Naungana na jamii ya kimataifa kutompa ushirikiano mheshimiwa Uhuru Kenyatta

haya yote yanajitokeza ni kutokana na CHADEMA kuumbuka kwa kumsupport ODINGA. Ndiyo maana inaanzishwa mijadala ambayo haina tija kwetu ili mradi tu wanaonyesha hisia zao za kumpinga Kenyatta
 
Wewe ni nani hata tukuhitaji kumwunga mkono Uhuru? Kwenda zako huko!! Mbona hii kesi inaenda kujifia yenyewe tu na jamaa litaendelea kupiga mzigo? Hongera wa-Kenya kwa haya mliyoyafanya, mmefanya maamuzi ya busara. Nina mashaka na huyu aliyeleta uzi huu atakuwa ni Mjaluo huyu anaugulia maumivu ya kushindwa, na jinsi walivyokuwa wamejiandaa kuwanyanyasa Wakikuyu imekula kwao nyamb..ff!!

Mataifa gani ya nje yanakujua wewe sisimizi wewe? Unafikiri Kenya ni omba omba kama ninyi kila uchao Rais anaenda kutembeza bakuli? Tafuta historia ya Kenya waliwahi kufungiwa misaada lakini majamaa yakapeta zaidi ya miaka mitatu bila kutegemea wazungu, chezea Kenya wewe, wenzetu wako mbele hatua nyingi sana hatuwakuti!!
 
Naomba kuungana na jamii za kimataifa hususani Marekani ambayo tayari imetanabaisha kutoiunga mkono serikali ambayo Kenyatta atachukua nafasi kuiongoza.

Najaribu kubrowse ili nione sehemu serikali ya Marekani imesema haitoiunga mkono serikali inayoongozwa na Kenyatta, lakini sijafanikiwa. Tafadhali nisaidie source ya taarifa hii.
 

Uganda na Tanzania tatizo ni ufisadi na Rushwa, hasa hasa Tanzania ndiyo tumezidi sasa sijui maendeleo yatatoka wapi hata kama hao wamagharibi wanatusapoti.
 
Hiv baada ya kubainika kuna mahackers na Uhuru akiwa 43% vipi kura zilirudiwa kutoka 0% kuja mpaka hii 50% ama ilikuwaje

lile lilikuwa ni jaribio la akina odinga kutaka kuvuruga uchaguzi. walitegemea tume itakataa mannual counting ili wawe na visingizio kuwa uhuru ameshinda kwa wizi. hata kura ziliporudiwa kuhesabiwa walikataa na walishinikiza zianze kuhesabiwa upya kutoka katika vituo vya kupigia kura. walitaka pia tume isikamilishe kazi yake ndani ya muda uliowekwa kikatiba uli uchaguzi urudiwe tena. hila zao zote chafu zilishindikana mwa vile waliamua kuwa wakweli badala ya kulewa na unafiki wa kichama
 
Uganda na Tanzania tatizo ni ufisadi na Rushwa, hasa hasa Tanzania ndiyo tumezidi sasa sijui maendeleo yatatoka wapi hata kama hao wamagharibi wanatusapoti.


hivi unadhan tatizo la rushwa na ufisadi kenya halipo? hivi unalikumbuka lile sakata la grand regency hotel?
 
Big up Mkuu!! Umempa za uso huyu kifulambute!!!

Eti liungane na mataifa? Mataifa gani yanakujua wewe nyengurumbe wewe? Wakenya wameamua kuwakomoa Wazungu ili waone nini kitatokea sasa sisi tuna nini cha kulaumu hapo? Wazungu wenyewe kutalii wanategemea watumie uwanja wa JKIA sasa wataenda wapi? Uchumi wao nao uko ICU unafikiri watapenda kuipoteza Kenya kirahisi hivyo? Thubutu!!!

RAO mwenyewe alikuwa anamwogopa Uhuru tangu zamani ndo maana akashupalia ICC ili apate urais kwa mtelemko sasa mambo yamegoma anatapatapa tu!!

Hpngera Wakenya kwa maamuzi yenu sahihi!!
 
