Naumia sana ninaposhindwa kuwa msaada kwa wazazi wangu

Naumia sana ninaposhindwa kuwa msaada kwa wazazi wangu

Unapokuwa nacho unawasaidia tu -alhamdullillah

Unapokosa unawaambia najua wataelewa - alhamdullillah min kul hali

Uzuri wa wazazi ni waelewa sanaa tofauti na mtu tu aliyekuwepo mbali na wewe na asiyekufahamu vizur ila ugumu unakujaga kwenye matatizo ya lazima hapo vichwa vinawakaga moto aisee

Ila ni kutokata tamaa nao na kujituma kwenye harakati zetu za kila siku kuna mda utafika na kujipongeza wewe mwenyewe wakati ambao pesa na mambo mazuri yatakuwa upande wako na shida kuwa mbali na wewe na kuzimudu shida zao zote wanazohitaji uwasaidie

Tusiwaache wazee wetu kwani wao hawakutuacha tulipokuwa wadogo
 
Mungu atusaidie wote ambao bado tuna wazazi na wameshazeeka tupate uchumi na moyo wa kuwasaidia ..its very important..na hivohivo kuendelea kupambana kuwawekea mazingira mazuri ya badae watoto wetu ili waje waweze kutusaidia ikiwa watakuwa na moyo huo.

A M E N
 
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wanahangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwe wa mwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.
Hello

Kwanza nikutie moyo kwa yote unayopitia na nikukumbushe tu

1. Kufanikiwa ama kufeli ni neno mtambuka kati ya mtu na mtu (kufeli kwako kwa mwingine ndio mafanikio and vice verse is true) na kwa kuanzia kabisa, kabla hujaangalia magumu unayopitia, hebu jaribu kuangalia yale mazuri na mafanikio kidogo uliyonayo tofauti na wale uliowazidi - kumbuka, utajiri na fanikio kubwa kabisa la kwanza ni afya yako, kama wewe hujambo na ni mzima wa afya then jipige kifuani tafuta ugali ule upumzike

2. Kufanikiwa kwa asilimia kubwa sana pamoja na mambo mengine huchangiwa na familia uliyotokea, jamaa na marafiki ulionao then comes wewe as an individual. Jaribu kujiuliza, katika jamii yako wewe ndio umefeli kuliko wote? I guess no! If so then endelea kuota mpaka ndoto zako zitakapokuwa kweli na kukimbiza ndoto zako muda wako waja.

3. Kufanikiwa katika maisha pia ni suala la bahati, haijalishi wewe ni nani ama upoje bahati ina nafasi yake hivyo endelea kumuomba Mungu wako akukumbuke huku ukiendelea kupambana, usichague kazi, tafuta ujuzi, bana matumizi na fanya kazi yoyote halali ya kukuingizia kipato.

4. Mafanikio mengi unayoona watu wanayo yamechukua ndoto za muda mrefu na muda mwingi sana, ni nyumba chache sana zinajengwa kwa mwaka mmoja, ni nyumba nyingi sana zimeisha kwa ndani, watu wengi kununua gari 1 sio chini ya miaka 5, kufanya kitu kikubwa kinachooneka kwa wengi si chini ya miaka 3 hivyo basi endelea kupambana na kuweka malengo ya muda mrefu mpaka pale jambo lako 1 litakapotimia.

Mwisho, achana na kusaidia wazazi, furaha kubwa zaidi ya wazazi wote ni kuona kwanza watoto wao wanafanikiwa na si kuona vile watoto wao wanawasaidia by so saying, keep your head moving, pray na endelea kupambana.
 
Pole kwa mugumu your unayopitiq mkuu,hakika haupo pekee yako kwenye Hali hiyo.

Kikubwa Ni kutokata tamaa na kuzidi kupambana Hadi pale utakapokuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwasaidia wazazi wako.
Waambie wazazi wako wawe na subira na Wala wasichoke kukuombea kea Mungu.Lazima ipo siku mambo yatakaa sawa na wazazi wako watajivunia kuwa na wewe.

Kila la heri zako mkuu Mungu akufanyie wepesi Katika safari yako ya utafutaji 🙏
 
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wanahangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwe wa mwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.
Mkuu embu njoo nbox tuongee kdg
 
Back
Top Bottom