Naungana na DC Magoti: Wanaume wanaolaumu Wake zao na kulalamikia wanawake sio Wanaume waliokamilika

Mfumo dume kwa sasa ni mfumo chakavu ,ambao kwa sasa wanaouendekeza ndio walalamishi wa kubwa

Mtu anayetumia mfumo Dume au jamii zinazotumia mfumo Dume duniani kote hazina hicho kitu unachokisema.

Mfumo dume hautumii mfumo wa ulalamishi isipokuwa kuchukua hatua.

Ukiona mwanaume yeyote ambaye mapenzi yalimshinda au alionewa na wanawake ujue alitumia mfumo jike, fair play au anatumia mfumo wa kiliberari
 

Alafu huo msemo Dikteta wengi wanaoutumia ni wanawake au wanaume ambao wameshindwa kuongoza familia zao.

Mfumo dume ndio mfumo sahihi Kabisa
 
hivi unaelewa maana neno ''kutii'' au unalitumia tu, binadamu mtu mzima anawezaje kumtii binadamu mwingine? only a slave ndiyo anatii au jeshini wanajeshi labda wanatii amri ya mkuu wa kikosi lkn siyo biandamu huru ...
.mwanamke yeye kumtii Mumewe sio hiyari ni lazima.
Kwa sababu Mume ni Mtawala, kiongozi WA familia.

Mtawala ni lazima umtii upende usipende. Wala sio Ombi.

Mamlaka zote kuanzia ngazi ya chini lazima uiitii. Sio hiyari
 
Hiyo labda uokote binti asiye na namna
 
Hoja ya kuwajibika kama mwanaume au kiongozi ina msingi, lakini imechukuliwa kwa upande mmoja sana.

Mamlaka ya kweli haijengwi kwenye kuogopesha au kufukuza watu kirahisi, bali kwenye uwezo wa kusimamia, kusikiliza, na kufanya maamuzi yenye busara.
Msingi wa Kwanza wa mamlaka yoyote ni uwezo wake wa kuunda na kubomoa. Hilo weka kichwani

Boss wako ili aitwe Boss anauwezo WA kukupa adhabu na kukufukuza pale unapokuwa unakosea.

Busara ni muhimu Sana lakini sio zalazima kwenye mamlaka.
Sheria ni muhimu kuliko busara

Familia si taasisi ya amri na adhabu pekee, ni mahusiano ya watu wawili wenye utu na hisia.
Familia ni taasisi.
Taasisi inaongozwa na Sheria na taratibu.
Hizo adhabu zinakuwepo kama Sheria na taratibu hazifuatwi.
Msingi mkuu wa Familia ni Sheria. Hatuzungumzii mapenzi ya teenage.
Upendo ni sehemu ya Sheria.
Utu unaozungumziwa upo kwenye Sheria humo.

Kiongozi anayefikiri suluhisho la kila changamoto ni ‘kufukuza’ au ‘kuanza upya’ anaweza kuonekana mkali, lakini mara nyingi hiyo huwa ni ishara ya kushindwa kusimamia changamoto kwa ukomavu.
Changamoto za kutokutii ni kufukuzwa Hilo wala halinaga mijadala.

Sasa kama hautii unataka nani akuendekeze? Ndio maana ya Mamlaka.
Usipotii usitegemee Mamlaka itakuchekea.
Mamlaka inaweza kukuchekea kwenye mambo mengine kama makosa ya kibinadamu na uzembe wa hapa na pale.

Lakini haitovumiliwa ukikaidi na kutokutii.

Iko hivi watu wanasamehe makosa lakini sio uhalifu.


Mataifa yote makubwa na waliojenga tawala kubwa duniani wote hawakutumia hiyo mifumo yako.

Na nikuambie tuu familia yenye wababa wademokrasia nyingi zinamatatizo. Wanawake wanawasumbua na watoto wanawashinda alafu wanakuja kulaumu wanawake hawaeleweki.

Hakuna mwanamke anayependa kuongozwa na mwanaume goigoi, mwanademokrasia, asiye na mfumo dune. Huyo mwanamke hayupo.

Ndio maana wanawake hupendelea Bad boy. Na sifa mojawapo ya bad boy ni mfumo dume.
 
.mwanamke yeye kumtii Mumewe sio hiyari ni lazima.
Kwa sababu Mume ni Mtawala, kiongozi WA familia.

Mtawala ni lazima umtii upende usipende. Wala sio Ombi.

Mamlaka zote kuanzia ngazi ya chini lazima uiitii. Sio hiyari

yeah kwa muslims na wa mila mila hiyo ni kawaida, lkn siyo Christian marriage, Christian marriage inafundisha watu kuheshimiana na siyo kutawalana, kuna sababu kwa nini democracy is Christian ...
 
yeah kwa muslims na wa mila mila hiyo ni kawaida, lkn siyo Christian marriage, Christian marriage inafundisha watu kuheshimiana na siyo kutawalana, kuna sababu kwa nini democracy is Christian ...
Ndoa ni taasisi lazima mmoja amtawale mwingine. Hilo huwezi kuliondoa Abadan
 
Wanawake wake wa wapi hao ? Ukiona mwanamke anakubali mfumo dume jua ni goigoi tu na hana namna

Ndio maana hamuwaelewi wanawake.

