Nawadharau sana Waingereza kwa kuendeleza utawala wa Kifalme

Uongo mkubwa ulioandika kwa unadhifu sana

1. Ufalme hakuwahi kuja au kuwepo sehemu kwa watu kuuchagua. Ufalme ulikuwa unaibuka na kujisimika kwa vita, nguvu na kumwaga damu. Hakuna mahali jamii ilichagua kuwa na wafalme dunia hii. Ni ujuha kusema Jafferson aliwaambia Wamarekani wasiige kuwa na ufalme kama Ulaya. Kwanza vita vya uhuru vya Marekani vyenyewe vilikuwa ni kuondokana na Ufalme.
 
2.Ni ujuha kufikri Wamarekani wameiga mambo ya Mongol empire,
Kama kuna Empires ambazo zilifanikiwa sana kidunia "global empires" ni British Empire na Spanish Empires ambazo zilikuwa za kidini kabisa. Hizo ndizo global Empires zilizoacha legasi kubwa na ya kudumu DUNIANI KOTE.
Mambo ya kidini hayakuingia kwenye katiba na mifumo ya Marekani kwa sababu founding fathers wake wengi walikuwa na imani tofauti na wengine hata imani zao halisi hazijulikani mpaka leo, pia wahamiaji wengi waliokimbilia katika makolini ya US kutokea Ulaya walienda kutafuta uhuru mkubwa zaidi wa kidini, Common sense tu ingekuambia kuingiza mambo ya dini kungeleta mvurugano na hivyo busara ilikuwa kuyaeupuka masuala ya dini.
 
Naunga mkono hoja. Yaani eti kuna familia haifanyi kaI yoyote inaabudiwa na kulindwa na waingereza wote. Bure kabisa hwa watu
Wameipata hiyo nafasi kwa njia ya upanga sio zawadi , baba wa eliza aliefarik jana aliuwawa kwa kukatwa kichwa
 
Kuamini kizazi cha mtu mmoja ndio kinafaa na kinastahili kuongoza watu katika taifa fulani, kwangu ulikuwa ujinga wa mtu wa kale na ni miongoni mwa mambo ambayo binadamu wa leo ambae tunaamini yuko civilised,
Salary Slip , Uko sahihi kabisa. Huu utawala wa kizazi kimoja wa kifalme, tunao vile vile kwa nchi zetu ambazo ni highly undemocratic. Muundo wa kifalme uko kwa njia nyingine ya mlango wa nyuma. Kikundi kidogo cha watu wa CCM kwa mfano, kinajiweka madarakani kwa kutumia nguvu za dola na hivyo kuwatawala watanzania kama malkia anavyowatawala waingereza kwa kutumia kikundi cha familia yake. As long as hakuna demokrasia, basi utawala wa kifalme kwa njia ya mlango wa nyuma iko pale pale.
Unapokuwa na Imperial president aliyewekwa na Katiba mbovu ya CCM/Nyerere, huo ni ufalme sawasawa na wa Kifalme wa Uingereza.
kabudi anafika mahali anamuita Magufuli Mungu! Ndio ufalme wenyewe...
 
3.THE ELECTORAL COLLEGE haikuweka ili kuhakikisha serikali ya US haishikiliwi na wajinga wajinga tu (Demagogues). Huu ni uongo mkubwa na hapa nakufananisha na wale ma DJ watafsiri wa movies za vibanda umiza. Electoral College iliwekwa ili kushawishwi majimbo madogo nayo yaingie kwenye federation na kuleta utangamano kwa kuyahakikishia kura zao zitakuwa na uzito na hayatamezwa na majimbo makubwa yenye idadi kubwa ya watu katika federation.
 
Waingereza wenyewe hawana neno juu ya utawala wao, wewe Mtanzania uliyeko hapo itigi uliyeshiba makande unawakosoa.
 
