Naunga mkono wazo la Mbunge kuweka Picha ya Rais Samia kwenye Sarafu ya Tanzania ili kutunza kumbukumbu na alama muhimu ya Maendeleo ya Nchi yetu.
BoT fanyeni haraka wazo hili.
===
Your browser is not able to display this video.
Mhe. Waziri Mkuu mwaka 2006 Bunge hili lilipitisha sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya kuipa mamlaka benki hii kudizaini fedha kwa kuweka nembo na material mbalimbali, mwaka 2021 nchi hii imepata Rais wake wa kwanza mwanamke anayefanya kazi nzuri na anatambulika katika Bara la Afrika na duniani kama Rais madhubuti na wa mfano, je, serikali haioni sasa kwamba kuna haja ya kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa Rais Samia Suluhi Hassan kwa kuweka picha yake katika fedha za nchi hii?" - Mbunge Ng'wasi Kamani.
Waweke picha yake kwenye pesa kwa maajabu gani aliyotufanyia??!!.
Hastahili, hata yeye ndani ya nafsi yake anajua hivyo ukiacha nyie chawa mnaofaidika na uzembe wake!.
Tukija kuona matunda ya Sera zake baada ya miaka 50 tutakumbuka kufanya hivyo, ila kwasasa ni mapema sana...watu wenye maono ni wale wanaoweka long term plan alafu zinatoa matokea chanya siyo wale wanalenga urefu wa pua yao.
Nashauri tu, mawazo ya mbunge yaheshimiwe ila asiseme mambo kwa pupa akiongozwa na ushabiki.
Samia ana historia gani kwenye hili taifa zaidi ya kuwa Mwanamke wa kwanza kupata urahisi kwa ngekewa baada ya mikakati mizito ya kumuondoa Mwana Chato!
Wanaostahili kuwekwa kwenye pesa ni Mkapa au Magufuli,hutaki hamia Haiti!