Nawashwa kwenye njia ya haja kubwa

Nawashwa kwenye njia ya haja kubwa

Pole sana Mkuu!.

Kitaalam kuwashwa sehemu ya haja kubwa (Pruritus ani) husababishwa na sababu kadha wa kadha.

Sababu kuu huwa minyoo. Matumizi ya viungo vingi kwenye chakula pamoja na utumiaji mkubwa wa pilipili huweza pia kusababisha kuwashwa kwa eneo hilo.

Unyevu unyevu sehemu ya haja kubwa inaweza kuchochea kuwashwa kwenye eneo la haja kubwa. Unyevu unyevu huo hukaribisha vijidudu na kupelekea kuwashwa.

Dalili za mwanzo za Bawasiri (Hemorrhoids) pamoja na anal fissures huenda ikasabisha kuwashwa kwenye eneo hilo.

Ufanye nini?
.Nenda hospital ukapime na kuangalia kama una minyoo. Daktari atakuandikia dawa kutokana na aina ya minyoo utakayokuwa nayo.

.Usafi binafsi kuhakikisha eneo hilo linakuwa kavu baada ya kujisaidia. Ukishaosha kwa maji, safisha kwa kitambaa kisafi au wipes nzuri. Nawa mikono yako kabla ya kutawaza. Usioshe kwa sabuni katika eneo hilo.

.Punguza kiwango cha matumizi ya viungo na pilipili kwenye mlo wako.

Endapo hali itaendelea, muone daktari kwa uangalizi zaidi!.

Pole sana.
 
Habari wadau.. Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu.. Nina kama mwezi sasa nasumbuliwa na kuwashwa kwenye njia ya haja kubwa.. Nimeshameza dawa za minyoo lakini tatizo bado lipo.. Kwahyo naomba mwenye kujua tatizo hili na dawa yake anambie..
nenda kwenye maombi haraka mzee, jini abubakar (jini popobawa) ameshakuingia, utakuwa unanyukwa usiku na mashetani bila wewe kujua. angalia wanaume wasikudanganye, kuwa makini tafadhari.
 
Yaan mi nilivyokuwa najikuna mpaka nasinzia kwa utamu......vidole havitakiwi viwe na kucha ili usijichubue tundu.Pole mkuu...tafuta sabuni uwe unaoshea
Mngh!!!! Ni ugonjwa gani mbaya sana huo, unajikuna mpaka unasinzia kwa utamu!!?[emoji15]
 
Back
Top Bottom