Nawezaje kuanzisha Men Brotherhood? Kikundi cha wanaume cha kujengana?

Nawezaje kuanzisha Men Brotherhood? Kikundi cha wanaume cha kujengana?

Apo nimetisha wap mkuu? Au unafikiri neno kafara nilazima lihusishe maimani ya kishamba ya kichawi?

Kafara inaweza kuwa kujitolea na kupoteza mambo fulani mazuri ili uweze kukamilisha jambo fulani, mfano unaweza Acha kulala , unaweza Acha starehe, unaweza poteza marafiki, unaweza Acha kujali mwili wako , unaweza hatarisha hata uhai ili tu ukamilishe jambo fulani ,hiyo ni kafara .

Achana na hizo story za washamba za mambo ya adakadabra.
Hapo sawa nilijua ushawaza mambo ya sangoma
 
Wazo zuri , watu mkiungana huwa mnakuwa na momentum kuliko kuwa mmoja mmoja.

In life, when you need to get on top collaboration matter most.
 
View attachment 2962233View attachment 2962245
Wanaume kiasili ni wasiri na wasiopenda kuwa na urafiki au vikundi kama ilivyo wanawake. Pia wanaume wengi huweka vitu moyoni na sio rahisi kufunguka yanayowasibu, wengi hawaonyeshi hisia aidha za furaha au huzuni yaani ni stoic.

Lakini kwa upande mwingine mwanadamu ni kiumbe social anahitaji ile socialisation ili kuishi vizuri na kuweza kustawi hasa kisaikolojia na afya ya akili. Hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na marafiki wenye common interest wa kujengana na kuweza kupeana motisha na ushauri mbalimbali katika maisha ya kila siku.

Kukosa hili husababisha upweke ambao athari zake hazina tofauti na uvutaji sigara. Hili linatokea hasa kwa wanaume kuanzia miaka 30 ambapo kila mmoja anakuwa bize na majukumu yake ya maisha.

Baadhi wanatumia vikundi vya unywaji, wengine vikundi vya michezo kama mpira, jogging, michezo ya magari katika namna ya kupata hiyo brotherhood ambayo husaidia utimamu wa mwanaume. Wengine hujiunga katika vikundi vya kifamilia n.k.

Lakini wengine duniani huko wapo kwenye vikundi vya siri (secret society) ambavyo vimekuwa vikubwa na powerful kiasi cha kuogopwa duniani.

Vile vile kuwa na umoja hurahisisha mambo mengi kwasababu ya mawazo tofauti na pia "network" ya watu mbalimbali. Wahindi wanatumia huu mfumo sana kwenye jamii yao na hata biashara ambapo asimilia kubwa ya biashara za wahindi wanatumia mfano benki ya exim ambayo ni ya wenzao vivyo hivyo kwa huduma nyinginezo.

Sasa je nawezaje kuanzisha Brotherhood, ya watu makini kwa ajili ya kupata ule ukomredi ( camaraderie) na kupeana changamoto na support katika maisha ya kila siku hapa nchini??

Je vikundi hivyo vipo tayari nchini?
Mshirikisheni pia Pdiddy ili kuwe na tija.
 
Basi nyie wote mliopo hapa nawaona kuwa mpo positive, ni watu wenye maono mazuri, mna life purpose na mnajali maisha yenu na ya wapendwa wenu, huu ndio msingi wa brotherhood yoyote ile, hivyo nawaalikeni kama founder members of The Saturday Brotherhood!

Karibuni katika brotherhood yetu! Tuna mambo mengi sana ya kushirikishana kati yetu na kuwashirikisha wengine pia. Maisha ni kushirikishana shida na raha. Kati yetu asiwepo hata mmoja mwenye lolote linalomtatiza akakaa kimya. Tushirikishane vipawa vyetu, hali zetu, mali zetu na hata changamoto zetu.

Brotherhood is all about udugu nje ya ule udugu wa vinasaba, udugu wa kuzaliwa. Ni udugu wa kifikra, kiimani, na kihisia.

Udugu wetu ambao kwasasa unaitwa jina la mpito, The Saturday Brotherhood utaongozwa na Duksi kama founder. Sisi wengine ni Co-founders. Karibu sana Duksi kuwa kiongozi wetu na hongera sana kwa wazo hili madhubuti!!!

Tunaweza kuanza kama a simple brotherhood na tunakua zaidi na kuwa chochote kile tunachopenda lakini tusisahau lengo letu la awali na la msingi, udugu.

