Hayati baba wa Taifa, aliweka huu Muungano kwa kigezo kimoja kikubwa na muhimu sana, ambacho ni swala la usalama wa nchi, ukaribu tulionao katika ya Tanganyika na Zanzibari...tukiruhusu zanzibar iwe nchi huru ni wazi tutakuwa tumeacha wazi mlango muhimu sana, kama mnavyofaham nchi ikijitegemea ina kuwa na sheria na taratibu zake haziwezi kuingiliwa hivyo maharamia na wabaya wetu ni rahisi kutuathiri kupitia mlango huu muhimu. Ila tukizungumza tunachonufaika hakuna, zanzibari wananufaika zaidi na huu Muungano kuliko sisi watanganyika, hata umeme unaotumika Zanzibari unatoka Tanzania bara, ila kwa tulipofikia hatuna budi kukubaliana na hili, ila Angalizo serikali lazima waweke mikakati mizito sana kwenye mipaka ya bahari, maana kiuzoefu, ndio sehemu ngumu mno kuilinda na ni rahisi kuvamiwa na maharamia. Nawasilisha🙏