Nawaonya Yanga SC mapema kuhusu kujidanganya kuwafunga Club Africaine katika CAFCC 'Knockout Stage' kwa Mkapa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Acheni kabisa kujidanganya kuwa kwa kuwa Kipanga FC ya Zanzibar alitoka nao suluhu (sare isiyo na magoli) basi hawa wapinzani wenu Club Africaine ya nchini Tunisia mnawaweza na mtawafunga.

2. Dhambi ile ile mliyoifanya kwa Al Hilal FC kwa kuwadharau na kujiona ni wakubwa kuwa mngewafunga ndiyo hiyo hiyo mnairudia tena leo.

3. Kumbukeni hawa Club Africaine hawatokei katika Madafu Premier League yetu Tanzania yenye farasi wakubwa wanne au watano, huku wao na nchi yao wakiwa miongoni mwa nchi kubwa na iliyoendelea sana kimataifa hasa katika mchezo wa mpira wa miguu.

4. Kwa ubovu wa timu ya Kipanga FC ilikuwa ni lazima tu Club Africaine ya nchini Tunisia wabovu kama wao (kipanga) na hivyo watashinda kiuwepesi na hatimaye kuingia makundi ya CAFCL.

5. Mnaoidharau Club Africaine ya nchini Tunisia (kutokana na ujuha wenu) kumbukeni kuwa hawa wenzenu walishafika hadi fainali ya CAFCC je, nyie (Yanga SC) mmeshafika huko walikofika au hata tu kupasogelea?

6. Ninavyowajua Waarabu walivyo makini katika michuano hii ya Afrika watakuwa tayari wameshabeba video za mechi za Yanga SC na timu zingine ili kujipanga zaidi kuwakabili kimchezo na kiufundi. Ila kwa niwajuavyo Yanga SC kwa sasa kipaumbele chao ni udhamini wa UNICEF na kuchanja UVIKO - 19, kuiroga kuifunga Simba SC Jumapili ijayo, kujisahau na ushindi wa ligi nyepesi ya NBC Premier League na ikifika tarehe 30 December 2022 siku tatu kabla ya kukutana na hawa Club Africaine ndiyo Watazinduka na kuanza kujiandaa na wakitolewa kama kawaida, mbuzi wao wa kafara na kichaka chao cha kujitetea kitakuwa ni kumlaumu mwamuzi (refa) kuwa amewaonea.

7. Tayari waandishi wa habari, watangazaji na wachambuzi wa michezo wameshaanza kujipendekeza kwa Yanga SC na kuwa waongo dhidi yao huku wakiwadanganya kuwa Club Africaine ya nchini Tunisia ni nyepesi mno na Yanga SC atashinda tu kote kote, wakati kiuhalisia wana Yanga SC wachache wenye akili wameshakubali kuwa kwa kimataifa Yanga SC anakufa na michuano hii haiwezi.

Endeleeni tu kujidanganya sawa?
 
WACHEZAJI WENYE THAMANI
WA CLUB AFRICAIN

1. LARRY AZOUNI
Nafasi: Kiungo Mshmbuliaji
Thamani: 1.6B Tsh
Jezi: Namba 8
Miaka: 28
Aliwahi kucheza Marseille, Lorient, Nimes zote za Ufaransa pamoja KV Kortrijk FC ya Ubelgiji

2. AHMEDI KHALIL
Nafasi: Kiungo Mkabaji
Thamani: 1.3B tsh
Jezi: Namba 5
Miaka: 27

3.NADER GHANDRI
Nafasi: Beki wa Kati
Thamani: 1B Tsh
Jezi: Namba 6
Miaka: 27

4.SKANDER LABIDI
Nafasi: Mlinzi wa Kati
Thamani: 900M Tsh
Jezi: Namba 3
Miaka: 29

5. NOUREDDINE FARHATI
Nafasi:Mlinda Mlango
Thamani: 900M Tsh
Jezi: Namba 1
Miaka: 22

NB: Thamani ya mchezaji namba moja wa Club
Africain ni sawa kununua akina Aziz Ki sita

Tuna Wachezaji wa Gharamaaa
 
,hee,,hee,,hee,,,ukijumlisha na gharama za wachezaji wengine na gharama zote kikosi kinafika thamani ya 1.trilion

Huku Jangwani wachezaji wa bure free agent tunao kama wote.
 
