Nauponda sana upinzani ila nikitaka kuisifu CCM nafsi yangu inanisuta

Nauponda sana upinzani ila nikitaka kuisifu CCM nafsi yangu inanisuta

Huko Uganda wapinzani wangekuwa na nguvu ya kupambana hivyo usemavyo, Museveni angekaa madarakani zaidi ya miaka 30?
Wapinzani wa Uganda wamewazidi Kwa mbali sana Hawa wetu kiupambanaji
 
Maendeleao hayana chama , achana na mambo ya vyama penda nchi yako.
Kwenye vyama utakutana na wasaliti waliochangamka akina Lisu
Mi nakuhakikishia kama hivi vyama vilivyopo vingetangaza kujifuta hata kesi ya kama za kina mdee zingekufa juu kwa juu. Tatizo ni kwamba ccm wanajisifu sana huko nje kwamba Tanzania tuna demokrasia ya vyama vingi wakati wanajua fika hivyo vyama vyenyewe wamevitia mfukoni.

Kwa hiyo ccm wamevigeuza vyama vya upinzani kama pori la kuombea mikopo
 
Wapinzani wa Uganda wamewazidi Kwa mbali sana Hawa wetu kiupambanaji

Ukienda Uganda wapambe wa Museveni wanasema kuwa wapinzani wa huko ni dhaifu sana, lakini ajabu huo udhaifu wa wapinzani unapimwa kwa kutumia ukandamizaji wa vyombo vya dola na sio ushindani wa kisiasa.
 
Kama hali ni hiyo wapo pale kufanya nini si wastaafu siasa ijulukane nchi haina upinzani ili tuanze upya kudai demokrasia kuliko kuwa na wapinzani ambao wana uhakika kuwa hawafurukuti

Ww ndio dhaifu, umebaki unalaumu vyama visivyo na silaha katika kupambana na vyombo vya dola, wakati huohuo ww umeshindwa kuanzisha hata chama, ila unataka vilivyopo vife ndio hicho chako kianze!
 
Kwakweli nilitarajia kutokana na ardhi tuliyojaaliwa, hali ya hewa ya kuridhishi, mito, mabonde mazuri, maziwa, mabwawa, bahati, misitu nk. Tungekuwa tunalisha ukanda wote wa Africa mashariki na kati Kwa 100%.
CCM ishajichokea, lazima tubadilishe katiba ili tupate mfumo mwingine mzuri wa uongozi wa taifa letu. Ukiniuliza leo nini ajenda ya kisiasa ya taifa letu nitakwambia - KATIBA MPYA, KATIBA MPYA KATIBA MPYA.

Hata uchaguzi wa 2025 hauna maana yoyote ile - ajenda ni KATIBA MPYA kwanza na ni leo leo leo.
 
Ukienda Uganda wapambe wa Museveni wanasema kuwa wapinzani wa huko ni dhaifu sana, lakini ajabu huo udhaifu wa wapinzani unapimwa kwa kutumia ukandamizaji wa vyombo vya dola na sio ushindani wa kisiasa.
Wapinzani wameunga juhudi lawama zinaenda kwa aliyowanunua, wengine sasa hivi hawakosoi tena wamekaa kimya lawama zinaenda kwa wananchi kwamba sababu ni wajinga na waoga.
 
Mnaoulalamikia upinzani mlifanya nini
Mbowe alipowekwa magereza karibu mwaka mzima na Lissu alicyochungulia kaburi?
Kila siku huwa unasema upinzani dhaifu, lakini kinachowafanya wawe dhaifu hukisemi.

Ni kama vile unalalamika kila siku unalo tatizo usilojua chanzo chake, ndio maana unachanganyikiwa, na kichwa kitaendelea kukuuma tu.
 
Back
Top Bottom