Mimi pamoja na familia yangu kwa dhati kabisa na kwa niaba ya Ukoo wangu wote ulio Kyela , DSM na nje ya nchi tunawatakia heri ya Mwaka mpya wanachadema wote , kwa maana ya viongozi katika ngazi zote na wanachama wote popote walipo ndani na nje ya nchi .
Imefahamika sasa Dunia nzima kwamba Chadema ni mpango halisi wa Mungu wa kupigania demokrasia , haki , heshima na Utu wa Mtanzania , katika hili hatuna wasiwasi nao hata chembe na nitakuwa mchoyo wa fadhila ikiwa nitashindwa kukishukuru chama hiki na kukiombea heri na baraka lukuki kwenye mwaka unaokuja , Chadema ndio nguzo ya demokrasia na amani .
Qurani tukufu imeandika kwamba , Nanukuu , " Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri " mwisho wa kunukuu .
Mungu ibariki Chadema .