Naungana na wasioamini uwepo wa Mungu

Kama ulikuwa unamwamini Mungu na unashindwa kuamini kuamini katika uwezo wako hapo ulikosea

God exist

But you need to get involved in things you love and being responsible for ur life 100%
 
Umeandika vizuri japo hasira imepelekea kuchanganya hoja. Dini zipo (kusanyiko la watu liaminilo jambo fulani). Kuhusu uwepo wa Mungu si hoja ya kujadili kati ya waamini na wasio amini. Mambo ya imani yataendelea kuwepo mpaka ukweli utakapo dhihiri. Ukiwauliza waumini watakwambia imeandikwa, fungua kitabu fulani. Lakini kuna mistari kamwe haisomwi kwenye mkusanyiko wa waumini, yana uongo ambao hata mtoto hawezi kukubali. Maendeleo ya science yakifika kiwango kikubwa uelewa kwa watu utaongezeka na kupata majibu ya maswali mengi yaliyokosa majibu enzi hizo na kubuniwa Mungu.
 
Kwani kweli alikuanayo hayo majini?
 
Angalia na hii:

Wengi wanaoamini Mungu hayupo ni ama wanadhani kwa kuung'ang'ania huo upotofu mno, basi kiaina utageuka kuwa ukweli (kama walivyofundishwa na wanafalsafa wapagani tokea utotoni mwao), au wana uelewa mdogo kiakili; au yote mawili kwa pamoja.

Pia wanadhani waumini hawajui kuhusu dhana potofu za dini au kwamba hawakuwahi kuwa wapagani kama wao kabla hawajaongoka. Kwa kifupi wanajidanganya na kudanganyika.
 
Maendeleo ya science yakifika kiwango kikubwa uelewa kwa watu utaongezeka na kupata majibu ya maswali mengi yaliyokosa majibu enzi hizo na kubuniwa Mungu.
Unaongea kuisifia sayansi kana kwamba yenyewe ndiyo imeumba? Ni sawa na kuitukuza fizikia eti kwa sababu roketi imepaa angani. Nonsense!

Msingi hasa wa hoja ni kwamba nini chanzo cha hizo nguvu ambazo fizikia ama sayansi zinajaribu kutufafanulia?
 
Angalia na hii:

Wengi wanaoamini Mungu hayupo ni ama wanadhani kwa kuung'ang'ania huo upotofu mno, basi kiaina utageuka kuwa ukweli.
Ukweli ni kwamba hayupo. Upotofu ni kuamini yupo wakati hauwezi kuthibitisha uwepo wake.
Haukujua kuhusu yeye mpaka walipokuja wakoloni fulani na kueleza hivyo.
(kama walivyofundishwa na wanafalsafa wapagani tokea utotoni mwao).
Atheist na agnostic hawafundishwi toka utotoni! Wanafundishwa wapi?

Ni kupitia fikra yakinifu za nje ya boksi, kuhoji na kutafuta maarifa ya ziada ndipo wengi huishia kuukataa uongo wa dini kuhusu mungu na sifa alizopewa kwa hadithi za vitabu kama biblia na kurani.
au wana uelewa mdogo kiakili; au yote mawili kwa pamoja.
Mtu anayefahamu kuhusu mungu mmoja wa dini mmoja kati ya maelfu ya dini na miungu duniani ana uelewa finyu mno. Huwezi linganisha na mtu aliyechukua muda wake na kufanya upembuzi wa dhana za dini mbalimbali kwa kina.
Pia wanadhani waumini hawajui kuhusu dhana potofu za dini au kwamba hawakuwahi kuwa wapagani kama wao kabla hawajaongoka.
Mlikuwa wapagani wapi wakati akili zinafunguka mshabatizwa nakuwa indoctrinated?
Kwa kifupi wanajidanganya na kudanganyika.
Kwa kifupi watu wa dini wengi wapi ndani ya mfumo ulioundwa kuwadhibiti, hawajawahi kujihoji kuhusu wanachoamini na wanaogopa hata kuwaza against Imani zao wakisema ni kukufuru.
Hata penye contradiction ya wazi, nafsi itamsuta na hofu itamvaa kuukubali ukweli.
😊
 
Kwahyo mtoa mada hyo pumzi unayovuta umepewa na mizimu ya kwenu? Umewahi kuuliza mizimu yako kwanini ipo hvo?Umewahi kuuliza mizimu yako kwanini jua linachomoza mashariki na kuzama magharibi kupelekea usiku na mchana je inaweza kubadili jua kuchomoza magharibi?Umewahi kuuliza mizimu yako inauwezo wa kuzuia kifo?Usijifunze sehemu moja hebu jifunze na kwingine upate uhalisia ulivo.
 
Bora hata niliamini Jua Lina matokeo yanayoonekana ila kuhusu swala la Mungu ni mtambuka sana
 
Kama ulikuwa unamwamini Mungu na unashindwa kuamini kuamini katika uwezo wako hapo ulikosea

God exist

But you need to get involved in things you love and being responsible for ur life 100%
God doesn't exist.... without research no right to speak
 
Mkuu umechagua sehemu sahihi.
Kuna kipindi nilikuwa mlevi wa dini, nilikuwa mtoa sadaka mzuri sana mpaka leo nazijutia hela zangu bora ningenunua hata nyama nikawape mbwa mitaani
Kaka Bora ungewekeza kwenye kilimo kinge kulipa kuliko kutoa SADAka...! Bora ungewapa masikini Moja kwa Moja wange kushukuru na universe ingekuridishia fadhira...!
 
Tatizo linalokusumbua ni uchanga katika imani.
Hao wachungaji kuwa hivyo ni Mungu mwenyewe kaamua ila nawao walipitia Maisha magumu kama hao wa chini.
Wamepanda hapo kwasababu ya Mungu.
 
Ha
Haya mambo yanafikirisha sana mi naona Kila mtu abaki na mtazamo wake
 
Tatizo linalokusumbua ni uchanga katika imani.
Hao wachungaji kuwa hivyo ni Mungu mwenyewe kaamua ila nawao walipitia Maisha magumu kama hao wa chini.
Wamepanda hapo kwasababu ya Mungu.
Wewe hutamani kuwa kama wao...! Ebu nionyeshe nyumba ya Ibada ambayo haihubiri SADAka niwe naenda...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…