelekeza machimbo ya mbususu na namna ya kuzichakata
Mbususu ndio zinatupa hasira ya kutafuta mkwanja kwa nguvu zote

Mbususu na hustling are direct proportional to each other
 
Ila mtiberi hili jambo mtambuka sana wazazi hawana makosa wao wamepata akili wamejikuta wapo Duniani na inabidi wafuate nature inavyotaka Mkuu uwe na pesa ausiwe na pesa au hali yoyote kiuchumi nature inakutaka uzae/uzalishe mtoto tu kwasababu umeumbwa na Genye, upweke ukikaa pekeyako nk

Mfano Mimi niliweka standard sana at least niwe na mke na mtoto nikiwa na kipato ila mpaka Sasa Sina na umri unaenda mpaka sasa nawaza nimseti manzi yeyote mkali nimuweke ndani hivyohivyo au kumpiga mimba tu mambo mengine yatajulikana mbele kwa mbele Mkuu sipendi hivi ila nimejipata akili nakujikuta Niko na vitu(resources) za kufanya hivyo na zimeumbwa kwa mtindo(alogarithim) ya lazima zitumiwe Kama hujatumia utapata adhabu i.e tumeumbwa na MASHINE haijari unauchumi wala malengo kihasi gani yenyewe inadinda tu uingize kule, Tumeumbiwa UMRI haujari ushatoboa au bado wenyewe unaenda tu unahitaji watoto wake kikuchota mav*** ukizeeka.

Mkuu haya mambo sio ya kulaumiana sisi binadamu muda mwengine tupo nje ya uwezonayo hakuna asiyepanga mipango ila moitishaji Mungu

Sijasema wazazi wanamakosa au Hawana.
Nilichosema ni kuwa mtoto Hana wajibu wala jukumu la kusaidia wazazi wake, tena Kwa mazingira ya Vijana wengi ambao wao(Vijana) wenyewe hawajiwezi, hawajimudu kimaisha.

Yaani kijana Aache kuwaza future yake na watoto wake awaze wazazi?
Mzazi ni mungu
wa pili, huwezi kuwaza kumsaidia mungu Bali kumshukuru.

Sisi kama wazazi wa kileo, Hii kwetu tuichukue kama changamoto. Maana uzee wetu NAO sio MBALI.
 
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wanahangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwe wa mwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.
usikate tamaa !kwa hicho kidogo ulichonacho wasaidie iko iko na mungu atafungua njia.mlilie mungu usiku wa manane afungue njia zako ,zile ibada za satisa na sanane muombe kwa dini yako mungu atafanya njia .
 
Shida zangu kivipi?
Hiyo Hana shida, Ila hiyo shida anajiendekeza, kujipendekeza na kujipa stress Kwa vitu ambavyo sio halali kwake.
Sasa MTU uzae mtoto alafu baadaye mtoto aumie kisa anashindwa kukusaidia, ilihali mzazi ndiye alitakiwa amsaidie mtoto mpaka awe na uwezo wa kujimudu kimaisha.

Mtu akishaweza kujimudu kimaisha automatically atakuwa na uwezo wa kutunza wazazi wake
Reasoning yako katika utoaji wa hoja huwa upo Vizuri saana mkuuu.
#Nakukubali
 
Kwenye jamii yetu ni jadi mzazi kuacha urithi mbali na Elimu.

Ninachojaribu kumueleza mtoa mada na vijana wengi wanaokabiliwa na changamoto hiyo(Mimi nikiwepo) kuwa wasijisikie vibaya, wala kukulaumu, wala kujipa stress zisizo na kichwa wala miguu. Kuhusu kusaidia wazazi ilhali Hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Huwezi umia Kwa kitu ambacho sio wajibu au jukumu lako. Huko ni kutokujitambua

Kama unaelewa kuwa kuacha urithi mbali na elimu ni jadi yetu, ugumu uko wapi wewe kuelewa pia kwamba ni jadi yetu kuwasaidia wazazi wetu? Na sio tu wazazi, mtu yeyote aliewahi kukusaidia kwa lolote, unatakiwa ulipe fadhila. Sio jukumu ila ni busara, wema, upendo na utu. Vyote hivyo ni miongoni mwa tofauti zinazotutofautisha sisi na wanyama.

