Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Dah mkuu umetumia maneno makali sana.
Huu msafala tupo wengi mnooYaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.
Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wanahangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.
Bora niwe wa mwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.
Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.
Kurusha lawama juu ya shida zako kwa upande mwingine ni miongoni mwa sifa kuu ambayo masikini wote have in common.
Kabisa mkuuSijajua ndugu mleta uzi uwezo wako kifedha ukoje
Siku moja nunua mahitaji yaliyo ndani ya uwezo wako halafu mpelekee bimkubwa
Ile asante ya wazazi wako ya kutoka moyoni itakuongezea nguvu ya kupambana na utapata furaha fulani
Mzazi kama alishindwa kufanikiwa Asitegemee mtoto aje kupambana kwa niaba yake.Tupo wengi sana huku mtaani, tunaumia sana tunapowaona wazazi wetu umri wao unaenda huku sisi tukiwa bado tuko kwenye msoto, huwa naumia ingawa sametimes wazazi wanatusave angalau kidogo Mungu atupe nguvu kwakweli
Noooooo,mzazi !!Your parents owe you nothing.
Wazazi wako hawakudai kitu.
Sio lazima na sio sheria ya kwamba mtoto lazima amsaidie Mzazi.
Pambania Maisha yako.
Kama mzazi yeye alipambana na akashindwa kuwa na maisha bora asitegemee mtoto apambane kwa niaba yake kisha aje kumsaidia.
Msaada si lazima ni hiyari.
Mzazi kupambana kuwalea watoto ni wajibu wao na ni lazima.Noooooo,mzazi !!
Hapana,tupambane tuwasaidie.
Kumbukua walivyopamba ili ufanikiwe,wakakulea,kukusomesha hata km ni Hadi la Saba tuuu,wanahitaji Sana support yetu
Sametimes nature inatulazimu kuwapambania wazazi, hata kama walishindwa kufanikiwa lakini ni mzazi acha tuwasaidie tu hata kwa hichi kidogo tunachojaaliwa ili tupate baraka za MunguMzazi kama alishindwa kufanikiwa Asitegemee mtoto aje kupambana kwa niaba yake.
Ila mkuu suala la kukata mawasiliano sio jambo jema maana hata kuwasalimia tu inaweza kuwa faraja kubwa sana kwao...wazazi Huwa wanahitaji kuwajali tu hata kwa namna ya kuwa karibu yaoPole sana fam. Napitia the exact same situation kwa sasa. Wazazi wametumia gharama kubwa kunilea na kunisomesha mpaka nimehitimu chuo, imefika muda nguvu yao kiuchumi na kimwili imepungua wanahitaji msaada ila wakuwasaidia ndo kwanza mambo bado kabisa.
Mama yangu anaumwa sana ila bado anahangaika sokoni kuuza bidhaa ndogo ndogo ili familia ipate kula. Kila nikiongea nae nasikia sauti yake ni ya mtu aliechoka, mwenye maumivu na mwenye kuhitaji msaada ila kijana wake ndo helpless kwa sasa. Imefika kipindi sitaki kwenda nyumbani kusalimia na nimekata mawasiliano kwakua najisikia vibaya na unyonge mkubwa hata kuongea nao.
Ila dunia haina huruma na mtu mkuu. We ought to turn this pain to fuel and rise. Tuendelee ku'force mkuu na tukipata hata kidogo unakumbuka nyumbani sio kusubiri mpaka uwe tajiri. That's the way forward.
Shida zangu kivipi?
Hiyo Hana shida, Ila hiyo shida anajiendekeza, kujipendekeza na kujipa stress Kwa vitu ambavyo sio halali kwake.
Sasa MTU uzae mtoto alafu baadaye mtoto aumie kisa anashindwa kukusaidia, ilihali mzazi ndiye alitakiwa amsaidie mtoto mpaka awe na uwezo wa kujimudu kimaisha.
Mtu akishaweza kujimudu kimaisha automatically atakuwa na uwezo wa kutunza wazazi wake
Nitakuelewesha na utaelewa wala usiwe na wasiwasi ndugu yangu.
Wazazi wetu wote humu ndani wamezaliwa miaka tofauti tofauti yote ikiwa ndani ya karne ya 20. Kwa historia fupi tu, kipindi hicho elimu juu ya masuala ya kijamii na kiuchumi haikuwa kubwa kama ilivyo kwa sasa. Uzazi ilikua ni fahari. Elimu ya uzazi wa mpango haikuwa kubwa kama ilivyo sasa. Wengi walipata watoto bila uwiano wa idadi dhidi ya uwezo wao kiuchumi.
Wazazi wa karne ya 20, wengi wao walijua ukishamsomesha tu mtoto basi umemaliza. Na kisheria hili ni sahihi kabisa kwani baada ya umri wa miaka 18 mzazi hawajibiki tena na maendeleo yako. Kinachofuata baada ya hapo ni hisani.
Ila kwa sasa dunia imeshabadilika sana kwani mzazi anaetaka mwanae awe vizuri kiuchumi, inambidi kumuandalia misingi mizuri kando ya elimu. Japo hili pia sio jukumu.
Mtoto kumsaidia mzazi pia sio jukumu bali ni upendo na jadi yetu sisi waAfrika hivyo hakuna ubaya wowote kwa mtu kujilaumu kwa kushindwa kutimiza jambo hili la upendo kwa watu waliomlea na kumgharamikia.
Unachokiongea wewe ni sahihi ila sio sahihi kwa jamii yetu.
Nawasilisha.
Ila mtiberi hili jambo mtambuka sana wazazi hawana makosa wao wamepata akili wamejikuta wapo Duniani na inabidi wafuate nature inavyotaka Mkuu uwe na pesa ausiwe na pesa au hali yoyote kiuchumi nature inakutaka uzae/uzalishe mtoto tu kwasababu umeumbwa na Genye, upweke ukikaa pekeyako nkInakera MTU akupe majukumu ambayo Kwanza huna uwezo nayo, pili yeye anasehemu kubwa ya kukusaidia alafu atake umsaidie. Huo ni ujinga.
Wazazi wa sasa(Sisi) tujifunze; kuzaa hata Watoto wetu watazaa. Kumtegemea mtoto kisa ulimzaa Wakati hukumjengea mazingira ya kukusaidia ni zaidi ya unyama. Hata wanyama hawafanyi hivyo.
Ukweli usemwe
Hongera sana elon mask watu kama nyinyi ndio mnaotakiwa humu sio kama Mzee
Hongera sana elon mask watu kama nyinyi ndio mnaotakiwa humu sio kama Mzee wa kupambania kutwa kutuelekeza machimbo ya mbususu na namna ya kuzichakata