Mkuu Wakenya wameamua kuwaonyesha mabeberu ni wanafiki na unafiki wao hauna maana. Marekani kwa kumuunga mkono Raila (Binamu wa Obama) walitunga njama za kumfungulia kesi ya kubambikwa bwana Kenyatta na Ruto ili wasipate nafasi ya kugombea Urais. Haiingii akilini kwamba Kibaki along'ang'ania na Raila aliyekataa kushindwa na kuwa mwanzo wa vurugu za Kenya hawakufikishwa mahakamani! Ushindi wa UhuRuto ni pigo kubwa sana kwa wanafiki wa ICC pamoja na inafiki wa Marekani. Lile tamko lao lilikuwa la kuwatisha wakenya ila hakika nawaambia kama alivyosema Uhuru Muigai Jommo Kenyatta mtoto wa Mama Ngina, wazungu hawatathubutu kuiweka kando Kenya kwa kuwa wana maslahi mengi huko Kenya. Agwambo alie tu na mbinu zake chafu alidhani angeshinda kirahisi kwa sababu ya vurugu alizoziratibu kupitia pale Pentagon House.

Wakenya wameamua kujitenga na unafiki wa nchi za magharibi. HONGERENI WAKENYA NA HONGERENI JUBILEE ALIANCE. HONGERENI WANA DIGITAL DHIDI YA ANALOGIA
 
TATIZO AKIRI YAKO NI GANZI. Upo chuo bado hujitambui? Mbeya imekwisha kwa Mawazo haya.
 
hivi unadhan tatizo la rushwa na ufisadi kenya halipo? hivi unalikumbuka lile sakata la grand regency hotel?

jiran zako Uganda na Tz zinapendwa sana na Hizo jumuia but mpaka leo wanazungumzia ' kuhakikisha hakuna ataekufa na njaa' badala ya Maendeleo!

nilikuwa nakujibu hapo kwenye blue ulipokuwa unashangaa kama mkuu wa kaya kwanini Tanzania ni Maskini wakati tuna rasilimali lukuki, sasa naona unakuja na hoja nyingine kabisaa.
 

Bado unaamini marais wa Afrika huchaguliwa na wananchi!?

Nothing comes to a sleeping man but dreams-Tupac Shakur
 
watu wengine mkiwa na hangover msipost ----- humu
kanywe supu kwanza.
wakenya wameamua,ni ridhaa yao
hawajakubali kukumbatia ukoloni mambo leo.
sisi Tz tuamke pia tumwondoshe mkoloni mweusi CCM
anaedhani TZ ni yake milele.
 
Huyu kijana si unamuona mdomo wake lakini na macho? Kama wakimnyima misaada ataanza kusafirisha bangi nje na ataunga mkono el shabab
 
nilikuwa nakujibu hapo kwenye blue ulipokuwa unashangaa kama mkuu wa kaya kwanini Tanzania ni Maskini wakati tuna rasilimali lukuki, sasa naona unakuja na hoja nyingine kabisaa.

we ndiyo umekuja na mada mpya. tatizo la rushwa lipo hata katika nchi zilizoendelea kiuchumi barani afrika. nenda huko angola na nigeria
 
Wamarekani na waingereza ndo wameishika dunia, ukibisha mulize mwenzenu chavez alijifanya kidume kaishia wap??
 
Waziri wa mambo ya kigeni wa marekani ametuma salam za pongezi kwa kenyatta na wakenya wote kwa maamuzi sahihi waliyofanya. Wewe umepata wapi hiyo taarifa yako ya kimajungu?
 
kwahiyo hoja hapa ni ipi???kama hayajatoka mioyoni mwa wakenya yametoka wapi??fikiria mbali...wakenya washaamua...waacheni
Walitaka wapigane ili wapate mwanya wa kufanya vitu vyao. Hongera waKenya:yo:
 
Kabla ya kuongea kitu chochote kuhusu siasa za mataifa ya Magharibi, jaribu kwanza kufanya homework.

Mataifa ya Magharibi yako kama kinyonga. Yanabadilika kulingana na mazingira.

Cha kufurahisha kuhusu Kenya ni kwamba, Mataifa ya Magharibi ( USA and UK) wahaihitaji sana Kenya wakati Kenya haiwahitaji sana wao.

Usishangae utakapo anza kusikia kauli na mitazamo tofauti zikitoka katika vinywa vyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…