Njia rahisi unaweza kuwauliza wanawake wenyewe angalau kumi. Waulize wangekuwa wanaume wangekuwaje?
Then utajua wewe uelewa wako kuwahusu ni wanawake ndio goigoi.

Kingine uanaume wengi kwa sasa wengi wa kizazi cha Leo hamjui ni nini.

Kama uliwahi kwenda jeshini basi Kule angalau kidogo utafundishwa maana ya mwanaume ili uwe mwanaume.
 
Mfumo dume ni wa wanaume dhaifu na waoga wanaogopa changamoto, ndio maana baada ya wanawake kupata elimu na kushika pesa mfumo dume unadondoka na walio na dhana hiyo wamebaki kulalamika tu
 
Ndoa ni taasisi lazima mmoja amtawale mwingine. Hilo huwezi kuliondoa Abadan

ndio maana mnashindwa na nchi nzima imejaa vilio na umasikini kila mahali kwa sababu ya mentality kama hizo, nchi inanzia kwenye familia, kama familia baba ni abusive watoto hawawezi kuwa healthy kichwani, na ndiyo hawa wanaouwa watu kama wanyama leo hii, wanafisadi kila kitu bila ya kufikiria wengine kwamba pia wana haki ya kuishi ni kwa sababu no one taught them upendo, hawakulelewa kwa upendo bali ukatili na ubabe hivyo watoto wanakuwa wakiamini mwenye nguvu ana haki ya kuchukua na kupora kama vile baba yeke alivyokuwa utotoni, i mean kuna sababu kwa nini sisi masikini wa mwisho duniani na matatizo yetu ni unique, sababu ni hiyo hatulelewi kwa upendo bali ubabe na ukatili ...
 
Naunga mkono hoja yako
 
Mfumo dume ni wa wanaume dhaifu na waoga wanaogopa changamoto, ndio maana baada ya wanawake kupata elimu na kushuka pesa mfumo dume unadondoka na walio na dhana hiyo wamebaki kulalamika tu

Mfumo dume upo na haujawahi kudondoka.
Unachokiona kwa sasa ni madhara ya wanaume dhaifu ambayo hawajui wao ni wanaume ndio maana kuishi na wanawake kwao kunawasumbua wakati hakuna kitu rahisi kama hicho.

Wanaume wanaotumia mfumo dume hawana msamiati malalamiko.
Unaowasikia wanalalamika sio waumini wa mfumo dume.

Rejea kauli ya DC Magoti kwamba Mamlaka haiwezi kulalamika. Isipokuwa inachukua hatua.
.
Wanaolalamika ni wanaume dhaifu wasio na mamlaka. Wasiojitambua. Hawajui nini chakufanya.

Nafikiri bwashee unashindwa kutofautisha mfumo dume na ukatili na dhulma. Na hilo sio kosa lako pekee. Watu wengi wapo kama wewe.

Mfumo dume ndio utawala wenyewe. Mamlaka na nguvu.
 
Uyo Mpwechepweche ,anaweza kuwa anayasema kwa adhara kumbe ndani anakula vibao vya kutosha , hizi ni tabia za wa zee wa Pwani , ukikuta kwenye kijiwe cha kahawa alivyo na misimamo ,utasema yesi nenda kwake kauli moja tu ya mke wake ,anaufyata ,vibaya mno.
 
Wanalalamika mara nyingi ni wale waliokuzwa kwenye mifumo dume wakaja nayo kwenye mifumo ya sasa , ndio hao hao mwenye mpaka matukio ya kufanya mauaji ndani ya ndoa chunguza
 

Kuna mambo mengi huenda huyaelewi na yanakuchanganya kuhusu mamlaka(mfumo dume)

Kwanza lazima ujue ukishasema mamlaka hapo ujue kuna Ubabe upo iwe ni direct au indirectly.

Labda hoja kuu iwe ubabe kwenye nini lakini unapozungumzia Kampala unazungumzia ubabe, forces, nguvu.

Yaani kufanya mambo yenye tija hata kama kuna wanaopinga, wanaokinzana na wasiotaka.
Mamlaka haina statement za hiyari, ukitaka, ukipenda nope!
Hiyari unakuwa nayo ukiwa nje ya mipaka ya mamlaka husika.


Umaskini ni matokeo ya kutotumia rasilimali vizuri. Na haitokani na Mfumo dume wa mabavu.

Mataifa yote yaliyoendelea maendeleo Yao yalipatikana kwenye mfumo wa mabavu na sio demokrasia.
Nafikiri historia unaijua
 

Sisi ya ndani kwake tunamuachia. Tunabaki na Yale yanayotuhusu ya hadharani
 
Wanalalamika mara nyingi ni wale waliokuzwa kwenye mifumo dume wakaja nayo kwenye mifumo ya sasa , ndio hao hao mwenye mpaka matukio ya kufanya mauaji ndani ya ndoa chunguza

Mauaji hayana uhusiano na Mfumo Dume.
Wapo walamba lips wanaua pia.
 
Wanaume na makende yao wameitana kujadili wanawake na other petty issues? Smh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…