Nawaheshimu sana walimu, lakini mwalimu yeyote akimfanyia mtoto wangu kama inavyoonyesha picha hii nitamtafuta kokote alipo tumalizane

UnamjuA Bruce Lee?
Sina cha kuongeza ila kama una Akili utajiongeza.
 
Mkuu; Kwanini usituambie kosa la mtoto ni lipi/nini?Au unalijua kosa lake? Naamini huyo mwl. sio kichaa na huenda ana watoto kama wewe. Unaijua au unafuatiliaga Tabia ya mwanao awapo huko shuleni?
Kama mwanao akigundua au pengine yuko huku Jf (hapo ni shule ya Sekondari)na akaisoma Mada yako jinsi ulivyotoa povu au kutema cheche, unadhani utakuwa umemjenga au ndo umemharibu jumla? Leo ni kwa Mwl.; kesho ni kwako wewe mzazi. Kwani kama hilo limekuudhi kiasi hicho kwanini usichukue hatua stahiki kwa huyo Mwl.? Mbona unataka kujichukulia Sheria mkononi boss?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…