Nawaonea sana huruma dada zangu. Kipindi wapo umri 25, uzazi upo rahisi kwao, hawapati wanaume wa kuwaoa. Wakifika 30s wakiwa na vihela ndio wanaolewa

Hawa viumbe tuwaombee tuu, tunawapitisha kwenye majaribu mengi sana kwa tamaa zao wanaishia kuharibikiwa
 
Hiyo sio rushwa ni uwezeshaji bana 😂😂
 
Jamii ambayo kutelekeza watoto ni deal of the day, sio jamii ya kuwapa wanawake pressure za kuzaa wakiwa wadogo. Percent nyingi sana za watoto wa Tz hawajalelewa kikamilifu na wazazi pande mbili. Bado anatokea mtu kushauri wanawake wazae kabla ya kujipata. Ni vile wengi wetu ni wanafiki (perfect wannabe) ila tungejaribu kuwa wakweli humu juu ya aina ya familia tunazotokea...... tungegundua suala la malezi bongo ni changamoto sana.

Dear women, kuzaa ni kuzuri zaidi ukiwa una uhakika wewe na mwanao/wanao mtaishije kabla ya msaada wa ME, hata kwenye ndoa kuna Leo na kesho na kesho hatuijui so jitahidi kuwa na kakitu. Ama sivyo utaishia kuwa bitter na kuwachukia wanaume wote kwa makosa ya mtu mmoja.

Yangu ni hayo.


 
Ukiwa above 35 tu Hospital wanakwambia viungo vya uzazi vimekomaa so unakua kwenye risk ya kupata changamoto wakati wa kujifungua
Hii ni fact ambayo wengi wanaikataa, hatulazimishwi ila kuzaa mapema ni bonus kwa afya ya mama na mtoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…