Nawadharau sana Waingereza kwa kuendeleza utawala wa Kifalme

Fikiri vizuri heri ufalme kuliko huu wa kwetu maigizo kibaooo na gharama nyiiiingi kufanya uchaguzi kumbe wanapeana wenyewe kwa wenyewe
 
Mbona nyie mmeikumbatia CCM miaka karibu sitini, huoni kwamba mnaelekea huko huko kwenye utawala wa kifalme?
 
Ni biashara tu ,
before pandamic (COVID) Forbes walisema Royal family wali contribute $28 Billion to Britain's economy.
 
Utawala wa kifalme uingereza hauna athari yoyote as long as democrasia yao ipo imara. Kiongozi wa kifalme ni ceremonial leader, hana mamlaka yoyote ya kiutendaji.
Hapo kwenye "hana mamlaka yoyote ya kiutendaji " umemaanisha nini mkuu?

Juzi tu nimemsikia kikeke akisema ili iwe sheria pale uingereza ni lazima isainiwe na malkia..
 
Nimekuja Manchester nimempa pole mzee wa kizungu anasema wala sioni uchungu kwa kifo chake na wengi hatuwapendi
Wanajilimbikizia hela zetu za kodi
Anasema watu wengi watakuja kuzika na kila kitu kitapanda bei na Hotel zao ndio zitafaidi

$28b thamani ya majumba yao na mali
Charles ana $400m bado za urithi wa mama sasa
Ila kwa mimi siwachukii na nipo hapa miaka kibao
 
Hapo kwenye "hana mamlaka yoyote ya kiutendaji " umemaanisha nini mkuu?

Juzi tu nimemsikia kikeke akisema ili iwe sheria pale uingereza ni lazima isainiwe na malkia..
Umewahi sikia kagoma? Umewahi sikia kamkataa waziri mkuu?? Umewahi sikia kateua waziri mkuu kwenye chama chenye wachache bungeni? Ndio maana tunasema ni ceremonial leader, mamlaka yote yapo mikononi mwa wananchi.
 
Ni Mtazamo wako lakini hata hapa kwetu TZ tuna viongozi wa makabila na wana nguvu labda useme ujui kwenu na kama ni kweli wewe ni hasara maana kuna faida kubwa sana kujua asili yako na mila zenu.
 
Ni ujinga kulipa kodi kwa familia eti sababu ni malkia na wafalme[emoji35] mbuta mbona sijaona wakiruka kama wao ni special beings?
Totally idiotic [emoji3062]
 
Mfumo wa utawala wa kifalme wa uingereza ni tofauti na vile wengi tunavyofikiria, pamoja na kuwa na ufalme lkn nchi Ina Serikali yenye mamlaka na inaongozwa na mihimili yote muhimu chini ya Waziri mkuu
 
Huelewei hata demokrasia ni nini ndio maana unaamini Uingereza, Scandinavian na US hakuna demokrasia ila bongo ndio kuna demokrasia ya kweli.
Poor.
Hebu Shusha madini hio demokrasia ya kweli 100% tuione
 
House of lords and commons zipo mpka leo ?

Bado vipo! Mabadiliko makubwa yaliyotokea ni yale ya 2009 kuitoa mahakama ndani ya bunge (House of Lords) na kuifanya ijitegemee yenyewe na kuwa mahakama ya juu ya Uingereza (The Supreme Court of the United Kingdom)......Zamani mahakama ilikuwa ni sehemu ya bunge na majaji walikuwa ni wabunge.....
 
Tena hii na madaraka juu.
 
Utawala wa kifalme uingereza hauna athari yoyote as long as democrasia yao ipo imara. Kiongozi wa kifalme ni ceremonial leader, hana mamlaka yoyote ya kiutendaji.
Tabu anakula kodi yao bure.
 
Ufalme ndo alama ya dola la kiingereza kipindi hicho imetawala dunia nzima, unaanzaje kuufuta ikiwa mwingereza bado anaendeleza ukoloni mamboleo kwenye maeneo yaliyokuwa himaya yake ambayo sasa anayaita commonwealth..​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…