Nawadharau sana Waingereza kwa kuendeleza utawala wa Kifalme

Acha upotoshaji, kililochokuwepo katika House of Lords ni kamati ya Rufaa ambayo ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi mbalimbali na pia watu kukata rufaa.

Kilichotolewa katika house of Lords ni hiyo kamati ya rufaa na ikaundwa mahakama kuu ya Uingereza ambayo ndio mahakama ya rufaa pia. Huku chini mahakama nyingine zilikuwa zinajitegemea kama kawaid.

Jambo lingine unalopaswa kufahamu Uingereza ina mfumo wa parliamentary sovereignty ambapo bunge linakuwa na mamlaka makubwa zaidi katika sheria, kanuni na miongozo ya nchi kuliko Mahakama na Serikali.

Bado vipo! Mabadiliko makubwa yaliyotokea ni yale ya 2009 kuitoa mahakama ndani ya bunge (House of Lords) na kuifanya ijitegemee yenyewe na kuwa mahakama ya juu ya Uingereza (The Supreme Court of the United Kingdom)......Zamani mahakama ilikuwa ni sehemu ya bunge na majaji walikuwa ni wabunge.....
 
Katika vitu ambavyo naviona ni primitive kwenye dunia ya leo, ni pamoja na Tawala za Kifalme.

Kuamini kizazi cha mtu mmoja ndio kinafaa na kinastahili kuongoza watu katika taifa fulani, kwangu ulikuwa ujinga wa mtu wa kale na ni miongoni mwa mambo ambayo binadamu wa leo ambae tunaamini yuko civilised, hapaswi kuyaendeleza.

Kwakweli Waingereza nimeshindwa kuwaelewa mpaka leo kukumbatia Ufalme.

Japo Uingreza ni taifa lililoendelea miaka mingi iliyopita, ila kwa hili la kulea Ufalme hakika nimewadharau na mpaka leo sipati majibu kwanini hawataki kuondokana na hii system iliyokuwepo hata kabla ya Yesu kuzaliwa.

Ina maana na Malkia Elizabeth alikuwa mfalme? Duh! Anyway endelea kuwadharau
 
Maisha ambayo yana usalama na uhakika wa kesho yangu kifedha
Una uhakika gani wa kesho wa masikini uliejaa shida lukuki.

Watoto wako ukute wanasoma shule za kayumba. Huna KAZI. Umepanga. Mwenye akaunti yako huna hata milion 50.

Masikini popote duniani Hana uhakika WA kesho yake
 
nchi Nyingi zenye Demokrasia ya kweli maendeleo watu ni madogo

1. Nchi za Scandnavia ambazo maendeleo watu ni makubwa wana wafalme, kina Norway, Denmark etc
2. Nchi za Gulf zina wafalme na Masultan
3. mashariki ya Mbali Japan utamkuta Emperor Naruhito

hata nchi ambazo unakuta wananchi wanachagua demokrasia inakuwa kama changa la macho Mfano Democrat na Republican una choice ya wawili tu, chagua left wing ama right wing huna choice ya kufikiria nje ya box.

njoo huku kwetu sasa, fujo pro max.
Tena kama marekani mnachagua alafu kuna kikundi cha watu wasiozidi 300 wanaenda kuchagua upya tena
 
Katika vitu ambavyo naviona ni primitive kwenye dunia ya leo, ni pamoja na Tawala za Kifalme.

Kuamini kizazi cha mtu mmoja ndio kinafaa na kinastahili kuongoza watu katika taifa fulani, kwangu ulikuwa ujinga wa mtu wa kale na ni miongoni mwa mambo ambayo binadamu wa leo ambae tunaamini yuko civilised, hapaswi kuyaendeleza.

Kwakweli Waingereza nimeshindwa kuwaelewa mpaka leo kukumbatia Ufalme.