Huyu jamaa kwa kiherehere hujambo. Mambo kajitungia mwenyewe halafu anawasingizia Yanga.
 
Kwa si ndiyo wewe uliyetabiri safari ile timu yako ya simba kufungwa na Nyasa Big Bullets!

Ni Mapopoma wenzako pekee ndiyo watakuunga mkono kwenye huu urojo wako.
 
Mkuu tarehe 23 inakaribia nakukumbusha utuletee na zile nyuzi zako za kuiba maiti kwajili ya mechi hiyo.
 
Yanga ina kaugonjwa kakujiita bingwa wa kihistoria. A.k.a wazee wa Unbeaten [emoji23] wanadhani michuano ya kimataifa wanaenda kucheza na Dodoma jiji.

Wakati wenzao wanaenda Sudan kucheza mechi za kujipima nguvu wao walikua wamejifungia kigamboni na kucheza na ngerengere Fc matokeo Yake chali.

Sasa wanarudia makosa Yale Yale. Ambayo mwarabu mweupe Hawezi kikuchekea Anakupiga Ndoige za USO [emoji23][emoji23][emoji23]

Hapo ndipo uvumilivu utakapo watoka nakuanza kufukuzana kama kawaida yao.
 
1. Acheni kabisa kujidanganya kuwa kwa kuwa Kipanga FC ya Zanzibar alitoka nao suluhu (sare isiyo na magoli) basi hawa wapinzani wenu Club Africaine ya nchini Tunisia mnawaweza na mtawafunga.

2. Dhambi ile ile mliyoifanya kwa Al Hilal FC kwa kuwadharau na kujiona ni wakubwa kuwa mngewafunga ndiyo hiyo hiyo mnairudia tena leo.

3. Kumbukeni hawa Club Africaine hawatokei katika Madafu Premier League yetu Tanzania yenye farasi wakubwa wanne au watano, huku wao na nchi yao wakiwa miongoni mwa nchi kubwa na iliyoendelea sana kimataifa hasa katika mchezo wa mpira wa miguu.

4. Kwa ubovu wa timu ya Kipanga FC ilikuwa ni lazima tu Club Africaine ya nchini Tunisia wabovu kama wao (kipanga) na hivyo watashinda kiuwepesi na hatimaye kuingia makundi ya CAFCL.

5. Mnaoidharau Club Africaine ya nchini Tunisia (kutokana na ujuha wenu) kumbukeni kuwa hawa wenzenu walishafika hadi fainali ya CAFCC je, nyie (Yanga SC) mmeshafika huko walikofika au hata tu kupasogelea?

6. Ninavyowajua Waarabu walivyo makini katika michuano hii ya Afrika watakuwa tayari wameshabeba video za mechi za Yanga SC na timu zingine ili kujipanga zaidi kuwakabili kimchezo na kiufundi. Ila kwa niwajuavyo Yanga SC kwa sasa kipaumbele chao ni udhamini wa UNICEF na kuchanja UVIKO - 19, kuiroga kuifunga Simba SC Jumapili ijayo, kujisahau na ushindi wa ligi nyepesi ya NBC Premier League na ikifika tarehe 30 December 2022 siku tatu kabla ya kukutana na hawa Club Africaine ndiyo Watazinduka na kuanza kujiandaa na wakitolewa kama kawaida, mbuzi wao wa kafara na kichaka chao cha kujitetea kitakuwa ni kumlaumu mwamuzi (refa) kuwa amewaonea.

7. Tayari waandishi wa habari, watangazaji na wachambuzi wa michezo wameshaanza kujipendekeza kwa Yanga SC na kuwa waongo dhidi yao huku wakiwadanganya kuwa Club Africaine ya nchini Tunisia ni nyepesi mno na Yanga SC atashinda tu kote kote, wakati kiuhalisia wana Yanga SC wachache wenye akili wameshakubali kuwa kwa kimataifa Yanga SC anakufa na michuano hii haiwezi.

Endeleeni tu kujidanganya sawa?
why unapoteza muda wako kwa yanga?
 
Back
Top Bottom