Naungana na DC Magoti: Wanaume wanaolaumu Wake zao na kulalamikia wanawake sio Wanaume waliokamilika

Mauaji hayana uhusiano na Mfumo Dume.
Wapo walamba lips wanaua pia.
Bwashee utembee na humu duniani sio ujifungie huko kihurio tu , kuna wanawake ukienda na hii mifumo yako utaonekana goigoi tu , shukuru pia umatumbini hakuna sheria , andiko kama hili kwa wenzetu likiamuliwa wewe na huyo sijui magoti mngekuta mnanyea ndoo sasa hivi
 
😅😅😅😅 Dah!
Kabisa ukiona mwanamke anakubaliana na hivyo jua kuna namna kabananishwa na maisha kwenye kona,ndio maana binti yangu kabla ya mimi kufa nimejipa kiapo lazima ajipate 🤔
 

Unachosema kuhusu sheria na uwajibikaji kina mantiki kwenye mifumo mingi ya uongozi, lakini kuna tofauti muhimu kati ya taasisi za kazi na familia.

Boss anaweza kufukuza mfanyakazi, lakini familia siyo contract ya kazi inayoweza kuvunjwa kirahisi bila athari za kina za kihisia na kisaikolojia.

Sheria zinaweza kuleta utaratibu, lakini haziwezi peke yake kujenga uaminifu na uhusiano wa kudumu. Ndiyo maana hata kwenye mifumo ya uongozi duniani, kuna tofauti kati ya power na legitimacy.

Unaweza kuwa na power ya kuadhibu, lakini kama huna legitimacy, watu wanatii mbele yako lakini wanapingana nawe kimya kimya.

Kuhusu hoja ya kuwa kutokutii sawa sawa na kufukuzwa bila mjadala, hilo linaweza kufanya kazi kwenye mifumo ya kijeshi au kazi fulani maalum, lakini ndani ya familia linaweza kuleta utii wa hofu, siyo uelewa.

Na ukilea kwa hofu, unapata nidhamu ya muda mfupi, lakini ukikosa uwepo wako, mfumo wote unalegea kwa sababu haukujengwa kwenye uelewa bali kwenye hofu.

Na mfano wa bad boy na mfumo dume, hiyo ni tafsiri rahisi ya mahusiano ya binadamu. Watu wengi huvutiwa na confidence na uthabiti, siyo lazima udikteta.

Confidence inaweza kuambatana na hekima na mawasiliano, si lazima iwe ukali au kukosa kusikiliza.

Kwa kifupi, mamlaka ya kweli siyo uwezo wa kuadhibu pekee, bali uwezo wa kuongoza watu wakaamini katika unachofanya, even when hawalazimishwi.
 

Kuwajibika na kuchukua hatua kama mwanaume ina msingi, lakini inaonekana kama kutokulalamika kumechukuliwa kama kipimo pekee cha uanaume au uongozi, jambo ambalo si sahihi.

Kuna tofauti kati ya kulalamika bila suluhisho, na kutambua changamoto kisha kuishughulikia kwa akili.

Hata viongozi bora duniani wanatambua matatizo waziwazi kabla ya kuyatatua hiyo si udhaifu, ni ufahamu.

Unaposema mfumo dume una mamlaka na nguvu, hilo linategemea unavyo ufafanua.

Kama mamlaka inaishia kwenye uwezo wa kudhibiti na kukandamiza, basi hiyo si nguvu ya uongozi bali ni matumizi ya power bila balance ya hekima.

Uongozi imara hauogopi maoni, hauogopi kujitathmini, na hauhitaji kuthibitishwa kwa ukali pekee. Ndiyo maana hata mwanaume mwenye uthabiti na kujiamini anaweza kusikiliza, kurekebisha, na bado akaongoza bila kupoteza mamlaka yake.

Twende taratibu mkuu..
 
Mfumo dume kwa sasa ni mfumo chakavu ,ambao kwa sasa wanaouendekeza ndio walalamishi wa kubwa
Mfumo dume ndo mfumo sahihi kwa 💯%. Baada ya kuukataa mfumo dume, ndo mashoga na wasagaji wameshamiri. Mfumo dume ukisimama hutaona huo uchafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…