Japo Uingreza ni taifa lililoendelea miaka mingi iliyopita, ila kwa hili la kulea Ufalme hakika nimewadharau na mpaka leo sipati majibu kwanini hawataki kuondokana na hii system iliyokuwepo hata kabla ya Yesu kuzaliwa.
Usiweweseke!
Baada ya maziko na ujio au kupanda cheo kwa Prince. Dunia inaenda kubadilika. Monarch ina 10-15yrs max. Usiweweseke wanaenda kuondoa imperialism.
Na sisi Waafrika tungo' ke COMMONWEALTH....Jumuiya ya Waliotawaliwa na kukubali kuendelea kutawaliwa, tungo'ke.
 
Tena kama marekani mnachagua alafu kuna kikundi cha watu wasiozidi 300 wanaenda kuchagua upya tena
Crimea: Ukiondoa Electroral College, basi Marekani ingetawaliwa na Candidates toka Los Angeles, New York, Chicago, na Texas, tu! Maana ndio wenye population kubwa. Hii ina maana States kama Iowa, New Hampshire na kama hizo ndogo ndogo Mgombea urais mtarajiwa hata asingezitembelea, maana hazina uzito! Electroral College ina fanya ziwe na sauti.
Mfano mzuri ni Kenya, Wakikuyu, Kalenjin na Luo ni lazima watakuwa wanatoa Rais! Makabila mawili yaki gang up basi makabila mengine madogo, hayana sauti! Lazima mgombea Kenya atoke Kabila mojawapo kubwa! Ndio maana umeona vyama vikubwa Kenya lazima Mkikuyu, Luo au Kalenjin awepo! Ni itaendelea kuwa hivyo.Lazima wafanye utaratibu wa kurekebisha hilo. Makabila madogo kila siku yatakuwa ni wasindikizaji.

Sisemi kuwa system hii haina mapungufu, inayo sana. ( labda siku nyingine tutazungumzia hilo) Lakini kuzifanya States zote zijione zina nafasi katika kutafuta kiongozi mfumo huu unafaa Marekani.

ingawa lazima tukubali kila mfumo wowote wa utawala unategemea sana jadi na historia ya taifa hilo! Kumbuka Marekani ina miaka mingapi toka iwe taifa, kuna proposals nyingi zimejaribu kutaka kuundoa au kuurekebisha mfumo huu, kila pendekezo linaonekana linakuja na mapungufu yake, na litashindwa kuleta mshikamano wa utaifa.
 
Maajabu mtanganyika anaidharau nchi ambayo inamsaidia Hadi hela ya kununua dawati za wanafunzi.

Miaka 60 ya Uhuru bado watu wanaumwa malaria, huu muda WA kudharau system ya kifalme na kimalkia ya Uingereza ungeitumia kupendekeza namna gani ya kuiboresha nchi yako
Lunatoc:
Hata kujifunza pia! Wengi hawajui pia hata hii Westminster Modal ya serikali zetu ni copy ya Uingereza, na kubambikiza ya kwetu.
Huo mfumo ambao tunajaribu kuukejeli ndio umepaisha uingereza toka 1700 ikatawala sehemu kubwa ya dunia.
 
Kwahiyo? Wanajeshi wangapi wanauawa vitani mbona familia zao hazipewi hiiyo hongo ya uongozi wa kudumu?
We takataka nani kuambiwa wamepewa? Hao wamepigana kuchukua eneo kwa jeshi lao wenyewe

Sawa na leo joseph konyi aingie madarakan utasema kuna wanajeshi bla bla, mtu amepigana akatwaa eneo hajapewa ni mali uake binafsi na kama unalitaka na ww kapigani

Ni kama saudia, wamepigana wakatwaa eneo likawa nchi wakiita jina la familia , Saudia
 
Mfumo wowote uimara wa kiutawala ni lazima uzingatie taasisi asilia (Local & Social Institutions) ambazo zimejengeka kwa muda mrefu ndani ya taifa husika. Hili la kuchukua na kuiga kila kitu kutoka mataifa ya nje ndilo linayagharimu mataifa mengi sana duniani. Jambo linaweza likawa zuri na likafanya kazi nchini Uingereza lakini lisiwe zuri nchini Tanzania. Ndiyo maana tunategemea wasomi wetu wa Tanzania wawe "Empiricists" huku wakiuliza swali hili kabla ya kufanya chochote kile "Will it work ??" and "And Why should it work ??"