Napendekeza kwamba tuwe na social group account kama vile WhatsApp au X (Twitter) na tuanze kushirikishana mengi. Kuna faidia kubwa sana katika udugu nasi tunapenda kuzijua faida hizo na kuzifaidi.

Tukifanikiwa katika hili, basi tutasajili brotherhood yetu na kuwa na utambulisho wa kisheria na kupanua shughuli zetu hata nje ya mipaka yetu! Tunaweza kuamua tunataka kufanya nini katika udugu wetu. Hakuna limit, lakini sisi tutachagua kilicho kizuri kwa watu wote na chenye kuleta manufaa zaidi.

Kwasasa tujuane zaidi, halafu tujue interests zetu na tuanze kushirikana tunu zetu. Baadaye tutatengeneza katiba ya udugu wetu.

Karibu kiongozi wetu Duksi, tafadhali endelea na kazi uliyoianza.

Karibuni The Saturday Brotherhood!

Asanteni

Fazili
Nasubiri link ya whatsap ili nijoin
 
View attachment 2962233View attachment 2962245
Wanaume kiasili ni wasiri na wasiopenda kuwa na urafiki au vikundi kama ilivyo wanawake. Pia wanaume wengi huweka vitu moyoni na sio rahisi kufunguka yanayowasibu, wengi hawaonyeshi hisia aidha za furaha au huzuni yaani ni stoic.

Lakini kwa upande mwingine mwanadamu ni kiumbe social anahitaji ile socialisation ili kuishi vizuri na kuweza kustawi hasa kisaikolojia na afya ya akili. Hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na marafiki wenye common interest wa kujengana na kuweza kupeana motisha na ushauri mbalimbali katika maisha ya kila siku.

Kukosa hili husababisha upweke ambao athari zake hazina tofauti na uvutaji sigara. Hili linatokea hasa kwa wanaume kuanzia miaka 30 ambapo kila mmoja anakuwa bize na majukumu yake ya maisha.

Baadhi wanatumia vikundi vya unywaji, wengine vikundi vya michezo kama mpira, jogging, michezo ya magari katika namna ya kupata hiyo brotherhood ambayo husaidia utimamu wa mwanaume. Wengine hujiunga katika vikundi vya kifamilia n.k.

Lakini wengine duniani huko wapo kwenye vikundi vya siri (secret society) ambavyo vimekuwa vikubwa na powerful kiasi cha kuogopwa duniani.

Vile vile kuwa na umoja hurahisisha mambo mengi kwasababu ya mawazo tofauti na pia "network" ya watu mbalimbali. Wahindi wanatumia huu mfumo sana kwenye jamii yao na hata biashara ambapo asimilia kubwa ya biashara za wahindi wanatumia mfano benki ya exim ambayo ni ya wenzao vivyo hivyo kwa huduma nyinginezo.

Sasa je nawezaje kuanzisha Brotherhood, ya watu makini kwa ajili ya kupata ule ukomredi ( camaraderie) na kupeana changamoto na support katika maisha ya kila siku hapa nchini??

Je vikundi hivyo vipo tayari nchini?
Naomba nafasi ya uhasibu kwenye hiko kikundi kama kitaanzishwa!!
 
Ila wafanya biashara asilimia kubwa sio waaminifu
Imagne kimchina uwe nae kikoba
Kimchina hamna mtu pale yule ni jambazi 🤣🤣🤣
Ila amejiharibia na kapoteza wateja ambao baadae atawatafuta hatowapata tena. Pesa zina muda zikikimbia na wateja wakikukimbia hakuna rangi ataacha kuona.!!
 
Utakimbizwa.
Utaambiwa una element za wale wengine.
 
Bongo kama sio pombe hakuna cha maana kitachoweza kukutanisha wanaume.
 
Kimchina hamna mtu pale yule ni jambazi 🤣🤣🤣
Ila amejiharibia na kapoteza wateja ambao baadae atawatafuta hatowapata tena. Pesa zina muda zikikimbia na wateja wakikukimbia hakuna rangi ataacha kuona.!!
Yule dada amefingua ofisi china juzi
Yaani ana ujasiri alafu ni mwizi wa wazi wazi
Inahuzunisha
 
Yule dada amefingua ofisi china juzi
Yaani ana ujasiri alafu ni mwizi wa wazi wazi
Inahuzunisha
Kashajiharibia haitofanya vizuri labda km ataendelea na biashara nyingine anayofanyaga ya pembeni
 
au unataka uanze kuwa anko knowledge kama P.didy wa united state of america
 
Back
Top Bottom