Hoja ya kuwajibika kama mwanaume au kiongozi ina msingi, lakini imechukuliwa kwa upande mmoja sana.
Mamlaka ya kweli haijengwi kwenye kuogopesha au kufukuza watu kirahisi, bali kwenye uwezo wa kusimamia, kusikiliza, na kufanya maamuzi yenye busara.
Msingi wa Kwanza wa mamlaka yoyote ni uwezo wake wa kuunda na kubomoa. Hilo weka kichwani
Boss wako ili aitwe Boss anauwezo WA kukupa adhabu na kukufukuza pale unapokuwa unakosea.
Busara ni muhimu Sana lakini sio zalazima kwenye mamlaka.
Sheria ni muhimu kuliko busara
Familia si taasisi ya amri na adhabu pekee, ni mahusiano ya watu wawili wenye utu na hisia.
Familia ni taasisi.
Taasisi inaongozwa na Sheria na taratibu.
Hizo adhabu zinakuwepo kama Sheria na taratibu hazifuatwi.
Msingi mkuu wa Familia ni Sheria. Hatuzungumzii mapenzi ya teenage.
Upendo ni sehemu ya Sheria.
Utu unaozungumziwa upo kwenye Sheria humo.
Kiongozi anayefikiri suluhisho la kila changamoto ni ‘kufukuza’ au ‘kuanza upya’ anaweza kuonekana mkali, lakini mara nyingi hiyo huwa ni ishara ya kushindwa kusimamia changamoto kwa ukomavu.
Changamoto za kutokutii ni kufukuzwa Hilo wala halinaga mijadala.
Sasa kama hautii unataka nani akuendekeze? Ndio maana ya Mamlaka.
Usipotii usitegemee Mamlaka itakuchekea.
Mamlaka inaweza kukuchekea kwenye mambo mengine kama makosa ya kibinadamu na uzembe wa hapa na pale.
Lakini haitovumiliwa ukikaidi na kutokutii.
Iko hivi watu wanasamehe makosa lakini sio uhalifu.
Uongozi wa kweli haupimwi kwa ukubwa wa sauti au ukali wa maamuzi, bali kwa uwezo wa kujenga uthabiti, maelewano, na heshima ya pande zote.
Ndiyo maana hata kwenye mifumo mingine ya uongozi duniani, viongozi bora hawatawali kwa woga bali kwa ushawishi na hekima.
Mataifa yote makubwa na waliojenga tawala kubwa duniani wote hawakutumia hiyo mifumo yako.
Na nikuambie tuu familia yenye wababa wademokrasia nyingi zinamatatizo. Wanawake wanawasumbua na watoto wanawashinda alafu wanakuja kulaumu wanawake hawaeleweki.
Hakuna mwanamke anayependa kuongozwa na mwanaume goigoi, mwanademokrasia, asiye na mfumo dune. Huyo mwanamke hayupo.
Ndio maana wanawake hupendelea Bad boy. Na sifa mojawapo ya bad boy ni mfumo dume.