Kabla ya kudharau take trouble kujifunza huo utawala uliwatoa wapi na kuwafikisha wapi
 
4.Ni ujuha na upotoshaji kusema Marekani ina "Imperial Presidency"/ Urais wa kifalme.
Kama kuna taifa ambalo Rais wake ana check kubwa kutoka mihimili mengine ni Marekani,
Bunge na Mahakama ya Marekani vina nguvu kubwa kuliko sehemu yoyote nyingine duniani na vinaweza kukwamisha au kuzuia ajenda, bajeti, miswaada na sera kubwa za Raisi wa Marekani zinapokuwa kinyume naye.

Rais wa Marekani hata katika uteuzi wake wa viongozi wa taasisi zote unadhibitiwa vikali sana na Seneti ndio maana huoni akiteua au akifukuza watu muhimu serikalini hovyo. Biden amekaa mwaka mzima bila kuwa na uwezo wa kubadilisha mkuu wa shirika la Posta asiyependwa na Wademokrati wenzake
Hapa bado sijazungumzia mfumo wa majimbo ambao katiba haimpi ruhusa Rais ya kuingilia mamlaka zake.
 
Kwanza jielewe wewe,
Nchi yako,ina maziwa,mito,ardhi kubwa yenye rutuba,lakini inapewa msaada wa pesa na Japan wa kununulia chakula!!tunapewa msaada wa chakula na nchi za kiarab zilizopo jangwani!!ni nchi ambayo waziri wake anaenda kukutana na waziri wa nchi fadhili Ili kuomba mkopo,waziri wa bongo anaenda na V8 la milioni 400!waziri mtoa pesa anakuja na baiskeli!!!
Ishangae nchi yako,Raisi anatumia msafara wa magari 60!!
 
Bajeti ya kutunza hiyo familia miak nenda miaka rudi inabebwa na nani kama sio walipa kodi wa Uingereza?
Ndugu yangu huko usiende. Si bora hata hiyo budget inayotunza familia ya kifalme maana hapo kuna waingereza wengi watanufaika kwa kupata ajira, biashara ya ndani na maisha ya ya watu wengi sana yataneemeka.
Lakini jiulize hivi walipa kodi wa Uingereza no nchi zingine wanaoichangia budget ya nchi hii almost 60% na wakafahamu matumizi ya kijinga na ufujaji unaofanyika hapa kwetu watajisikiaje?
Mimi nadhani kama tunawa hurumia UK tax payers, tuwashauri waache kuipa misaada ya kibajeti ya serikali ya CCM kwanza kabla ya kuingilia maisha yao ya ndani maana wanayafurahia na haijapata kuwa mzigo kwao.
 
Hapo Chadema hamna Mfalme?
Nadhani umefika wakati upewe utambuzi wa jitihada zako za kuibadili JF kutoka kuwa "The home of great thinkers" na kuwa "The house of Comedian".
Ila sijui kama utafanikiwa maana kuna watu wamewekeza kuifanya JF itambuliwe ilivyo sasa.
Mtu mwenye akili timamu huwezi kuwa unatumia 2/3 ya muda wako kuwa JF na kuandika mizaha tuu.
 
Very poor timing ya hiki ulichoandika hapa, expect the backlash hata kama una hoja.
Mmechotwa akili na wazungu na kuamini kila chao ni bora wakati nyie leo hii tawala zenu za kina Mkwakwa na wengineo mnazidharau. Sisi ni mavichwa ya kushikiwa. Tumetawaliwa mwili hadi akili..
 
Hilo ni chizi
 
Mbona umeishia kutoa ngonjera za kwenye vijiwe vya kahawa badala ya kutoa japo elimu kidogo ya kile unachokijua?

Itakuwa umememezeshwa na teja mwenzio hicho ulichoandika lkn huna unachokijua na hujui kwamba hujui
 
Wameipata hiyo nafasi kwa njia ya upanga sio zawadi , baba wa eliza aliefarik jana aliuwawa kwa kukatwa kichwa
Kwahiyo? Wanajeshi wangapi wanauawa vitani mbona familia zao hazipewi hiiyo hongo ya uongozi wa kudumu?
 
Nani anapokea rambi rambi ya msiba wa malkia Elizabeth? Tujitahidi kuchangia, wasije wakashindwa kusafirisha na kuzika mwili wa mpendwa wao.wana JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…