Nawezaje kuacha kuishi na kinyongo kwa mtu huyu

Nawezaje kuacha kuishi na kinyongo kwa mtu huyu

Aaah wapi! Tena nahisi zamani walikulana kuliko sasa hivi maana walikuwa wanavurugana humu jukwaani balaa🤣🤣🤣

Walipangwa hadi sio poa.
Hukuwa mmoja wa waliokuwa wanavurugana?🤣
Kuna mtu niliwahi mwambia kuwa hizo "good old days" watu walichapana balaa.
 
Hukuwa mmoja wa waliokuwa wanavurugana?🤣
Kuna mtu niliwahi mwambia kuwa hizo "good old days" watu walichapana balaa.

Mimi sio mkongwe 🤣🤣🤣

Na walitifuana sana jukwaani.
 
nilikutana naye humu humu jamiiforums, nakiri nilimpenda sana sana anajua hili, ghafla tulitofautiana padogo bas akanibwaga,nikajaribu kumcheki kwenye email, hangout, sjui wasap kibaya akabadili id nakiri siijui id yake ya sasa,ila kwakipindi kile nilijitahidi kufanya jitihada nyingi mwisho nikawa naomba misamaha bas tuyajenge lakini mnajua mumivu ya kua ignored? hakuna majibu, sijjibiwa chohote nikajiongeza mtoto wa kike nikaendelea na maisha yangu, mwanzoni niliishi kwa tabu sababu bado nilijua kuna siku atanitafta ilipofika mwaka nikasema huyu si wangu tena.

nikaendelea na maisha yangu, et baada ya ten good fucking years huyu kiumbe amerejea with a just simple excuse, jaman sijalala nina hasira mpaka muda huu nawezaje kuondoa kinyongo nawezaje, najua utasoma hii thread, kinachoniumiza ni kuona naonewa mwenzenu, i tried to search a version of him kwa watu ambao nimekutana nao baada yake, hakuna aliemfikia, he was so special lakini kwa alionitendea sina ham naye

D, nilikupenda ukanilipa unayostahili, ni heri usingejileta umenifanya napata flashbacks kibao najitahidi kukusahau lakini nashindwa kinachoishi moyon mwangu ni hasira na chuki, nawezaje kuondoa hii hali wenzangu nisaidieni.
dah pole sana aise,
sio vizuri kabisa alichofanya jamaa, nichek inbo tuone namna ya kufanya, we will start with God, I hope linaisha hilo pole sana...
 
Miaka 10 bado mnatujazia threads?
Si mtoto angekuwa anamaliza shule ya msingi ?
I wanted to ask the same question, 10 good years na bado hana mtu! Haja move on, yaani ni kama alikua anamngojea mwamba arudi.

Ni maajabu.
 
kilichonifanya niumie yan the way mtu aanakubwaga bila sababu of course najua hanistahili hata hivo nimebeba ushaur wako
Sababu zipo ila silazima uambiwe. Halafu huwezi mchagulia mtu muda wa kukusamehe. Yaani kukosea ukosee wewe halafu unichukie mimi kwakutokukusamehe huo si utoto huo. Ukiharibu umeharibu huna haja ya kujitetea.
 
Naomba nikwambie ukweli huu mchungu Mwanaume hawezi kumuacha Mwanamke anayempenda kirahisi hawezi huyo wako hakuwahi kukupenda hata sasa alivyorudi.
Nakataa, namimi ni mwanaume. Yaani ufanye makosa useme kwasababu nakupenda basi siwezi kukuacha, labda kama sijapewa moyo wa nyama na nafsi. Wasioweza ni kijana ambaye bado hajakuwa na kuona mapenzi ni kila kitu wakati kuna maisha zaidi ya hayo.
 
sasa ndio huyo d et akanuna baba zima na ndevu zake kaa mbuzi maisha haya
Tatizo bado hamjifunzi, mipaka inawekwa ili iheshimiwe, wewe kwako ni madogo lakini kwake ni makubwa ila sijui kwanini mnapenda kuchukulia vitu for granted hasa kwaupande wetu wanaume. Ndio maana hata kuoa sikuizi mtu anaona ni upuuzi, everything is mind games to you. Bado hujajifunza na still unaliona hilo kosa dogo[emoji23][emoji23][emoji23]. Ukiwa na msimamo haki huwezi kuishi na mke.
 
Back
Top Bottom