Jamani nisaidieni na mimi nimsaidie huyu mwanaume
Tuna mahusiano inaelekea mwaka sasa lakini nashindwa namna ya kufanya ili kumsaidia huyu kijana
Jamani kijana ananuka mno mno mno mdomo kiasi kwamba najisikiaga mpk kutapika mpk nina mkwepa kuonana nae
Tangu mara ya kwanza nakutana nae alikuwa hivyohivyo nikafikiri labda sio msafi.. jamani kijana ni msafi sana sana anaoga mara nyingi kushinda mimi kwa siku anapiga mswaki Asubuhi na jioni
Hanuki jasho kabisa ila mdomo jamani
Kiasi kwamba akianza kuongea huwa nakwepesha sura kukwepa harufu ya mdomo wake hata kukiss huwa napata kichefuchefu nikitoka nalamba ndimu na yeye anapenda kulambana lambana inanikata kwakweli
Nataka Dawa ya kumsaidia sitaki kumuacha