Ukisoma historia ya katiba ya Marekani (Constitutional History of the United States) utafahamu kwamba waliiga mambo mengi sana kutoka nchini Uingereza. Kuanzia mgawanyo wa madaraka (Separation of Powers), mfumo wa sheria na utoaji haki (Legal System/The Common Law System) na mfumo wa haki za binadamu (Bill of Rights) lakini kuna mambo mengi hawakuiga. Wao badala ya kuweka Mfalme kama baadhi walivyotaka wenyewe wakaweka Raisi anayeteuliwa. Badala ya kuwa na dini ya taifa kama Uingereza (State Religion) wakina Thomas Jefferson wakaingia maktaba na kutafuta mfumo ambao ungelifaa taifa la Marekani.

Thomas Jefferson ndiyo aliyewashauri Wamarekani waachane na kuiga mifumo ya Ulaya na kuanza kusema Marekani ni taifa la kikristo. Hili alilifanyia majaribio alivyokuwa anaandika katika ya jimboni kwake Virginia. Kama wangeiga, hili la dini lingewavuruga kabisa. Jefferson akaamua kuiga mfumo wa Sheria wa Mongolia (The Ikh Yasa) uliotungwa na Tamujin a.k.a Ghengis Khan miaka zaidi ya 700 iliyopita. Ndiyo ukaona Marekani likawa ndiyo taifa la kwanza kabisa la Magharibi kuruhusu uhuru wa kuabudu (Freedom of Religion), kitu ambacho kiliwahi kufanywa na taifa la Mongolia peke yake.

Jefferson akaenda mbali zaidi na kuanzisha THE ELECTORAL COLLEGE ili kuhakikisha serikali haishikiliwi na wajinga wajinga tu (Demagogues). Eti kila mtu ambaye ni maarufu basi tumpe nchi kisa kapata kura nyingi. Hili limesaidia sana nchini Marekani kuwafunga spidi gavana baadhi ya watu. Sasa huku Tanzania utasikia mara, tuige Uingereza, tuige Marekani, tuige Singapore, na tuige hadi Kenya (Yaani Kenya ni ya kuigwa kweli ???), bila kujiuliza swali la msingi kabisa "Will it work here ???"

Sasa mlianza na Ujamaa, mkalimbikiza nguvu zote za dola kwa mtu moja (Raisi Mfalme/Imperial Presidency). Hili likawashinda vibaya na mpaka leo hii mnaisoma namba na mnataka Raisi apunguziwe madaraka. Lakini, kule Marekani Raisi Mfalme (Imperial Presidency) imefanikiwa vizuri sana kwasababu wana BUNGE na MAHAKAMA Imara, pia raia wengi wa Marekani ni watu wenye uelewa mpana wa mambo tofauti na Tanzania ambako vyama vinawaamulia raia kitu.

Mambo, kama haya ndiyo mnatakiwa wasomi myaangalie. Mimi sitawaambia ni mfumo upi unafaa kwa Tanzania, nilichofanya ni kutoa mwongozo tu. CHADEMA wanataka sera ya majimbo, tena wanataka na serikali tatu na wameigeuza hii kama ndiyo ajenda ya watanzania wote (Well and good. But will it work ??). Kule Marekani majimbo yalifanikiwa kwasababu zile zilikuwa ni nchi huru, huku mnataka majimbo yawe kimikoa na kikanda ambako bahati mbaya sana kila mkoa hukaliwa na kabila fulani.

