Basi nyie wote mliopo hapa nawaona kuwa mpo positive, ni watu wenye maono mazuri, mna life purpose na mnajali maisha yenu na ya wapendwa wenu, huu ndio msingi wa brotherhood yoyote ile, hivyo nawaalikeni kama founder members of The Saturday Brotherhood!
Karibuni katika brotherhood yetu! Tuna mambo mengi sana ya kushirikishana kati yetu na kuwashirikisha wengine pia. Maisha ni kushirikishana shida na raha. Kati yetu asiwepo hata mmoja mwenye lolote linalomtatiza akakaa kimya. Tushirikishane vipawa vyetu, hali zetu, mali zetu na hata changamoto zetu.
Brotherhood is all about udugu nje ya ule udugu wa vinasaba, udugu wa kuzaliwa. Ni udugu wa kifikra, kiimani, na kihisia.
Udugu wetu ambao kwasasa unaitwa jina la mpito, The Saturday Brotherhood utaongozwa na
Duksi kama founder. Sisi wengine ni Co-founders. Karibu sana Duksi kuwa kiongozi wetu na hongera sana kwa wazo hili madhubuti!!!
Tunaweza kuanza kama a simple brotherhood na tunakua zaidi na kuwa chochote kile tunachopenda lakini tusisahau lengo letu la awali na la msingi, udugu.
Napendekeza kwamba tuwe na social group account kama vile WhatsApp au X (Twitter) na tuanze kushirikishana mengi. Kuna faidia kubwa sana katika udugu nasi tunapenda kuzijua faida hizo na kuzifaidi.
Tukifanikiwa katika hili, basi tutasajili brotherhood yetu na kuwa na utambulisho wa kisheria na kupanua shughuli zetu hata nje ya mipaka yetu! Tunaweza kuamua tunataka kufanya nini katika udugu wetu. Hakuna limit, lakini sisi tutachagua kilicho kizuri kwa watu wote na chenye kuleta manufaa zaidi.
Kwasasa tujuane zaidi, halafu tujue interests zetu na tuanze kushirikana tunu zetu. Baadaye tutatengeneza katiba ya udugu wetu.
Karibu kiongozi wetu Duksi, tafadhali endelea na kazi uliyoianza.
Karibuni The Saturday Brotherhood!
Asanteni
Fazili