Nawaza ingekuwa Rais Samia ndio kasaini Mkataba wa SGR...

haawalioni hilo.

Makinikia hayo yakapanda meli yakaondoka. Yamepita hapo hapo bandarini au ndicho kinachoogopwa, yatabunburuka?
Samia na serikali yake ipo inafanyanini kama ujinga??
 
Wewe katika wale wapigaji na mnajuwa mwisho wenu kupiga bandari umeisha, tafuta kazi nyingine janja janja imefika mwisho mnataka hamtaki DP wanakuja ku operate.
 
Tena Mungu mkubwa sana, Kikwete tayari ile mikataba, SGR ilikuwa kishawapa China, Bwawa kishawapa Brazil, bandari ya bagamoyo alishawapa China na Oman, jamaaa alipoingia tu akaipiga chini yote.
Acha fix, hakukuwa na mpango wowote zaidi ya nia ya Mwl Nyerere. Hii miradi ni purely JPM initiatives. Hata kuhamia Dodoma mmejipa misifa tunawachora tu! Kila mtu ashinde mechi zake!
 
haawalioni hilo.

Makinikia hayo yakapanda meli yakaondoka. Yamepita hapo hapo bandarini au ndicho kinachoogopwa, yatabunburuka?
Nani kasaini mikataba inayoruhusu makinikia kuondoka
 
Shida ni viongozi wa CCM kusaini mikataba mibovu, siyo kusaini mikataba na Waarabu. Tatizo lako ni udini na kwa kauli zako inaonyesha una Uzanzibar fulani!!
 
Shida ni viongozi wa CCM kusaini mikataba mibovu, siyo kusaini mikataba na Waarabu. Tatizo lako ni udini na kwa kauli zako inaonyesha una Uzanzibar fulani!!
Kuwa na Uzanzibari ni sifa njema kabisa. Ni ustaarabu wa hali ya juu.

Mkataba upi mbovu?
 
Kuwa na Uzanzibari ni sifa njema kabisa. Ni ustaarabu wa hali ya juu.

Mkataba upi mbovu?
Faiza unauliza mkataba upi mbovu tena. SSH hakulalamikiwa kusaini mkataba kati serikali na DPW kwa Sababu ya Uzanzibar wake, wala dini yake au jinsia yake, hisipokuwa kilicholalamikiwa ni mkataba wenyewe. Mkataba wenye mashariti ya hovyo!! Unapotuambia SGR na Bwawa la mwl. Nyerere kwamba angekuwa amezisaini SSH pasingetosha una maana gani? Ubaguzi siyo?

Kama Uzanzibar wenu ni fahari, si tuachieni Utanganyika wetu. Wabara tumejitwisha mzigo usiokuwa na faida Ila basi tu D-Day is coming!!
 
Mama Samia hajasaini mkataba wowote mbovu, watu wana chuki kwa kuzibiwa mianya ya kuchota.
 
Mama Samia hajasaini mkataba wowote mbovu, watu wana chuki kwa kuzibiwa mianya ya kuchota.
Siyo kweli Foxy, labda uniambie, aliuziwa mbuzi kwenye junia na kwamba kuna mbinu chafu dhidi yake ndani ya CCM. Na kama mbinu ipo wanaotumika ni viongozi waandamizi serikalini, wanasiasa na washauri wake wa karibu. Kama kuna watu wanachota pale bandarini, si hao tunaopiga kelele kuhusu mkataba, bali wachotaji na wawezeshaji wa uchotaji huo ni haohao anaokula nao, kuzunguka nao na kucheka nao. Tunaomwambia ukweli ni siye tuliyoko pembeni.
 
Huo mkataba wa mauziano ni upi na uko wapi?
 
Miradi ya JPM imehujumiwa na cartel za mafisadi wa awamu ya sita hasa ya aliyekuwa waziri wa nishati anayetetea mazingira
 
Na majengo ya chuo Cha TANESCO morogoro yaliyotolewa na rais wa awamu ya tatu kuipa taasisi ya Muslim development inayosimamia Muslim university of morogoro (MUM) Majengo Yale yangetolewa na rais muislamu maaskofu wasingeandika waraka tu (KIPEPERUSHI CHA UDAKU ) Bali wangeandika biblia mpya!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…