CCM wanataka Chama kushika hatamu (Party Supremacy) na kulimbikiza madaraka (Centralization) kama kule Uchina, lakini bahati mbaya sana hawana mfumo imara wa Serikali za Mitaa ( Local Government) ambao ndiyo chombo muhimu kinachofanya kazi kuhakikisha wananchi wa kawaida na viongozi wa huku chini wanafanya kazi moja kwa moja na Serikali Kuu (Central Government). Serikali za mitaa za Uchina zina nguvu kubwa mnoo na ziko huru (Autonomous) , ndiyo maana mfumo wao unafanikiwa. Sisi Tanzania kuna kipindi Mzee Nyerere aliamka amevurugwa tu akaamua kufuta serikali za mitaa. Baada ya muda yakamshinda akaamua kuzirudisha.

Raisi Magufuli naye akaamua kuzinyang'anya serikaliza mtaa mapato yake na kuyapeleka serikali kuu. Hapa unadhani serikali zitajiendeshaje ilhali mapato yake yote yanaenda hazina ???

Lakini, mbaya zaidi taasisi asilia (Local Chieftainship) ambazo ndiyo ziko jirani na watu zilufutwa na Mzee Nyerere ili kujenga Ujamaa. Nadhani hili halikuangaliwa kwa undani na mapana yake zaidi. Nasema hivi kwasababu Kama taasisi za kikabila ni kitu kibaya kwanini basi ubakize sheria za kikabila (Customary Laws) ambazo zinafanya kazi na kutumika mpaka leo hii ??? Kingine ni kwamba wanaotatua kesi za kikabila ni wasomi (Judges/Magistrates) wasio na ujuzi wowote ule kuhusu watu wa jamii husika, mbali na kusaidiwa na wazee wa baraza ambao hawana nguvu yoyote ile......

NB 1: Tukikata kutoka hapa ni lazima kwanza tuifahamu Tanzania hii vizuri na jamii yake, siyo kuiga-iga kila kitu tunachosoma darasani au kuoana kwenye televisheni, halafu tunataka kutengeneza A CARBON COPY OF FOREIGN MODELS. Mimi nawakubali sana wapinzani, lakini kuna wakati ukiwasikiliza wanaharakati wao unabaki tu mdomo wazi. Haya angalia kali ya leo aliyotuletea ndugu Salary Slip....

NB 2: Hivi unafahamu kwanini IRAN mbali na matatizo yao wanafanikiwa kuliko nchi nyingi za kiislamu ??? Ni kwasababu, tofauti na falme nyingine na mataifa mengine ya kiislamu, waajemi wametengeneza serikali mchanganyiko (A Mixed Government) ambayo inazingatia tamaduni za waajemi ambazo zimedumu kwa miaka zaidi ya 6000. Wamechanganya (Theocracy, Democracy and Aristocracy ). Tofauti na Saudi Arabia, Qatar au U.A.E ambako ni aidha utii SHARIA LAW au upigwe JAMBIA, Iran wameweza kuweka uwaiano mzuri biana ya sheria za dini na zile za kiraia.

Nchi kama hii ambayo kila mtu ana sehemu yake ni ngumu kuifanyia uzandiki (Subversion) na hujuma (Sabotage) za kisiasa. Khomeini kafa lakini nchi inadunda tu......Sisemi kwamba huu ndiyo mfumo sahihi (Ideal Model), lakini walau umeonyesha kufanya kazi kuliko mataifa mengine kama yetu ambapo Raisi akifa tu, anakuja mwingine na mambo yake. Mwishowe nchi inajaa vurugu na hakuna kinachoendelea. Hebu angalia kinachoendelea saa hizi hapa nchini.....
Mkuu uko vizuri[emoji3578]
 
Katika vitu ambavyo naviona ni primitive kwenye dunia ya leo, ni pamoja na Tawala za Kifalme.

Kuamini kizazi cha mtu mmoja ndio kinafaa na kinastahili kuongoza watu katika taifa fulani, kwangu ulikuwa ujinga wa mtu wa kale na ni miongoni mwa mambo ambayo binadamu wa leo ambae tunaamini yuko civilised, hapaswi kuyaendeleza.

