Naumia sana ninaposhindwa kuwa msaada kwa wazazi wangu

Naumia sana ninaposhindwa kuwa msaada kwa wazazi wangu

turubbo

New Member
Joined
Aug 1, 2023
Posts
3
Reaction score
179
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wanahangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwe wa mwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.
 
Kaka/dada

Najua unavyojiskia kwa kushindwa kua msaada kwa wazazi wako ila amini kwamba haitakua hivyo siku zote. Endelea kumuomba Mungu akupe njia ya kupata mishe yoyote halali itakayokuletea chochote kitu au kama unayo ila haina maslahi sana basi akupe yenye maslahi.

Maisha ni hatua ndugu yangu. Usikate tamaa wala usijiskie vibaya. Endelea kutafuta mchongo wala usione aibu. Nimewahi kupitia hali kama yako. Mwenye nyumba wetu alikua ananipa maneno makali sana pale nilipokua nachelewesha kodi. Lakini mama yangu sasa hivi yuko kwenye nyumba yake niliyomjengea mwenyewe.

Mungu atakusaidia. Hesabu baraka zako za sasa kwamba haujafa na wala hauko hospitali ukiumwa maradhi mazito mazito

Mambo yatakaa sawa [emoji1545]
 
Ni kawaida, pia usikate tamaa ipo siku utawasaidia tu.

Kitu hujua ni kuwa wazazi hatutegemei sana kwa watoto, tunajipambania, ikiwa anatokea mtoto Mungu akamuinua akasaidia wazazi pia tunashukuru.

Lengo la mzazi ni kuona watoto wamesimama kwa miguu yao wenyewe.

Wapigie wazazi simu wasalimie, hilo pia ni muhimu.
 
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wana hangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwewamwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.
Polee sanaa mkuu....nahisi maumivu yako.

1. Badili mtazamo wako anza leo jione mwenye bahati,jione unaweza na jione unamsaada kwa wengine.

2.Jaribu jaribu na ujaribu tena usikate tamaa....kukata tamaa ni dhambi na umaskini ni nusu ya ukafiri kaa ukijua hilo.

3.mwamini muumba wako...fanya uzalishaji wa kizazi,Allah kashaandika rizki ya kila mja...rizki yako ni yako na watoto watakuwa na rizki yao pia,kikubwa hakikisha unafanya hasibabi (sababu) sio unalala ndani ukategemea pesa ikufate au ukaenda kwa mwamposa ukategemea ata kupa nguvu za kutafuta..
 
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wana hangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwewamwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.

Wao ndio wanatakiwa Waumie Kwa Kushindwa kukusaidia kama mtoto wao ili ujikimu na kujimudu kimaisha.
Kama walikuzaa kama Mnyama bila mipango tatizo sio lako
 
Mwenyezi Mungu atakusaidia... Amini kuwa haupo peke Yako unaepitia hali hiyo... Mimi nilipo gundua kuwa Kuna mambo hata nifanyaje siwezi kuyafanikisha...Huwa naiachia nature iniamulie...nimeamua kuichagua furaha kuliko karaha. Furaha unayo wewe mwenyewe usijiwazie mabaya...jiwazie mambo mazuri...amini kuwa IPO siku mzazi wako atakuomba elfu 10 na wewe Kwa shangwe utamtumia milioni...😊​
 
Pole Sana mkuu, maisha ni mapito.
👉Unaeza uka jihisi wewe una shida zaidi, ila kiukweli kila mmoja ana majnga mazito.
👉 Kikubwa Usikate tamaa, amini unayo nguvu ya kukufanya kunyanyuka Tena
👉Jaribu kuji changanya kwa mtaa, Kuna nafasi Unaeza pata.
👉Iki kubidi Hama mtaa,wilaya, au mkoa unao ishi, ili ujaribu Fursa pengine.🙏🙏
 
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wana hangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwewamwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.

Pole sana fam. Napitia the exact same situation kwa sasa. Wazazi wametumia gharama kubwa kunilea na kunisomesha mpaka nimehitimu chuo, imefika muda nguvu yao kiuchumi na kimwili imepungua wanahitaji msaada ila wakuwasaidia ndo kwanza mambo bado kabisa.

Mama yangu anaumwa sana ila bado anahangaika sokoni kuuza bidhaa ndogo ndogo ili familia ipate kula. Kila nikiongea nae nasikia sauti yake ni ya mtu aliechoka, mwenye maumivu na mwenye kuhitaji msaada ila kijana wake ndo helpless kwa sasa. Imefika kipindi sitaki kwenda nyumbani kusalimia na nimekata mawasiliano kwakua najisikia vibaya na unyonge mkubwa hata kuongea nao.

Ila dunia haina huruma na mtu mkuu. We ought to turn this pain to fuel and rise. Tuendelee ku'force mkuu na tukipata hata kidogo unakumbuka nyumbani sio kusubiri mpaka uwe tajiri. That's the way forward.
 
Hata wazazi wanaumia wanapoona kijana wao anapambana ila hafanikiwi

Ukiwasaidia kwa kidogo ulicho nacho watakushukuru sana. Wanaelewa hali unayopitia

Pambana mkuu ipo siku utawasaidia kwa kingi zaidi

Kuna kipindi hata wazazi huwa wanajilaumu kuwa hawakuwawekea msingi mzuri watoto wao
 
Nikwambie kitu... tupo wengi kinoma.. Usiuwazie umri sana utakata tamaa.. kama bado una hema amini katika baadae yoyote inaweza kuyabadilisha maisha.. Kikubwa Tujiyunze Sana. wazazi hawaumii kisa haturudishi marejesho, tunawaumiza yunapokosa Amani na Furaha.
 
Wao ndio wanatakiwa Waumie Kwa Kushindwa kukusaidia kama mtoto wao ili ujikimu na kujimudu kimaisha.
Kama walikuzaa kama Mnyama bila mipango tatizo sio lako

Kurusha lawama juu ya shida zako kwa upande mwingine ni miongoni mwa sifa kuu ambayo masikini wote have in common.
 
Yaani jinsi maisha yalivyo magumu kwangu nawaza maishani mwangu nisije kupata mtoto akaja duniani kuja kula msoto kama Mimi.

Maana Mimi mwenyewe niña wazazi lakini siwezi kuwasaidia msaada wowote wanahangaika nauzee wao mtoto wao sieleweki.

Bora niwe wa mwisho kuteseka ila damu yangu nisiilete duniani kula huu msoto.

Najilaumu na utu uzima huu sina msaada wowote kwa wazazi Bora wasinge nizaa naona Hadi aibu kurudi home au kupiga simu.
Rudi shambani
 
Mazee, Mungu akufanyie wepesi ufanikiwe.
Nafurahi kuona hata unawawaza wazazi, hii inaonyesha wewe ni mtu muungwana mno.
Usikate tamaa mambo yatakaaa sawa tu, muhimu ni kuwa na nidhamu na kuendelea kupambana.
 
Back
Top Bottom