Kukosa uwezo wa kufanya kitu hakubadilishi uhalisia wa kwamba unatakiwa ukifanye. Katika kutambua kuwa unapaswa kufanya jambo fulani ndipo utakapopata chachu ya kutafuta namna ili ufanikishe na sio kubweteka na kujificha kwenye kivuli cha "SIO JUKUMU LANGU".

Asiejitambua ni mtu anaetumia nguvu zote kukwepa kusaidia waliomsaidia. Face your fears, running is never a solution in the long run. Na hio ni sehemu ya kuwa mwanaume.
 
Endelea kupambana ipo siku utawasaidia ,nifuraha sana kama unapata kipato chakuweza kuwasaidia wazazi hata kwa kidogo tu inaleta amani ya moyo sana.
 
Ninachoshukuru Mungu kwaajili yako ni kwamba hujataja kizuizi chochote cha ww kuweza kujitaftia riski yako kama matatizo ya kiafya

Lakini naomba nikuaminishe kwamba kile unachopitia ni kama mtu anapoumwa na njaa kwasababu muda aliozoea kula haujafika na haimpi shida ile njaa kwasababu anajua ni muda tu ndyo kikwazo cha njaa.

Naomba nikuaminishe kuwa hakuna kitu kizuri kama kile ulichokipata kwa taabu.kwahyo kupambana,kuomba sana Mungu ndyo kila kitu.
 
Kaka/dada


Najua unavyojiskia kwa kushindwa kua msaada kwa wazazi wako ila amini kwamba haitakua hivyo siku zote. Endelea kumuomba Mungu akupe njia ya kupata mishe yoyote halali itakayokuletea chochote kitu au kama unayo ila haina maslahi sana basi akupe yenye maslahi.

Maisha ni hatua ndugu yangu. Usikate tamaa wala usijiskie vibaya. Endelea kutafuta mchongo wala usione aibu. Nimewahi kupitia hali kama yako. Mwenye nyumba wetu alikua ananipa maneno makali sana pale nilipokua nachelewesha kodi. Lakini mama yangu sasa hivi yuko kwenye nyumba yake niliyomjengea mwenyewe.

Mungu atakusaidia. Hesabu baraka zako za sasa kwamba haujafa na wala hauko hospitali ukiumwa maradhi mazito mazito

Mambo yatakaa sawa [emoji1545]
Good Relief
 
Hongera sana elon mask watu kama nyinyi ndio mnaotakiwa humu sio kama Mzee

Hongera sana elon mask watu kama nyinyi ndio mnaotakiwa humu sio kama Mzee wa kupambania kutwa kutuelekeza machimbo ya mbususu na namna ya kuzichakata
Samahani mkuu, Ina bidi tujifunze kufurahia uwepo was watu wote.
👉Hulka ya mwanadamu ni kufurahia Yale yote yalio mazuri machoni mwake, ana sahau lililo zuri kwako laweza kuwa baya kwangu.
👉Mimi ni jobless wa kimataifa, hata huyo Mzee wa kupambania, ana jua Sana.
👉Nina mpango wa kuomba anagalau ki barua kwa Mzee wa kupambania, ili nipate angalau ka ugali🙏🙏💪
 
Samahani mkuu, Ina bidi tujifunze kufurahia uwepo was watu wote.
👉Hulka ya mwanadamu ni kufurahia Yale yote yalio mazuri machoni mwake, ana sahau lililo zuri kwako laweza kuwa baya kwangu.
👉Mimi ni jobless wa kimataifa, hata huyo Mzee wa kupambania, ana jua Sana.
👉Nina mpango wa kuomba anagalau ki barua kwa Mzee wa kupambania, ili nipate angalau ka ugali🙏🙏💪
Daaah! 😅
 
Back
Top Bottom