Naunga mkono suala la kubinasifisha Bandari ya Dar es Salaam

Sasa hapa Tatizo ni bandari au ni Serekali?

Kwanini unapendekeza bandari ibinafsishwe bada ya Serekali inayoshindwa kusima bandari ndio ibinafsishwe.
Watu wake, kwami wale Ma director wana share pale?
 
Saa100 kichwa anakitumia kufungia ushungi amna mtu pale
 
Nyie mmeweza nini? Taka kimoja wapo mlicho weza kufanya biashara
 
Upi? Hakuna commitment pale make muda wowote mkurugenzi anapigwa chini
 
Tatizo 10% na ujinga wa viongozi kiwango cha SGR, na hata tunachopata sasa hatutapata, zitaundwa kampuni za mikobani kama Richmond then tutaambiwa ni DP Dubai, dawa ni kutafuta CEO mwenye uzoefu na uendeshaji wa bandari kubwa, apewe malengo, budget na bila kuingiliwa na wanasiasa na ikiwezekana aripoti moja kwa moja kwa Raisi (bandarini kuna pesa nyingi sana pale), hakuna haja ya kugawana na mtu yeyote wakati tunaweza kukusanya zote na zaidi, bandari sio kampuni za simu ,too much money there
 
Ccm mnauza bandari yetu miaka 100? Mkataba gani wa miaka 100? Kwa malengo Yapi? Miaka 100 mabadiliko yatakua makubwa sana hapa Duniani, Kwanini tunahukumu vizazi vyetu vitatu au vinne kwa tamaa za sasa?

Baada ya hapo atakuja mwingine ajifanye Mzalendo wakati alishiriki uchafu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Aisee ndio maana nilimsikia Mbunge mmoja akiwasifia sana baada ya kwenda ziara huko Dubai. Kumbe ndio zao hawa Mabwana. Haya kila la kheri waungwana.
 
👀Muda Wa Kubembelezwa Umefika Sasa
Your browser is not able to display this video.
 
Kama Alhaji Mwinyi Alivyifanya Loliondo Kuitoa Miaka 100 Kwa Mwarabu
Yanakwenda Kukamilishwa Tena Na Mama Anawapa Tena Waarabu Bandari Miaka 100
 
Huu ni ukoloni wa kidigitali/ Digital era colonialism ndio hizi hadithi wanakuja na mifumo yao ya kisasa. Huu ni ukoloni ule ule kwa mbinu za kisasa. Mifumo gani ambayo mswahili wa leo hawezi kuweka? Kuna wakati tuliaminishwa miamala ni Maximalipo tu mbona kuliwekwa mifumo mengine ya kiserikali na mambo yanaenda. Kinachotakiwa ni utashi na mitazamo ya waliopewa jukumu la kuongoza wenzao.

Binafsisheni na majeshi nayo kama mmeaamua kujitoa ufahamu kiasi hiki.
 
Kama Alhaji Mwinyi Alivyifanya Loliondo Kuitoa Miaka 100 Kwa Mwarabu
Yanakwenda Kukamilishwa Tena Na Mama Anawapa Tena Waarabu Bandari Miaka 100



Kumbe Mwinyi naye ndivyo alivyo?!

Mmnh?!
 
Wewe ukiunga mkono haimaanishi jambo hilo ni halali.
 
Kubali tu hata ubishe vipi huo ndiyo ukweli. Kwani TTCL imekodishwa? Angalia performance yake ilivyo
 
Sipendi ubinafsishaji wa Bandari ya Dar sababu itaondoa uwezo wa Clearing Agents ku clear mizigo kwa kodi ya chini kwa faida ya mteja haswa magari yaliyoyochakaa ambayo ni over taxed. Kwa mfumo uliopo, Clearing Agents wana nafasi kubwa ku clear mizigo kwa kodi ya chini kuliko ile ambayo TRA wangedai. Hii ni win-lose situation. Hakuna mtu mwenye akili nzuri anayetaka kulipa kodi ya TRA ambayo inaenda kununua Land Cruiser LC300 na kujenga mahekalu ya MaCCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…