Naunga mkono wazo la Mbunge kuweka Picha ya Rais Samia kwenye Sarafu ya Tanzania

Naunga mkono wazo la Mbunge kuweka Picha ya Rais Samia kwenye Sarafu ya Tanzania

Hahahahaha mbunge wa Bunge la nchi ya Tanzania katika ubora wake
 
View attachment 2897672
"Mhe Waziri Mkuu mwaka 2006 Bunge hili lilipitisha sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya kuipa mamlaka benki hii kudizaini fedha kwa kuweka nembo na material mbalimbali, mwaka 2021 nchi hii imepata Rais wake wa kwanza mwanamke anayefanya kazi nzuri na anatambulika katika Bara la Afrika na duniani kama Rais madhubuti na wa mfano, Je serikali haioni sasa kuna haja ya kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa Rais
@SuluhuSamia kwa kuweka picha yake katika fedha za nchi hii?," - Ng'wasi Kamani

Machawa wa Maza hao .... hii tabia aliyotuachia JPM inalitafuna sana Taifa.
 
Mnajipendeza mpaka mnakera. Watu hatuna umeme, unaongelea picha ya Rais kuwekwa kwenye noti!
 
We ngwasi kaman,nimegundua Kwa nn ukiwa central buhongwa ss buhongwa mkolani Mwanza, form 3, ulgombana na kaka ako damas kaman sababu alikula wali wako na maharage.
 
Siipingi hiyo Hoja ya Mbunge mimi sio Mbaguzi wa Jinsia au Ubaguzi wa aina yoyote lakini huwezi kumfananisha Samia Suluhu na Harriet Tubman.

Ni mapema mnooo!! For God's sake mbona mnapenda ku rush?

Mgao wa Umeme, Wizi Serikalini, High Cost of Living Wananchi hawapati HAKI Mahakamani Uhuru wa Vyombo vya Habari unaingiliwa na RC wa Mkoa na Mwenezi wa Chama nk. nk.

Nchi iko kwenye Crisis.
 
chadema mnakasirika nini mlitaka iwekwe ya mbowe

👆 Bunge liongelee mambo haya ya Msingi.
 
itakua imekaa poa.hasa ukizingatia Dunia ya sasa ni ya gender issue ni muhimu sarafu yetu iwe na Rais wa kwanza mwanamke.
 
Bila shaka hii itapunguza shida ya umeme na bei ya sukari pamoja na kupandisha thamani ya fedha yetu.

Tuwafundishe watu wetu kudeal na mambo magumu Magumu na kuachana na hizi issue ndogo ndogo za kijinga.
 
Vituko kama hivi vinaletwa na watu wachache umu jf..mwananchi gani aliyewahi kumchagua uyo raisi
 
Kama watafanya hivyo basi itakuwa ni ujinga wa kiwango cha juu Sana. Wazo hili linawezakupigiwa debe na wajinga, matapeli,wapumbavu, vilaza na takataka zingine. Lakini mzalendo wa kweli na mwenye utimamu sawasawa hawezi kukubali kutia nuksi sarafu ya nchi.
Nuksi ipi?
 
Watanzania kwa unafiki na kujikomba hamjambo

Nchi ina shida nyingi za kujadiliwa mnajadili huu ujinga😏😏😏😏
Kuwa na shida nyingi ndio kunazuia nini kujadili picha ya Rais kwenye Sarafu?
 
Awekwe kama kielelezo cha taifa lisilokua na ubaguzi wa kijinsia, kwamba ni mama wa kwanza kuwa raisi wa taifa letu
 
Ukiweka hiyo picha kwenye pesa tatizo la umeme, maji, sukari na mengine yata isha?
Sijui wabunge wengine wana toka wapi?
 
Naunga mkono wazo la Mbunge kuweka Picha ya Rais Samia kwenye Sarafu ya Tanzania ili kutunza kumbukumbu na alama muhimu ya Maendeleo ya Nchi yetu ,naunga mkono wazo la kuweka picha ya Rais Samia kwenye Sarafu ya Fedha zetu.

BoT fanyeni haraka wazo hili.

===


Mhe. Waziri Mkuu mwaka 2006 Bunge hili lilipitisha sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya kuipa mamlaka benki hii kudizaini fedha kwa kuweka nembo na material mbalimbali, mwaka 2021 nchi hii imepata Rais wake wa kwanza mwanamke anayefanya kazi nzuri na anatambulika katika Bara la Afrika na duniani kama Rais madhubuti na wa mfano, je, serikali haioni sasa kwamba kuna haja ya kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa Rais Samia Suluhi Hassan kwa kuweka picha yake katika fedha za nchi hii?" - Mbunge Ng'wasi Kamani.
Without prejudice naliunga mkono jambo hili kwa sababu ndiye rais wa kwanza mwanamke.

Mapungufu yake ya kisiasa yasimnyime haki yake kwenye historia ya nchi yetu
 
Kwahiyo hiyo picha itaongeza thamani ya shilingi kwa dola? Itapunguza bei ya sukari? Itaondoa mgao wa umeme? Yaani hili bunge kama hawa ndo wabunge basi lifutwe tu serikali iamue kila kitu. Ila hii tabia ya kujipendekeza itaua hii nchi
Itatunza historia muhimu ya Taifa na inamheshimisha Rais katika harakati z kuyatatua hayo unayoyaeleza.
 
Back
Top Bottom