Naungana na wasioamini uwepo wa Mungu

Naungana na wasioamini uwepo wa Mungu

😁
 
Attachments

  • 1729537363971.jpg
    1729537363971.jpg
    218 KB · Views: 5
Jamani mimi naomba tu nielezwe
Kama Mungu ni mjuzi zaidi anajua kila kitu kwanini tunafundishwa kusali?

Kwanini Shetani amekosea kaletwa duniani bustanini EDEN alafu sisi tukikosea tunaenda motoni

Ibilis laanatullah kwa mujibu wa mafunzo ya uislam ameumbwa kwa moto sio
sasa siku ya mwisho atarudishwa motoni?
Tunafundishwa kusali kwa sababu ndiyo namna bora ya kuwasiliana na Mola. Akili haizaliwi ikiwa tayari imejengeka maarifa, bali inafundishwa kupokea na kutumia maarifa.

Uwepo wa Shetani duniani ni sehemu ya mpango mkuu wa Mungu kuutokomeza uovu mazima ulimwenguni kote.

^9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo Wake; maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.^ (Ufunuo 12).

Kwa nini mbingu ^zishangilie^ (aya ya 12) wakati Ibilisi ametupwa duniani? Na kwa nini panatangazwa wokovu wakati Shetani ametupwa duniani?

Jibu rahisi ni kwamba kutupwa kwa Ibilisi duniani ni hatua mojawapo katika utekelezaji wa lile anguko lake kuu la mwisho.

^Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.^ (Ufunuo 20:10).
 
Suala la kuumbwa ni mtambuka,hakuna muumbaji na ikiwa yupo basi naye atakuwa na muumbaji wake naye muumbaji wake atakuwa na muumbaji wake.............
Kwa ajili ya hoja, hebu tuseme uko sahihi. Kwa hiyo ulimwengu umetokana na nini? Kwa nini, kwa mujibu wa sayansi, kila dutu, ikiwemo miamba, ina chanzo chake?
 
Wengi wanaoamini Mungu yupo ni either kwa kuwa wanaogopa kuchomwa moto (kama walivyotishwa na wachungaji tokea utotoni) au wana uwezo mdogo wa kufikiria mambo kwa kina.

Pia, waamini wengi hawajawahi kusoma chochote kinachohusu dini zao nje ya yale yaliyo nje ya vitabu vyao vya kidini. Kwa kifupi, wana upeo mdogo sana wa mambo ya dini.
 
Ukiiwaza Dunia na kuangalia mienendo yake kwa umakini mkubwa na Kisha kutafakari.

Basi utagundua huyo Mungu kama anavyoelezwa na Vitabu vya dini hayupo na kama basi hana nguvu wanazomnasibisha.

Angalia mauaji hapo Sudan, Kongo, Ethiopia, Gaza na kule Ukraine(Ukirene).

Angalia shida wanazopata watu mbalimbali, wanaomba maombi hawajibiwi.

Magonjwa na Vita, mabalaa kama Vimbunga.

Hivyo Kuna asilimia zaidi ya 93% hakuna Mungu.
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Watu wanahangaika sana kumuongelea na kumuelezea Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe, kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe yeye kama yeye kwamba yupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe hadharani ajidhihirishe kama ana huo uwezo.
 
Kwa hoja zangu hizo dhaifu natangaza rasmi Mimi sio muumini wa dini yoyote Ile na siku nikifa mnizike KIMILA
Mwenzio alisema hivyo hivyo akaenda mbali akasema akifa tumchome moto watu wale wakamfuata wakampa dili la mamilioni baada ya akiulizwa anasema akifa azikwe km wanavyozikwa wazungu, Pesa ugumu wa maisha unaweza ukakufanya ufanye maamuzi ya kiduanzi Mimi sihami dini kwenda dini yoyote na sitaki mtu yoyote ajipendekeze kwenye dini na dini yangu ni upendo sio nyingine ni Upendo, sina mbambamba sijui mizimu matunguli ni yenu Mimi dini yangu ni upendo kuna Mungu hakuna Mungu Mimi dini yangu ni upendo
 
Sawa ila ndio hivyo...dini ni upotoshaji wa wadhi wadhi tunao fanyiwa...huku serikalini wakijitanabaisha kuwa Haina dini...sasa kama kweli dini ni kitu hai kwanini serikali isiwe na itikadi Kali ya Imani yoyote...!​
 
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Watu wanahangaika sana kumuongelea na kumuelezea Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe, kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe yeye kama yeye kwamba yupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe hadharani ajidhihirishe kama ana huo uwezo.
Huu ndio ukweli japo ni mchungu ila wafia dini watakuja kukupiga mawe...dini Zina himiza tutoe SADAka🤣🤣🤣🤣 tulitajirishe huku sisi waumini tukibaki na machungu yetu
 
Ikizidi 80 ni mateso tu. Ila Cha ajabu kwako Mungu hayupo. Ila Mizimu aka majini yapo. Hahahaaaaa. Mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu.
Mateso kwetu sisi mafukara unadhani mzee kikwete Ako na miaka mingapi kwa sasa...? Je kwake ni mateso...?
 
Mkuu umechagua sehemu sahihi.
Kuna kipindi nilikuwa mlevi wa dini, nilikuwa mtoa sadaka mzuri sana mpaka leo nazijutia hela zangu bora ningenunua hata nyama nikawape mbwa mitaani
 
Back
Top Bottom