Kwakweli Waingereza nimeshindwa kuwaelewa mpaka leo kukumbatia Ufalme.

Japo Uingreza ni taifa lililoendelea miaka mingi iliyopita, ila kwa hili la kulea Ufalme hakika nimewadharau na mpaka leo sipati majibu kwanini hawataki kuondokana na hii system iliyokuwepo hata kabla ya Yesu kuzaliwa.
Kwani hapa Tanzania watoto wa viongozi wakuu huwaoni kwenye nafasi kubwa za uongozi wa nchi. Unadhani we kapuku hapa Nchini ni rahisi mwanao kuwa waziri ? Yote sawa tu. Bora waingereza hawataki unafiki.
 
Unauelewa mpana sana. Asante sana.
 
Acha upotoshaji, kililochokuwepo katika House of Lords ni kamati ya Rufaa ambayo ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi mbalimbali na pia watu kukata rufaa.

Kilichotolewa katika house of Lords ni hiyo kamati ya rufaa na ikaundwa mahakama kuu ya Uingereza ambayo ndio mahakama ya rufaa pia. Huku chini mahakama nyingine zilikuwa zinajitegemea kama kawaid.

Jambo lingine unalopaswa kufahamu Uingereza ina mfumo wa parliamentary sovereignty ambapo bunge linakuwa na mamlaka makubwa zaidi katika sheria, kanuni na miongozo ya nchi kuliko Mahakama na Serikali.
Bwahahaha! Humu JF nzima hakuna mtu anayenipenda kama wewe aisee! Unajuwa mabandiko yako nilianza kuyapuuza tangu siku uliposhangaa UDSM kutoa shahada ya utabibu. Nikafahamu kabisa una shida kubwa....

Sasa leo ndiyo nikasema nisome unachoandika walau siku ile ulikuwa umepitiwa. Nilichokutana nacho kimenifanya nicheke, lakini kikubwa zaidi ni kiwango ambacho uko Obsessed na mimi.

Mara ya kwanza nilihisi labda wewe ni mwanamke, maana nimefuatilia na kushangaa kwamba kila nilichowahi kuandika humu JF lazima ulijibu. Kukusoma vizuri nikatambua kumbe wewe ni mwanaume. Nimeshangaa sana.....
 
Poor Malcom
House of Lords imebaki kama pambo tu, hata mishahara hawalipwi katika hilo bunge.
Aisee, this is more than an obsession. Ndani ya uzi huu tu, umenijibu mara 7. Halafu unachojibu ni kama unalazimisha niongee na wewe. Dude are you straight ???
 
tofauti ya utawala wa kifalme na utawala wa CCM ni kwamba utawala wa kifalme haupotezi gharama za uchaguzi
 
Katika vitu ambavyo naviona ni primitive kwenye dunia ya leo, ni pamoja na Tawala za Kifalme.

Kuamini kizazi cha mtu mmoja ndio kinafaa na kinastahili kuongoza watu katika taifa fulani, kwangu ulikuwa ujinga wa mtu wa kale na ni miongoni mwa mambo ambayo binadamu wa leo ambae tunaamini yuko civilised, hapaswi kuyaendeleza.

Kwakweli Waingereza nimeshindwa kuwaelewa mpaka leo kukumbatia Ufalme.

Japo Uingreza ni taifa lililoendelea miaka mingi iliyopita, ila kwa hili la kulea Ufalme hakika nimewadharau na mpaka leo sipati majibu kwanini hawataki kuondokana na hii system iliyokuwepo hata kabla ya Yesu kuzaliwa.
Unawadharau Waingereza kwa kuuenzi ufalme huku wao wanaouenzi ni matajiri na hawana shida ndogo ndogo. Ila wewe unayewadharau umejaa umaskini kwa wazazi wako, ndugu zako na nchi yako. Pumbavu!!!
 
Back
Top Bottom